HALICHACHI vs HALIISHI vs HATUPIMI, njooni tujuzane nani yuko pouwa hapa

Swizzy

JF-Expert Member
Nov 4, 2016
773
514
habari wanaJF!!!

Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza kumekuwa na makampuni mengi ya mawasiliano hapa Tanzania, hali inayo pelekea kuwa na ushindani mkubwa sana.

kwa upande wetu sisi watanzania ushindani unavyo zidi kuwa mkubwa hali ya unafuu wa gharama za mawasiliano zinakuwa afadhali kidogo kwa kukimbilia mtandao unao ona unafaa wewe.

Hivi Karibuni tumeona/kusikia kila kampuni imekuja na ofa yake ya maBANDO yasiyo kuwa na vikomo kama ifuatavyo:-
1. HALICHACHI (TIGO)
-Tsh1000 Dk20, SMS500, MB10 (SIKU 7).
-Tsh2000 Dk40, SMS1000, MB20 (BILA KIKOMO).

2.HALIISHI (VODACOM)
-Tsh1000 Dk23 (voda-voda), Dk2 (mitandao yote), SMS 50, MB5. (BILA KIKOMO)
-Tsh1000 Dk10 (mitandao yote), Dk2 (voda - voda), SMS 50, MB5. (BILA KIKOMO)
-Tsh5000 Dk125 (voda -voda), Dk10 (mitandao yote), SMS100, MB25. (BILA KIKOMO)

3. HATUPIMI (AIRTEL)
-Tsh1000 piga simu za Airtel to Airtel BURE, Dk10 (mitandao yote), SMS50. (SAA 24)
-Tsh5000 piga simu za Airtel to Airtel BURE, Dk50 (mitandao yote), SMS 500. (SIKU 7)
-Tsh10,000 piga simu za Airtel to Airtel BURE, Dk100 (mitandao yote), SMS 3000. (SIKU 30)

Haya sasa tusaidiane kujuzana hapa ni huduma ya mtandao upi bando lake la BILAKIKOMO lina unafuu kwa Watanzania wote?

na vitu gani viongezwe au vipunguzwe kwenye mtandao husika?. Ili wahusika watakapokuwa wanasoma huu uzi wakavifanyie kazi.

Mimi binafsi ningependa MB (Megabyte) ziongezwe kwa kila mtandao kwenye haya mabando (ya Bilakikomo), maana kwa hali iliyofikia sasa kwa watanzania wengi tuna tumia zaidi ya MB 200 kwa siku na nikiangalia hayo mabando juu wame bana sana kweny MB (Megabytes).

Unaweza ukaongeza mitandao mingine (Ambayo sija itaja hapo juu) kama nayo ina huduma ya BANDO bila kikomo.

...........TUSAIDIANE KUJUZANA HAPA ILI WAHUSIKA WATAKAPOKUWA WANA SOMA HUU UZI HABARI ZIWAFIKIE.........

[HASHTAG]#SWIZZY[/HASHTAG]
 
Bando iwe bila kikomo waache porojo wameshavuna sana faida. Wakati wa kurudisha faida kwa wateja wao sasa
 
Airtel Hana Bila Kikomo yeye Kaweka Bado Masaa 24.. Wiki na Siku 30. Sasa Hapo Bila Kikomo Kunatoka Wapi?

Naona Voda kawapiku Wengi.. ingawa in Reality huwezi kutumia Dakika hizo walizotoa Kwa Muda Mrefu. Nyingi Zinaishia Siku moja Au Mbili tu...
 
Hujui hawajamlimit mtu unapiga SAA 24 bila wasiwasi najua utakua na akili kwa sababu ya hii avatar
 
Hivi Mb 10 unafanyia nini?

Na nashangaa watu mnavyoshoboka!
Vifurushi vya masms na madakika havina mpango sasa hivi watu wanataka bando labda kwa ambao hawana smartphone.

Nashangaa mitandao ya simu imeshindwa kutambua soko kubwa liko wapi kati ya vifurushi vya kupiga na data.
 
wanajua kabisa tatizo lenu ni bando ndio maana wanabana ili wapatie pakufanyia biashara ukiwa na bando kwenye smart phone huhitaji sana sms maana kuna whatsaap na kuna wajana wakiwa na pando hawa hitaji dakika wanapigiana kwa mitandao yenye video call.
 
Hivi Mb 10 unafanyia nini?

Na nashangaa watu mnavyoshoboka!
Vifurushi vya masms na madakika havina mpango sasa hivi watu wanataka bando labda kwa ambao hawana smartphone.

Nashangaa mitandao ya simu imeshindwa kutambua soko kubwa liko wapi kati ya vifurushi vya kupiga na data.
Ndio maana hallotel wamewapatia sana
 
Kwa hili bando la airtel naweza nika mwambia bosi wangu akate nimpigie dah (angekua hum sipandishwi mshahara tena).
 
Back
Top Bottom