Hali yazidi kuwa tete mkoani Arusha, vurugu za madiwani sasa zahamia Arusha vijijini

Ukilaza wako unakuwasha huko kichwani, unachokitafuta hapo Ar hukipati ng'o, nimeshaujua mchezo wako!!
Mkuu nilichokua ninachokitafuta nimeshakipata.....kwani walimu wanalipwa madeni yao na huduma zinaboreka.
 
Hahahahah

Mheshimiwa sana kinena,
Posho za Madiwani zina taratibu zake kwenye Majiji na Halmashauri kulingana na sheria na taratibi za Serikali za Mitaa(Tamisemi). Huwezi kunishawishi kwa namna yoyote ile kwamba posho za madiwani zinapangwa baada ya Jiji au Halmashauri kupata fedha kutokana na sijui fidia au chanzo chochote cha mapato!
Ulicholeta hapa ni ushabiki wa kipuuzi ambao hauna tija yoyote kwa Serikali.Kumbuka kwamba Posho nyingi katika Majiji na Halmashauri zilipangwa na haohao ma CCM na ndiyo maana kwenye Miji na Halmashauri zinazoongozwa na CCM hatusikii kelele kuhusu posho!

Kilicho dhahiri mpaka sasa kwenye Utawala huu wa JPM ni mbinu za chinichini za kuminya posho za Madiwani na kuvuruga taratibu za ukusanyaji wa pesa ili kutaka kuonyesha Majiji na Halmashauri chini ya Upinzani hazi perform! Hii ni akili ya kipumbaf kwelikweli! Yaani unalazimisha eti wapinzani wasionekane kuwa wana perform simply because wewe CCM ulikosa Ubunge na Umeya!!!!!
Hii ni akili ya matope na kamwe hicho kinachosemwa Tanzania ya Magufuli ni viwanda sijui na upuuzi gani wa Bombadier ni sawa na kufukuza upepo! You won't achieve anything in your 5 years term!
 
Hawa madiwani wa Chadema wameingia kwenye zama za udhibiti sasa hawana namna ya kurejesha mikopo yao
 
Kila siku huwa nasema chadema ni wezi tu watu hawaelewi.Kitendo cha kufanya vurugu kulazimisha kujilipa pesa za fidia huo ni wizi wa mchana kweupe.
Mkuu hebu imagine Lowassa ndiye angekua rais leo.
 
Kikao kimevugika jana na barua imeandikwa na kufika wizarani jana hiyohiyo duu. Wizara siku hizi open 24hrs? Barua ilipelekwa na gari za magazeti naona.
 
ufipa hawaaminiki..kwao hata maprofesa huona nyeupe ni nyeusi..refer Lowasa presidential race...ni wapigaji kuliko hata lumumba...they don care...anyway ngoja ninywe lite zangu hapa..politics is crazy!!
 
hoja hapa sio njaa, kama hizo posho ni stahili zao , walipwe tu.

madiwani wote wanalipwa posho iwe wa CCM au upinzani.

CCM na Serikali pamoja na kukaa madarakani kwa zaidi ya miaka 50, they are totally immature
 
Jana 23 Desemba 2016 kikao cha kamati ya fedha uongozi na mipango halmashauri ya Arusha DC kiliishia njiani baada ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo Dk Wilson Mahela kulazimika kutoka nje ya kikao na wataalam wote baada ya mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri hiyo kwa tiketi ya Chadema kuibua hoja ya posho zilizokatwa kuwa zilipwe hapohapo. Posho hizo zilifutwa baada ya kugundulika zipo kinyume na utaratibu. Hali hiyo imekuja baada ya Halmashauri hiyo kupokea shs bilioni 1 na milioni 500 kama sehemu ya Fidia ya ardhi ambazo zinawachanganya madiwani hao wakitaka wazifaidi badala ya maslahi ya wananchi. Baada ya vurugu na kejeli ya madiwani hao dhidi ya mkurugenzi huyo ndipo alipoamua kuwaachia ukumbi ili watoe matusi yao wakiwa wenyewe. Madiwani hao wengi wao wakiwa ni CHADEMA waliingia na matarajio makubwa ya kujipatia kipato binafsi lakini kutokana na aina ya wateule wa rais waliopo ndoto zao hizo zimeyeyuka hivyo wanaamua kuanzisha migogoro isyo na maana ambapo wamemuandikia tuhuma 21 mkurugenzi huyo na kuziwaslilsha ofisi ya rais utumishi bila kuzipitishia mkoani kwa kuogopa kuwa RC Mrisho Gambo hataki majungu wala ujingaujinga. Mwezi uliopita madiwani wa Chadema wa halmashauri ya wilaya ya Meru walisababisha kikao cha kamati ya fedha kuvunjika kwa kutoa tuhuma kwa mkurugenzi mtendaji kuhusu masuala hayo hayo ya posho na kutaka kumjadili mkuu wa wilaya ambaye kiitifaki ni bosi wao. Baada ya mkurugenzi huyo kuwafafanulia kitaalam hawakumsikiliza wakavunja kikao.
MAONI
Madiwani wa Chadema waache njaa na wa tafuta kazi za halali za kuwapatia kipato .fedha za halmashauri ni za moto na ni kwa ajili ya maendeleo. Waache kuwatia tenda kuomba rushwa kwa wafanyabiashara wadogo na kuuza maeneo ya ardhi ambapo wengine waliopo jiji wamefikishwa mahakamani . KILA MTANZANIA MWENYE UWEZO WA KUFANYA KAZI MAAFANYE KAZI ILI TAIFA LISONGEBELE KIMAENDELEO. SIASA ZISUBIRI 2020
Tuma salamu kwa watu watatu.
 
Kikao kimevugika jana na barua imeandikwa na kufika wizarani jana hiyohiyo duu. Wizara siku hizi open 24hrs? Barua ilipelekwa na gari za magazeti naona.
Unajua kitu kinaitwa e-mail??....ama huko chadema mnasomea ujinga??
 
Unajua kitu kinaitwa e-mail??....ama huko chagadema mnasomea ujinga??
Sijuwi hicho. Duu mtumishi wewe noma oficial complain za serikali kwa email? Kweli propaganda unaziweza, lakini sie tunaojuwa taratibu za kiserikali tumekuelewa.
Kachukue buku 7 yako.
 
Sijuwi hicho. Duu mtumishi wewe noma oficial complain za serikali kwa email? Kweli propaganda unaziweza, lakini sie tunaojuwa taratibu za kiserikali tumekuelewa.
Kachukue buku 7 yako.
Mzee government inatumia emails officially....sio za domain ya yahoo au gmail
 
Back
Top Bottom