Hali yazidi kuwa tete mkoani Arusha, vurugu za madiwani sasa zahamia Arusha vijijini

kunena

JF-Expert Member
Nov 29, 2016
355
500
Jana 23 Desemba 2016 kikao cha kamati ya fedha uongozi na mipango halmashauri ya Arusha DC kiliishia njiani baada ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo Dk Wilson Mahela kulazimika kutoka nje ya kikao na wataalam wote baada ya mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri hiyo kwa tiketi ya Chadema kuibua hoja ya posho zilizokatwa kuwa zilipwe hapohapo. Posho hizo zilifutwa baada ya kugundulika zipo kinyume na utaratibu. Hali hiyo imekuja baada ya Halmashauri hiyo kupokea shs bilioni 1 na milioni 500 kama sehemu ya Fidia ya ardhi ambazo zinawachanganya madiwani hao wakitaka wazifaidi badala ya maslahi ya wananchi. Baada ya vurugu na kejeli ya madiwani hao dhidi ya mkurugenzi huyo ndipo alipoamua kuwaachia ukumbi ili watoe matusi yao wakiwa wenyewe. Madiwani hao wengi wao wakiwa ni CHADEMA waliingia na matarajio makubwa ya kujipatia kipato binafsi lakini kutokana na aina ya wateule wa rais waliopo ndoto zao hizo zimeyeyuka hivyo wanaamua kuanzisha migogoro isyo na maana ambapo wamemuandikia tuhuma 21 mkurugenzi huyo na kuziwaslilsha ofisi ya rais utumishi bila kuzipitishia mkoani kwa kuogopa kuwa RC Mrisho Gambo hataki majungu wala ujingaujinga. Mwezi uliopita madiwani wa Chadema wa halmashauri ya wilaya ya Meru walisababisha kikao cha kamati ya fedha kuvunjika kwa kutoa tuhuma kwa mkurugenzi mtendaji kuhusu masuala hayo hayo ya posho na kutaka kumjadili mkuu wa wilaya ambaye kiitifaki ni bosi wao. Baada ya mkurugenzi huyo kuwafafanulia kitaalam hawakumsikiliza wakavunja kikao.
MAONI
Madiwani wa Chadema waache njaa na wa tafuta kazi za halali za kuwapatia kipato .fedha za halmashauri ni za moto na ni kwa ajili ya maendeleo. Waache kuwatia tenda kuomba rushwa kwa wafanyabiashara wadogo na kuuza maeneo ya ardhi ambapo wengine waliopo jiji wamefikishwa mahakamani . KILA MTANZANIA MWENYE UWEZO WA KUFANYA KAZI MAAFANYE KAZI ILI TAIFA LISONGEBELE KIMAENDELEO. SIASA ZISUBIRI 2020
 

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
3,565
2,000
Wangekuwa wamechukua ikulu katika uchaguzi wa 2015 wangefanya hivi kweli? Yaani mzee Edo angekuwa anawaruhusu tu kugawana mipesa ya maendeleo ya wananchi kiholela namna hiyo? Wawe waungwana: posho za watumishi wa umma zina taratibu zake na kamwe diwani au mtumishi yo yote yule hawezi kujipangia kiwango chake cha posho. Laa sivyo bajeti yote ya serikali itaishia kwenye posho tu, jambo ambalo haliwezekani kwenye awamu hii ya kubana matumizi mbele ya Ngosha.
 

bushland

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
7,029
2,000
We kinena itakuwa wewe Ni Diwani WA ccm uliepigwa chini uchaguzi uliopita ndo mana Una hasira Sana, fyuuyyuuu
 

kunena

JF-Expert Member
Nov 29, 2016
355
500
sijakuona mleta uzi ila napata picha sura yako utakuwa umepaka wanja mweuusiii, una kipin puani, na umevaa blauzi kitovu kiko nje na kikuku mguuni. Na sikukuu hii unaonekana utaimalizia Shivaz.
Hahahahah
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom