Hali yawa tete kivuko cha ferry kigamboni

hsbaky

Member
Apr 29, 2009
25
6
Wadau,
Nawasalimu.
Wakati navuka leo asubuhi hii nimekumbana na adha ya kivuko pale ferry Kigamboni. Kwa sasa iko panton moja tu ndogo. Watu ni wengi sana kupita maelezo na kuingia kwenye panton ni kwa kutumia 'ugali'. Hali kwa kweli ni mbaya na hii ni kama mara ya tatu katika kipindi cha juma hili moja tukio la kuharibika panton kubwa linatokea. Naomba niwashirikishe kwa picha;
uploadfromtaptalk1353647955317.jpg
 
Attachments

  • uploadfromtaptalk1353648106099.jpg
    uploadfromtaptalk1353648106099.jpg
    141.8 KB · Views: 122
Ukiiona jinsi ilivyo inatisha. Kuna wakati wanajeshi wamelazimika kuingilia kati kwa kuwateremsha abiria kwa virungu ili panton iondoke. Sijui kama wahusika wanafuatilia majukumu yao vilivyo. Tukisikia vifo sitashangaa
 
Wakati wa asubuhi na jioni kunakuwa na adha kubwa, binafsi naona kuwa ubovu wa pantoni ya magogoni unasababishwa na wasimamizi wenyewe. Mv magogoni ina injini nne lakini cha kushangaza huwa zinawashwa injini mbili pekee, hili ni tatizo linalozaa usumbufu tunaopata. Nilikomaa hadi nikafika kule kwa kapteni:laser:
 
Wadau,
Nawasalimu.
Wakati navuka leo asubuhi hii nimekumbana na adha ya kivuko pale ferry Kigamboni. Kwa sasa iko panton moja tu ndogo. Watu ni wengi sana kupita maelezo na kuingia kwenye panton ni kwa kutumia 'ugali'. Hali kwa kweli ni mbaya na hii ni kama mara ya tatu katika kipindi cha juma hili moja tukio la kuharibika panton kubwa linatokea. Naomba niwashirikishe kwa picha;
View attachment 72105

hapo kwenye nyekundu sijaelewa kwamba uwe umeshiba ugali ndio uweze kuingia au?
 
Poleni sana. Hii ni hatari na aibu sana kwa nchi kubwa kama hii. Na huu uzembe wa kuzubaa kuweka mambo sawa hadi yatokee majanga, utaendelea kutugharimu.
 
Hapo ni Kigamboni, kilometa chache sana kutoka Ikulu na Wizarani.
MTIZAMO: Wahusika wamegoma kushughulikia kivuko kwa kuwa wapo bize na daraja. Mwaklyembe yupo bize na reli ya DSM (ambayo imekwishahujumiwa). Tuombe Mungu isitokee ajali.
 
Suluhisho ni daraja tu.

Hilo ni jibu rahisi kwa swali gumu. Ikiwa kama kivuko kinachobebe mamia ya watu kwa wakati mmoja kimetushinda, je hayo mabasi yatafanikiwa kubeba mamia ya watu ndani ya muda mfupi? Maamini, baada ya kukamilika kwa daraja kivuko kitatelekezwa kabisa.
 
bongo eheee bongo dalasalamu utaria ria ria ria ria weeee ndani ya daresalamu...ni wimbo profesa j
 
Wakati wa asubuhi na jioni kunakuwa na adha kubwa, binafsi naona kuwa ubovu wa pantoni ya magogoni unasababishwa na wasimamizi wenyewe. Mv magogoni ina injini nne lakini cha kushangaza huwa zinawashwa injini mbili pekee, hili ni tatizo linalozaa usumbufu tunaopata. Nilikomaa hadi nikafika kule kwa kapteni:laser:

enheee ikawaje sasa alisemaje kuhusiana na hii adha..
 
Back
Top Bottom