Hali yavurugika Lubumbashi (Congo), Watanzania wakwama!

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Kuna kundi la Watanzania waliokwama Lubumbashi, DRC baada ya waasi wa nchi hiyo kuingia mtaani.

Wanatafuta mawasiliano na ubalozi hawana wanaulizwa walienda huko kufanya nini. Baadhi ni wafanyabiashara na familia zao na wengine ni madereva na wasaidizi wao na watumishi wa kampuni za Kitanzania ambao wamejikusanya karibu na airport ya Lubumbashi kusubiri rehema za Mungu.

Naiomba serikali iwasiliane na mamlaka husika au Balozi wetu ili watanzania hawa waweze kupata hifadhi haraka. Sina pengine pa kupeleka kilio chao isipokuwa hapa JF
 
Mkuu rushanju,

Hii inatokea sasa hivi. Hali ni mbaya, mabomu yanarindima na watanzania hawajapewa mafunzo ya jinsi ya kujihami mambo yanapoenda kombo wawapo ughaibuni au kokote.

Kama kuna mtu ana mawasiliano na Waziri Membe, basi amweleze awasiliane na wahusika wawanusuru wenzetu.
 
Congo sio mahala salama hata kidogo.

Uzuri ni kwamba wa Congo hawana roho mbaya na sio watu wa kuwadhuru wageni. tatizo ni mali tu hizo nina uhakika ndio zimepotea
 
Kuna kundi la Watanzania waliokwama Lubumbashi, DRC baada ya waasi wa nchi hiyo kuingia mtaani.

Wanatafuta mawasiliano na ubalozi hawana wanaulizwa walienda huko kufanya nini. Baadhi ni wafanyabiashara na familia zao na wengine ni madereva na wasaidizi wao na watumishi wa kampuni za Kitanzania ambao wamejikusanya karibu na airport ya Lubumbashi kusubiri rehema za Mungu.

Naiomba serikali iwasiliane na mamlaka husika au Balozi wetu ili watanzania hawa waweze kupata hifadhi haraka. Sina pengine pa kupeleka kilio chao isipokuwa hapa JF

kwa taarifa yako tu, balozi zetu si za miasada sana
 
Duh, ukisikia vita inapiganwa Lubumbashi hujue DRC hakuna tena sehemu iliyo salaama.Muungu wasaidie ndugu zetu walioko huko.
 
Mkuu rushanju,

Hii inatokea sasa hivi. Hali ni mbaya, mabomu yanarindima na watanzania hawajapewa mafunzo ya jinsi ya kujihami mambo yanapoenda kombo wawapo ughaibuni au kokote.

Kama kuna mtu ana mawasiliano na Waziri Membe, basi amweleze awasiliane na wahusika wawanusuru wenzetu.

membe hana habari hiyo,yupo busy kumwinda wanasiasa na Mwandishi mwingine ambae ni adui yake amfanyizie
 
Kuna wafanyakazi wa Camel Oil, mabasi ya Taqwa wapo, Oilcom wapo, Lake Oil, GBP, wale wa mabasi ya Falcon n.k.

Majuzi inadaiwa walikamatwa Mayimayi wengi upande wa TZ, uoga wa walio huko ni kwamba waasi wanaweza kuchukulia TZ inasaidia Serikali ya Congo. Mali zao mpaka sasa zipo salama, wamefunga vituo vyote vya mafuta.
 
balozi wa tanzania congo alishaondoka toka mwaka jana pale kuna jamaa ana kaimu ............tuombe mungu tuu watoke salama........
 
Suala la msaada toka kwa serikali ilo sahau kwa sasa wako bize na maandalizi na ujio wa raisi wa China iyo Kesho.
Poleni device your own mechanism on how to save your souls.
Bwana aliyewaleta dunia hii awatangulia hakika mtakuwa salama
 
Wadau wenzangu wa Jamiiforums kama kuna mwenye uwezo wa kufanya mawasiliano na anga tajwa jamani na atowe msaada na bila shaka Ndg zetu wananusurike!
 
Magogoni wapo busy na rais wachina anayekuja kuangalia malipo ya Riz1 alivyokamatwa huko china
 
Kuna kundi la Watanzania waliokwama Lubumbashi, DRC baada ya waasi wa nchi hiyo kuingia mtaani.

Wanatafuta mawasiliano na ubalozi hawana wanaulizwa walienda huko kufanya nini. Baadhi ni wafanyabiashara na familia zao na wengine ni madereva na wasaidizi wao na watumishi wa kampuni za Kitanzania ambao wamejikusanya karibu na airport ya Lubumbashi kusubiri rehema za Mungu.

Naiomba serikali iwasiliane na mamlaka husika au Balozi wetu ili watanzania hawa waweze kupata hifadhi haraka. Sina pengine pa kupeleka kilio chao isipokuwa hapa JF

Sasa mko Watanzania wangapi?mko eneo gani? Mnapatikana kwa simu namba zipi? Maelezo uliyoyatoa hayawasaidii kufikiwa na msaada wa mtu yotote. Ni kama mtu aseme jamani niko dar es salaam manomu yanarindima tunahitaji msaada.
 
Mkuu rushanju,

Hii inatokea sasa hivi. Hali ni mbaya, mabomu yanarindima na watanzania hawajapewa mafunzo ya jinsi ya kujihami mambo yanapoenda kombo wawapo ughaibuni au kokote.

Kama kuna mtu ana mawasiliano na Waziri Membe, basi amweleze awasiliane na wahusika wawanusuru wenzetu.
Mbona wa Tz tunauzoefu wa mbagala na gongola moto.
 
Back
Top Bottom