mkadiriajimajenzi
JF-Expert Member
- Dec 31, 2015
- 549
- 608
Wafanyakazi wa Kitanzania hasa wale wa mkandarasi mkuu wa mradi huo Sumitomo Mitsui wamekua wakinyanyaswa na kudhalilishwa sana na baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo hasahasa kwa kiongozi wa ujenzi ambaye ni raia wa Kijapani anayetambulika kwa Jina la Akiharu Ishii, Huyu jamaa ni tatizo pale,mpaka sasa wafanyakazi takribani watano wameamua kusitisha mkataba wa ajira kutokana na manyanyaso yake,Anapiga ,Anatukana mbele ya hadhira,Anadai waziwazi kwamba hawezi fanywa lolote kwa sababu hela za mradi ni za msaada n.k
Mbali na kuitisha vikao vya kumuonya amekua ni mtu asiyebadilika na mwenye dharau na kejeli,Wafanyakazi wa kiTanzania walio wengi pale wanavumilia tu kwa sababu hali ya mtaani ni ngumu ila hali si shwari kwenye mioyo yao.
Kibaya zaidi kwenye huo mradi kuna raia kama 20 wa kifilipino wanaofanya kazi kama mainjinia , huyu jamaa amekua akiwapa hadhi ya juu sana hao jamaa na kukandamiza waTanzania kwa madai kwamba Mainjinia wakiTanzania hawajui lolote ni sawa na unskilled labours,yote anayoyafanya kwa waTanzania hathubutu kumfanyia mfilipino hata siku 1.Tunauomba ubalozi wa Japan na serikali yetu kwa ujumla ilione na kulifanyia kazi hili suala .huyu mtu ni kero sana