Hali ya wafanyakazi wa KiTanzania mradi wa Flyover TAZARA

mkadiriajimajenzi

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
465
500
Wafanyakazi wa Kitanzania hasa wale wa mkandarasi mkuu wa mradi huo Sumitomo Mitsui wamekua wakinyanyaswa na kudhalilishwa sana na baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo hasahasa kwa kiongozi wa ujenzi ambaye ni raia wa Kijapani anayetambulika kwa Jina la Akiharu Ishii, Huyu jamaa ni tatizo pale,mpaka sasa wafanyakazi takribani watano wameamua kusitisha mkataba wa ajira kutokana na manyanyaso yake,Anapiga ,Anatukana mbele ya hadhira,Anadai waziwazi kwamba hawezi fanywa lolote kwa sababu hela za mradi ni za msaada n.k
Mbali na kuitisha vikao vya kumuonya amekua ni mtu asiyebadilika na mwenye dharau na kejeli,Wafanyakazi wa kiTanzania walio wengi pale wanavumilia tu kwa sababu hali ya mtaani ni ngumu ila hali si shwari kwenye mioyo yao.
Kibaya zaidi kwenye huo mradi kuna raia kama 20 wa kifilipino wanaofanya kazi kama mainjinia , huyu jamaa amekua akiwapa hadhi ya juu sana hao jamaa na kukandamiza waTanzania kwa madai kwamba Mainjinia wakiTanzania hawajui lolote ni sawa na unskilled labours,yote anayoyafanya kwa waTanzania hathubutu kumfanyia mfilipino hata siku 1.Tunauomba ubalozi wa Japan na serikali yetu kwa ujumla ilione na kulifanyia kazi hili suala .huyu mtu ni kero sana
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,817
2,000
Mainginia wa kibongo = unskilled labour... Inawezekana akawa sawa tu, kila siku humu tunalalamikia elimu yetu ya kilimo cha miwa Jamaika, na maporomoko ya maji USA...
 
Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
51,265
2,000
Badala ya kuja kulalamika hapa hebu muonyeshe huyo mjapani kwa vitendo, yaani jitume, onyesha weredi hadi akuheshimu! Vinginevyo acha kazi njoo hapa kwenye baraza la gahawa utusaidie kuisoma namba!
Pumbavu
 
Abunwasi

JF-Expert Member
Jun 25, 2009
5,491
2,000
Wafanyakazi wa Kitanzania hasa wale wa mkandarasi mkuu wa mradi huo Sumitomo Mitsui wamekua wakinyanyaswa na kudhalilishwa sana na baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo hasahasa kwa kiongozi wa ujenzi ambaye ni raia wa Kijapani anayetambulika kwa Jina la Akiharu Ishii, Huyu jamaa ni tatizo pale,mpaka sasa wafanyakazi takribani watano wameamua kusitisha mkataba wa ajira kutokana na manyanyaso yake,Anapiga ,Anatukana mbele ya hadhira,Anadai waziwazi kwamba hawezi fanywa lolote kwa sababu hela za mradi ni za msaada n.k
Mbali na kuitisha vikao vya kumuonya amekua ni mtu asiyebadilika na mwenye dharau na kejeli,Wafanyakazi wa kiTanzania walio wengi pale wanavumilia tu kwa sababu hali ya mtaani ni ngumu ila hali si shwari kwenye mioyo yao.
Kibaya zaidi kwenye huo mradi kuna raia kama 20 wa kifilipino wanaofanya kazi kama mainjinia , huyu jamaa amekua akiwapa hadhi ya juu sana hao jamaa na kukandamiza waTanzania kwa madai kwamba Mainjinia wakiTanzania hawajui lolote ni sawa na unskilled labours,yote anayoyafanya kwa waTanzania hathubutu kumfanyia mfilipino hata siku 1.Tunauomba ubalozi wa Japan na serikali yetu kwa ujumla ilione na kulifanyia kazi hili suala .huyu mtu ni kero sana
Watanzania bwana!!!!!!!!!!
 
supermarket

JF-Expert Member
Sep 10, 2016
7,300
2,000
Mkuu wetu anawathamini sana mainjinia wa Tz na amewapa jukumu la kuijenga Tanzania mpya.
-Huyo mjapani hajielewi huyo anapingana na kauli ya mkuu
 
KAHUSE

Senior Member
Sep 27, 2016
199
250
Siku moja nipo kwenye foleni ndani ya daladala tukiwa tumezuiwa kupisha msafara wa Mkulu. Nikajikuta nawaangalia wafanyakazi wa kitanzania wakifanya kazi zao. Nilichokiona nilijiambia kama ndio wakandarasi wazawa basi tutasubiri sana kukabidhiwa mradi ulikamilika. Yaani wanafanya kazi kwa uvivu na kwa kutegea fulani. Hata kama mimi ningekuwa huyo Mjapani kwa hali ile ningekuwa mkali kama kweli nataka kaxlzi ya kiwango na inayokamilika kwa wakati. Tubadilikeni jamani, mengine tunayoyalalamikia humu ni kazi ya mikono yetu. Kama kuna madai ya haki yafakisheni kwa wahusika kwa itaratibu mliojiwekea!!
 
Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
11,351
2,000
Nimeg

Nimegonga like kuuuubwa, hatujitambui
 
BAFA

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
3,070
2,000
Waraab wanasema almuhtaaaj khaneeth walau kaana rijaaal (mwenye shida ni khaneeth hata kama mwanaume kamili) sasa maadamu ni msaada hatuna budi kufanywa makhaneeth
 
ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,386
2,000
Siku moja nipo kwenye foleni ndani ya daladala tukiwa tumezuiwa kupisha msafara wa Mkulu. Nikajikuta nawaangalia wafanyakazi wa kitanzania wakifanya kazi zao. Nilichokiona nilijiambia kama ndio wakandarasi wazawa basi tutasubiri sana kukabidhiwa mradi ulikamilika. Yaani wanafanya kazi kwa uvivu na kwa kutegea fulani. Hata kama mimi ningekuwa huyo Mjapani kwa hali ile ningekuwa mkali kama kweli nataka kaxlzi ya kiwango na inayokamilika kwa wakati. Tubadilikeni jamani, mengine tunayoyalalamikia humu ni kazi ya mikono yetu. Kama kuna madai ya haki yafakisheni kwa wahusika kwa itaratibu mliojiwekea!!
Shida ya hii, ni kulipwa kwa siku. Hivyo wana buy time waendelee kulipwa
 
kimkakati

Member
Oct 18, 2016
39
95
Watanzania wengi wavivu bila kujali kisomo. Ukikuta mradi wowote wa barabara wa waswahili asilimia kubwa utawakuta wamekaa wanapiga soga.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom