Hali ya usalama mpaka wa Tanzania na Malawi shakani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali ya usalama mpaka wa Tanzania na Malawi shakani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Oct 6, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  4th October 2009







  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mpaka wa Tanzania na Malawi wa Kasumulu uliopo wilayani Kyela mkoani Mbeya umezidi kuwa katika hali mbaya kiusalama kutokana na kukabiliwa na msongamano wa magari ya mizigo zaidi ya 300 ambayo yamekwama kuendelea na safari.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hatua hiyo imefuatia serikali ya Malawi kuyazuia magari ya wafanyabiashara wa Tanzania kwenye mpaka huo na hivyo kusababisha mengine kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati kukwama kupitia kuelekea Malawi na nchi nyingine. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kutokana na sakata hilo, wafanyabiashara wa mbao wa Tanzania ambao magari yao yamebeba mbao zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi bilioni nne kuzuiliwa kupita kwenye mpaka huo, wamepanga kufanya maandamano katika ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambayo wamedai imekaa kimya katika kushughulikia suala hilo. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kukwama kwa magari hayo kumeanza kuleta athari kwa wasafiri ambapo nyumba za kulala wageni zimefurika katika mpaka huo na kusababisha baadhi ya wageni kulazimika kulala nje chini ya magari yao huku wakijisaidia vichakani hali ambayo inahatarisha usalama wa maisha yao iwapo kutatokea mlipuko wa magonjwa kama vile kipindupindu. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Miongoni mwa magari ambayo yamekwama kuendelea na safari ni yale yaliyobeba mafuta ya petroli na dizeli yakitokea Tanzania kuelekea Malawi inayokabiliwa na ukosefu wa mafuta ambayo yamekwama upande wa Tanzania yakisubiri hali itengamae baada ya viongozi wa nchi hizo mbili watakapokutana na kujadiliana ili kufikia mwafaka wa tatizo lililojitokeza. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Msongamano huo wa magari ya wafanyabiashara wa nchi za Uganda,Tanzania na Kenya umetokana baada ya serikali ya Malawi kuyazuia magari zaidi ya 200 ya wafanyabiashara wa mbao wa Tanzania wapatao 150 kupita katika mpaka huo kwa madai kuwa hawajazingatia taratibu za biashara hiyo. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Magari hayo ya wafanyabiashara wa Tanzania yamezuiliwa katika mpaka huo kwa takribani miezi mitatu sasa ambapo yalikuwa yakisafirisha mbao hizo kutoka Malawi kupeleka kwenye masoko yaliyopo Dar es Salaam (Tanzania), Nairobi na Mombasa nchini Kenya. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wakizungumza na Nipashe iliyofika katika mpaka huo kujionea hali ilivyo, waliitupia lawama serikali hususani Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwamba imeshindwa kulipatia ufumbuzi tatizo hilo hali ambayo imesababisha waendelee kusota kwenye mpaka huo na hivyo maisha kuzidi kuwa magumu. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mmoja wa wafanyabiashara wa Tanzania, Zakayo Mkilamweni alisema kutokana na magari hayo kuzuiliwa hali ya maisha imezidi kuwa ngumu ambapo hakuna chakula cha kutosha kwa sababu ya msongamano mkubwa wa watu kutoka nchi mbalimbali duniani. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema mbali na tatizo hilo, wafanyabiashara wa Tanzania wameanza kuingia na hofu kukwama na biashara ya mbao kutokana na baadhi yao kukopa fedha katika benki mbalimbali za hapa nchini na kuwa na hatari ya dhamana zao walizowekeza kama vile nyumba na magari kupigwa minada endapo watashindwa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati katika taasisi za fedha walikokopa. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mkilamweni alisema wanashangaa kitendo cha serikali ya Malawi kuzuia magari ya wafanyabiashara wa Tanzania katika mpaka huo wakati walifuata taratibu zote zinazotakiwa kwa kulipa ushuru wote unaotakiwa kulingana na sheria za Malawi kwa sababu kwa zaidi ya miaka mitatu sasa wamekuwa wakiifanya biashara ya kununua mbao kutoka misitu iliyopo Malawi hivyo wana uzoefu wa namna ya kufuatilia taratibu zote zinazotakiwa katika nchi zote mbili. [/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Hatuelewi kwa nini magari yetu yamezuiliwa, kwa sababu kwanza kila mfanyabiashara amelipia Kwacha 2800 sawa na Dola 20 za Kimarekani ambazo ni kwa ajili ya leseni ya misitu pia tumelipia Dola 20 nyingine kama gharama za ukaguzi wa misitu na Dola 70 za mapato na hizi zote ni gharama zilizowekwa na serikali ya Malawi na ambazo tumekuwa tukitoa kila mwaka na tumezilipa zote,”alisema Mkilamweni. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mfanyabiashara mwingine Julius Minja, alisema magari yao yalipoanza kuzuiliwa na Mamlaka ya Mapato ya Malawi licha ya kwamba walikuwa wamefuata taratibu zote zinazotakiwa walikubali kutoa faini ya dola za Kimarekani 200 kwa maana ya kila gari dola 100 na kila kichwa dola 100 na ndipo yaliruhusiwa kuanza safari kuja mpakani Kasumulu. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Minja alisema katika hali ya kushangaza magari yaliyosheheni mbao yalipofika katika mpaka huo wa Kasumulu Maafisa wa Mamlaka ya Mapato ya Malawi waliyazuia yasivuke ambapo walitangazIwa utaratibu mpya wa kwamba mfanyabiashara anayetaka kufanya biashara ya kusafirisha mbao kutoka Malawi lazima awe na fomu ya CD One. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema wafanyabiashara wa mbao wa Tanzania wamekwama katika hilo kwasababu utaratibu wa kupata fomu hiyo ni kwamba lazima uwe raia wa Malawi ambaye umewekeza fedha katika benki za nchi hiyo zisizozidi Dola za Kimarekani 1,200 na ndipo utaruhusiwa kufanya biashara hiyo kwa uhuru bila kusumbuliwa utaratibu ambao haukuwepo tangu awali. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Utaratibu mwingine uliotangazwa na serikali ya Malawi ni kwamba kila mfanyabiashara ambaye siyo raia wa nchi hiyo lazima aonyeshe ‘invoice’ inayoonyesha kuwa alibadilisha fedha za nchi aliyotoka kuwa fedha za Malawi katika benki zilizopo Malawi utaratibu ambao umekuwa mgumu kwa wageni wasio raia wa Malawi kwani maduka ya kubadilishia fedha yaliyokuwepo mpaka wa Kasumulu yalishafungwa hivyo kila mgeni anayekwenda Malawi anakuwa amezibadilisha fedha zake. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Naye mfanyabiashara mwingine Kadari A.Kadari alisema matatizo yote hayo yamejitokeza kutokana na chuki waliyojenga wafanyabiashara wa Malawi ambao wanaona biashara ya mbao wanayoifanya wafanyabiashara wa Tanzania inawanufaisha sana hivyo katika kuwakomoa wakashinikiza kuwekwe utaratibu mgumu utakao washinda na hivyo kuchukua hatua ya kuachana na biashara hiyo. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kadari alisema kilichowasukuma wafanyabiashara wa Tanzania kwenda kununua mbao Malawi ni kwasababu mbao nchini Malawi zinauzwa bei rahisi ya Sh.100,000 kwa mita moja ya ujazo wa mbao wakati kwa upande wa Tanzania mbao kama hiyo inauzwa Sh.180,000 hadi Sh.200,000 hivyo wanashindwa kupata faida wananunua Tanzania na kwenda kuuza katika masoko yaliyopo Nairobi,Mombasa na Dar es Salaam. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Maafisa wa Mamlaka ya Mapato ya Malawi waliohojiwa na Nipashe iliyotaka kujua kiini cha tatizo hilo kwa sharti la kutotaja majina yao, walisema kimsingi wao hawawezi kutoa maelezo yeyote kuhusiana na suala hilo kwa madai wanasubiri maamuzi yatakayotolewa na viongozi wa juu wa serikali ya Malawi ambao walidai wanaendelea kulijadili. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Abdallah Kihato alipoulizwa na Nipashe alisema uongozi wa serikali ya mkoa umewasiliana na viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambao wanaendelea kulishughulikia tatizo hilo. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hivi karibuni kulitokea vurugu kubwa katika mpaka wa Kasumulu ambapo vijana wa Tanzania walichukua hatua ya kuufunga mpaka huo kwa zaidi ya masaa kumi kwa kuweka magogo na mawe kuzuia magari na na wananchi wa Malawi wasivuke kuja Tanzania. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hatua hiyo ilichukuliwa na vijana wa Tanzania kufuatia ya magari ya mizigo (maroli) yapatayo ya wafanyabiashara wa Tanzania yaliyosheheni mbao kuzuiliwa nchini Malawi na vijana wa nchi hiyo kwa madai hayalipi ushuru yanapoingia Malawi. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Tukio hilo lilitokea Septemba 29 majira ya saa moja asubuhi katika mpaka huo hali iliyoilazimu Kamati ya Ulinzia na Usalama ya Wilaya ya Kyela chini ya Mwenyekiti wake Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Abdallah Kihato kufika katika mpaka huo kwa ajili ya kuwatuliza vijana hao waliokuwa wamepandwa na jazba wasiweze kufanya maasi. [/FONT]



  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

  http://www.ippmedia.com/
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  nafikiri malawi tunaweza kuwadhibiti wakileta choko choko
   
Loading...