Hali ya usalama kwa wanafunzi/ Watanzania waishio Wuhan nchini Uchina ipo matatani, waiomba Serikali iwarudishe nchini

Hapana aisee Hicho Kirusi kikiingia Tanzania Tutapukutika tuishe Wao Wavumilie

Nao watuonee huruma kama sisi tunavyowaonea huruma
Humu tutarumbana tu ila mwisho serikali ndo muamuzi wa mwisho, tusubiri tuone itafanya nini
 
KENZY,
Mkuu umenena vizuri kabisa , niko beijing na its locked down kila mahali , na si beijing tu ni sehemu nyingi za china , tatizo watu wanasambaza maneno mengi paka inaleta panic.
 
Hakuna anaetaka wengine wage
Ila kufanya maamuzi ya kijinga linaweza wafanya wote wage
Maamuzi ya kijinga yashafanya Sana. Ata mv Bukoba baadhi ya watu hawakuokolewa kutokana na maamuzi ya kijinga ya kutoboa meli
Watu mna roho mbaya sana na unafiki wa kiwango cha hali juu. Halafu mnajidai watz tuna upendo. Upendo gani huo wa kutaka mwenzako afe. Wivu na roho mbaya ndio zinawasumbua. Yaani unaandika kabisa wanajisikia sababu wameenda China, seriously?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanafunzi wakitanzania walio Wuhan (China) walilia kurudi nyumbani Tanzania.

Hiizo picha ni za kweli ni za Watanzania wenzetu waishio china,hawa wengi ni wanafunzi wa vyuo mbalimbali mji wa Wuhan ambao ni mji mkuu wa Hubei ,hii ndio sehemu ambayo masmbukizi yalianza hivyo yanaendelea kuzidi kila siku .

Taarifa za Leo tar 11/02/2020 (Last update) • Death toll: vifo sasa ni 1017, Recovered: waliopona ni 4014, Confirmed cases, Waliothibitishwa kuambukizwa ni 42714, Suspected cases: (wanaodhaniwa kuambukizwa ni 21675.

Hao waliopo hapo ni Watanzania wengi wakiwa Wuhan kwani, kwani wamewekwa ndani tu ,vyuo vimefungwa, hawatoki nje. Ukweli kisaikolojia lazima wateseke sana sababu ugonjwa unazidi kusambaa, hawatoki nje, hawajui lini vyuo vitafunguliwa, wanateseka wakijiuliza hivi hawana umuhimu kwa Taifa lao, hivi wao sio Watanzania?

Nimeongea pia na rafiki zangu ambao wapo Zhejiang na Gwangju wamethibitisha namna ambavyo wao binafsi na Watanzania wa Wuhan walivyo na wasiwasi sababu Wuhan ndio epicenter ya ugonjwa huo.

Nchi nyingi sasa tayari zimechukua (Evacuate/airlift out) Raia wao US, Ukraine,Spain, France nk Afrika ni Morroco, Algeria,Tunisia, Libya na juzi hapa Rais Uhuru Kenyatta ametangaza mpango wa kwenda kuchukua Raia wake.

Raia wanaomba Serikali ikawachukue hata kama sio wote ila wale wa Wuhan waondolewe sababu hofu ni kubwa ya maambukizi na hawaijui hatma yao na ugonjwa unazidi kuenea.

Mwanzo nilikuwa nina kisirani kwanini serikali yetu imetelekeza Raia wake huko China hasa wale wa Wuhan, ila hii asubuhi nimemsikiliza Balozi wa Tanzania huko China, ameongea kama dakika 10, ameongea vizuri sana kwamba sasa hivi ni kama week Wuhan hakuna ndege inaruhusiwa wala magari watu wote wapo ndani, Japan waliondoa watu wao bahati mbaya watu watano wakaambukizwa kati wakarudi kwao Japan na huo ugonjwa wengine wakaambukizwa Airport walipofika huko Japan, ameongea vizuri sana.

Tunawaomba ndugu zetu Watanzania huko Wuhan wawe na matumaini, amani na wasiwe na mawazo kwani Watanzania tunawaombea dua yote haya yataisha, na tunaiomba serikali yetu hali ikitulia na uangalizi wa kuwasafirisha ukiwa mzuri zaidi basi wawa evacuate .Mungu yupo nanyi.

Abdul Nondo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa wakirudi Tanzania itakuwaje? Kuna manadalizi yeyote kwa watu wanaorudi toka china?
 
Hawa wanafunzi ilitakiwa yale maeneo ya ubarozi huko huko china kwa muda wangejengewa holi kubwa kama ukumbi iwe kambi yao ya muda. Lakini kuja huku hao,ikitokea mmojawapo amekuja na huo ugonjwa ninavyojua kama china wenyewe wanahaha mpaka sasa hivi wanapukutika,sisi ndio tutafukiwa wote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom