Hali ya usalama kwa wanafunzi/ Watanzania waishio Wuhan nchini Uchina ipo matatani, waiomba Serikali iwarudishe nchini

mazojms

JF-Expert Member
Sep 22, 2017
1,607
2,481
Nafikiri ni muda sasa Serikali iwafikirie vijana wetu Watanzania walioko nchini China (hasa walio kwenye maeneo yalioathirika zaidi na Corona virus).

Hofu inazidi kutanda si kwa vijana hao pekee bali hata kwa ndugu zao tulio Tanzania.

Nimehuzunishwa sana na ujumbe wa video ikiwaonyesha vijana wakiitaka na kuiomba serikali iwarudishe nyumbani Tanzania.

I believe serikali yetu inapenda raia wake, na hawa vijana wapo kwenye wakati ambao wana uhitaji huo upendo more than anything.

Screenshot_2020-02-10-22-55-22-1.jpeg
Screenshot_2020-02-10-22-55-32-1.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa unaosababishwa na 'corona virus' huko wihan nchini china ambao umeripotiwa kusababisha vifo vya mamia ya watu nchi nyingi zimeonekana kuchukua hatua za haraka kuhakikisha usalama wa raia wao waishio maeneo yenye mlipuko wa ugonjwa huo.

Licha ya juhudi zinazofanywa na wazazi wa wanafunzi Watanzania walioko maeneo ya Wuhan ambako ndiko chimbiko la mlipuko huo kuwarejesha nyumbani, Serikali ya Tanzania imeonekana kuchukua hatua kwa speed ya kinyonga hali inayozua sintofahamu miongoni mwa wanafunzi Watanzania walioko Wuhan.

Kwa maelezo ya mwanafunzi mmoja aliyeko Jianghan University hapo Wuhan amesema kuwa wazazi wao wameandika barua mara kadhaa kwa serikali na pia wao wameshafanya kikao na balozi lakini bado serikali haijatoa tamko lolote kuhusiana na kurejeshwa kwao.

Mwanafunzi huyo pia alisema kutokana na hali kuwa mbaya zaidi hosptali zimefurika wagonjwa mpaka kufikia hatua ya kulaza wagonjwa chuoni hapo.

Nichukue fursa hii kuitaka serikali uchukue hatua za haraka ili kuhakikisha usalama wa Watanzania walioko Wuhan.

Screenshot_20200211-073133.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini sisi tunapowazuia hawa je serikali imezuia safari za ndege kutoka China kuja hapa?
Unajua kiongozi kuwarudisha hawa watu sio tatizo, Tatizo ni kwamba tunavipimo vyenye weledi wa kugundua hakunaaliyeambukizwa?!?!, Serikali iko makini sana juu ya suala hili. Si unaona China yenyewe (kwa maana ya Taifa kubwa) limewazuia watu kwenye meri ili wajiridhishe kuwa hakuna mwenye maambukizi atakayeingia kitaa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanafunzi wa Kitanzania anayesoma Urusi lakini kwa sasa yupo China kufanya Field kwa kipindi cha miaka miwili (Jina tunalihifadhi), amekubali kuelezea taarifa kuhusiana na video inayosambaa katika mitandao ya kijamii ambao inaonesha watanzania wanaomba kurudi nyumbani

Amesema tatizo sio kukosa nauli lakini Airport na njia nyingine za usafiri katika miji waliopo wamezuiwa kutoka kwa hofu ya kuepuka kusambaa zaidi kwa virusi vya Corona.

Hizi video zinazoendelea kusambaa sio kwamba wananchi wa tanzania ni wa kwanza kuomba msaada, kuna baadhi ya raia waliopo wuhan waliomba masaada kwa serikali zao na wakafuatwa na serikali

Sijui utaratibu gani, lakini najua kuna utaratibu ambao unafutwa kuwaondoa wananchi wake katika mji huu.

Sio kwamba wanafunzi nchini huo hawana nauli ya kurudi ila kwa sheria ya sasa hawaruhusiwi kutoka kwa ugonjwa huo, hivyo wanaomba serikali iwarudishe kwa kufuata utaratibu kwa kuwa wao wenyewe hawezi kurudi kutokana na tishio la ugonjwa.

Watanzania hao wameshika mabango kuwa hawajaambukizwa ugonjwa huo na wanahitaji kurudi nyumbani kwa kuwa mji wa Wuhan umekuwa mgumu kwa sheria za kutotoka wala kusafiri ili kuuia kusambaa zaidi kwa ugonjwa huo.
 
Unajua kiongozi kuwarudisha hawa watu sio tatizo, Tatizo ni kwamba tunavipimo vyenye weledi wa kugundua hakunaaliyeambukizwa?!?!, Serikali iko makini sana juu ya suala hili. Si unaona China yenyewe (kwa maana ya Taifa kubwa) limewazuia watu kwenye meri ili wajiridhishe kuwa hakuna mwenye maambukizi atakayeingia kitaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hatuna wataalam na vipimo vya kueleweka mpaka sasa? Basi hii seeikali itakuwa ni useless kabisa.
 
Back
Top Bottom