Hali ya Usafiri Kimara na Mbezi baada ya kufutwa kwa daladala za kwaiida

kuch-kuch

Member
Jan 14, 2014
40
17
Habari wanajukwaa.
Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko ya usafiri kwa wakazi wa Kimara na Mbezi hasa kutokea katikati ya mji kama Kariakoo na Kivukoni. Watu wengi wamekuwa wakichangia aidha kwa kutojua hali halisi ama kwa mitazamo ya kisiasa. Hakika kama mdau wa usafiri kwa maeneo hayo kwa siku za karibuni hali imekuwa mbaya juu ya upatikanaji wa magari yanayotosheleza mahitaji. Kiufupi kwa muda huo nimeshuhudia haya yafuatayo:
Mosi, Mabasi ya mwendokasi kuzidiwa na kushindwa kutoa huduma sitahili kwa wananchi wanaotumia huduma hiyo. Mfano, leo asubuhi nikiwa kituo cha Kimara tumejikuta tukiwa stranded kwa zaidi ya dakika 40 bila gari kufika. Kwa muda huo tu nilishuhudia kituo kujaa mpaka kufikia zaidi ya watu 400. Mara baada ya basi kufika ilikuwa mwenye nguvu ndiye aliweza kuingia.
Pili, Kwa wakazi wa Mbezi hali imekuwa mbaya zaidi kwani nauli nayo imeongezeka kufikia shs 1050 kwa safari moja badala ya 500 au 600 waliyokuwa wanalipa kwenye daladala za kawaida.
Tatu, hali hii imesababisha hali ya usafiri katika maeneo mengine kuwa ngumu na wananchi kulanguliwa na waendesha bajaji na Noah. Mfano, sasa hivi pale Ubungo stendi ya daladala nauli ya kwenda Manzese au Magomeni ni shs 1000. Hii hufanyika bila woga wala kificho. Kumbuka ili upande mwendokasi ni lazima upande daraja refu kutokana na sababu kuwa abiria watokeao stendi kuu kuwa na mizigo mingi au wagonjwa imekuwa vigumu kuweza kupanda.
OMBI
Sisi wakazi wa Kimara na Mbezi tunaomba serikali iendelee kuziruhusu daladala kama zamani au iimarishe huu usafiri wa mabasi ya mwendokasi ambao unaonekana kusuwasuwa.
 
Mimi niliona mbali tokea mwanzo nikawambia nchi hii sasa inarudishwa katika mfumo wa ujamaa. Ujamaa ni mfumo wa hovyo sana ila kwa kuwa ulipambwa kwa jina la kitapeli "ujamaa", watu wengi wameshindwa kugundua uhovyo wa mfumo huu na kasumba zake(legacy). Kilichofanyika hapo ni kasumba ya ujamaa ambayo inachukia ushindani wa soko huria. Haioni faida ya ushindani. Poleni sana wana Dar es salaam.
Habanajukwaa.
iri kwa maeneo hayo kwa siku za karibuni hali imekuwa mbaya juu ya upatikanaji wa magari yanayotosheleza mahitaji. Kiufupi kwa muda huo nimeshuhudia haya yafuatayo:
Mosi, Mabasi ya mwendokasi kuzidiwa na kushindwa kutoa huduma sitahili kwa wananchi wanaotumia huduma hiyo. Mfano, leo asubuhi nikiwa kituo cha Kimara tumejikuta tukiwa stranded kwa zaidi ya dakika 40 bila ga
 
Badala ya kutatua tatizo wao wamelikuza na wanazidi kukuza tatizo, hii ni hatari....hizi transition ni hatari kwa viumbe wa hali ya chini
 
Mm mpaka leo natamani Mtu anieleweshe Logic kamili ya zile Ngazi pale Kimara na Moroco .
Nimekaa nikatafakari walikua wanakwepa nini Kwakweli sijaona.
 
Back
Top Bottom