Hali ya Uongozi na Changamoto za Tanzania: Je, Viongozi Wetu Wanatimiza Wajibu Wao?

Upekuzi101

Senior Member
Aug 28, 2020
134
348
Habari Jf.
Hivi Tangu Tanzania ipate Uhuru Kuna viongozi wangapi wamejiuzulu nafasi zao pale wanaposhindwa kukidhi mahitaji?

Imekuwa kawaida sana kwa viongozi wengi katika nchi ya Tanzania kutokuwa na sense ya responsibility pale wanaposhindwa kutekeleza majukumu yao.

Waziri kama Mwigulu na Ashatu Kijaji bila aibu bado wapo ofisini na mamlaka za uteuzi hasa Rais naye anaonekana kuwa kimya na kuendelea kuwakumbatia hawa wadhaifu.

Kama Waziri wa biashara na cabinet yake yote wanashindwa kusimamia kero ndogo ndogo kama hizi Rais Samia anategemea zuri lipi au jema lipi kutoka wizara hii hasa ikiongozwa na hawa viumbe?

Kama kero ya kariakoo iliyopo karibu na ofisini zote za Serikali hapo Dar es salaam imegharamu waziri mkuu Kuja je tatizo kama Hilo ni kubwa kiasi gani kwa maeneo mengine ya nchi? Na nani anategemewa kutatua hizo changamoto?

Kama viongozi wanasubiri migomo ndo watatue kero, itakuwaje kama Mwanza, Arusha Mbeya, Lindi, Mtwara na Tanzania nzima wakigoma kwa wakati mmoja?

Maoni yangu ni kuwa viongozi wengi wa Tanzania hawana connection halisi na maisha ya kawaida ya watu wa chini kwaiyo hawajui kinachoendelea kwaiyo siku moja utashangaa nchi nzima kada karibu zote zimegoma ndo mwanzo wa Tanzania kupoteza amani. Kwaiyo ni vema hata kama hampendi mjenge hata mazoea ya kila wizara kuwa na siku moja at least kila mwezi kutatua, kujadili na kupokea maoni katika kuboresha huduma.

Tatizo la Tanzania ni uongozi na viongozi wenyewe. Jamani viongozi nyinyi siyo miungu, wala malaika, acheni kusinzia ofisini shida na matatizo ya Tanzania ni nyinyi tu.
 
Back
Top Bottom