Hali ya uchumi yazidi kuwa tete hotel za kitalii za Mount Meru na SnowCrest za Arusha zapigwa mnada

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,647
9,574
Arusha. Hoteli mbili za kitalii za Mount Meru na Snow Crest za mkoani hapa zimetangazwa kuuzwa kutokana na kuongezeka gharama za uendeshaji huku moja ikielezwa kushindwa kulipa stahili za wafanyakazi.
Pia, kuuzwa kwa hoteli hizo kunaelezwa kuchangiwa na kudorora kwa uchumi na kukosa wateja huku nyingine kadhaa mkoani hapa zikipunguza wafanyakazi.
Awali Mount Meru ilikuwa ikimilikiwa na Serikali kabla ya kubinafsishwa na kufanyiwa ukarabati mkubwa. Hoteli hiyo na Snow Crest, zilizinduliwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete.
Mount Meru imetangazwa kuuzwa na Dalali wa Kimataifa Mark Danford, ambaye anaishi nchini Marekani kwenye mitandao mbalimbali.
Msemaji wa Mount Meru, Queen Joseph aliliambia gazeti hili kwamba hoteli hiyo inauzwa kwa taratibu za kawaida huku akiwataka watumishi na wananchi kutokuwa na hofu.
“Ni kweli hoteli hii inauzwa na tayari imetangazwa, lakini hatua hii haitokani na kukosa wageni,” alisema Queen.
Queen alisema historia ya hoteli hiyo ni ndefu na fedha za kuifufua baada ya kubinafsishwa zilitolewa na mifuko ya wafadhili mbalimbali, hivyo inatakiwa kuuzwa ili kuzirejesha.
Hoteli ya Snow Crest iliyopo eneo la Ngulelo nayo ipo kwenye mchakato wa kupigwa mnada kutokana na deni la zaidi ya Sh400 milioni, inazodaiwa na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Tangazo la kuuzwa kwake linasema kwamba asilimia 25 italipwa baada ya mnada na asilimia 75, ndani ya siku 14 za kazi baada ya mnada huo.
Kufuatia hali hiyo, gazeti hili lilifika hotelini hapo na kukutana na walinzi, ambao walikataa kuzungumza chochote kwa madai kuwa siyo wasemaji.
Meneja wa NSSF mkoani Arusha, Dk Frank Maduga alithibitisha shirika lake kuidai hoteli hiyo malimbikizo ya mafao ya waliokuwa wafanyakazi wake.
Dk Maduga amesema Bodi ya Wadhamini ya NSSF kwa niaba ya wateja wao (wafanyakazi) ilifungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Arusha mwaka 2016 kudai fedha hizo na kushinda, hivyo kinachofanyika ni utekelezaji wa hukumu hiyo.
“Tulifungua kesi mahakamani ambako tulishinda na ikaamriwa mali na jengo viuzwe kufidia fedha hizo, sasa tunatekeleza hukumu ya Mahakama,” alisema Dk Maduga.

Source:Mwananchi.
 
JF ni zaidi ya magazeti yote, habari ilishaletwa humu zaidi ya wiki 2 zilizopita. Habari hii bora mods waiondoe tu.
 
JF ni zaidi ya magazeti yote, habari ilishaletwa humu zaidi ya wiki 2 zilizopita. Habari hii bora mods waiondoe tu.
Hapana, habari hii ifanywe "sticky" ili iendelee kuwakumbusha waajiri wanaokataa kupeleka makato ya wafanyakazi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwamba siku zao zinahesabiwa!
 
Hapana, habari hii ifanywe "sticky" ili iendelee kuwakumbusha waajiri wanaokataa kupeleka makato ya wafanyakazi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwamba siku zao zinahesabiwa!

Habari iendelee ili iwakumbushe wamiliki wa mahoteli na wafanya biashara wengine umuhimu wa kulipq kodi stahili. Huwezi kuwa tajiri kwenye nchi maskini kama hujaibia serikali.
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Back
Top Bottom