HALI YA UCHUMI: Tuwashauri serikali hapa nini kifanyike

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,588
11,668
Lugha rahisi Uchumi ni hali ya ustawi wa jamii au eneo husika. Kwahiyo nitazungumzia hali ya uchumi hata mimi sio mchumi.

Uchumi mara nyingi hutazamwa kwenye ngazi za kijiji , eneo , taifa au dunia.

Sayansi ya Uchumi (kwa Kiingereza
economics ) ni tawi la elimu inayochunguza masharti ya uchumi kufaulu au kushindwa.

Katika uchumi wa kisasa mara nyingi sekta tatu hutofautishwa lakini wataalamu wengine hutaja sekta ya nne.

Kuelekea uchumi wa viwanda ni muhimu serikali ikaanza na Agro based industries ili kuongeza market ya mazao ya kilimo.

Pia serikali isaidie kurudisha uwezo wa CB kuendelea kukopesha kwani sekta binafsi imedorora baada ya serikali kupunguza matumizi.

Sekta binafsi ndio mwajiri mkubwa kuliko serikali hivyo ni muhimu kutengeneza mazingira bora ya sekta hii kukua.

Kuna kiwango cha ukomo wa bajeti ya mwaka 2017/2018

IMG_20170330_114056.jpg

Ni muhimu kwa serikali kuweka mazingira ya vijana kujiajiri kuwa mazuri, kwani kwasasa mazingira ni magumu kila kukicha,ajira nazo ni changamoto kubwa.Vijana wamekata tamaa.

Uchumi ni sayansi unaendeshwa kwa kufuata "scientific principles" ambazo huwezi kuzipindisha ukabaki SALAMA.

Serikali hatuwezi kukua kichumi kama tu bajeti ya 2016/17 wizara ya kilimo mifugo na uvuvi waliomba karibu ya billion 101.5 lakini mkawapa billion 2 tu.

IMG_20170330_002352.jpg

Kwa hali hii huwezi kushangaa kwa inflation ya chakula kuwa kubwa zaidi.

IMG_20170330_081505.jpg

Taifa lenye viongozi makini na lenye sera nzuri kiuchumi hutumia sekta moja ya uchumi kukuza sekta zingine.

Utalii=Viwanda.

Kama wazee wetu wanazungumz hali ya uchumi kwa sasa kwanini tuache.
IMG_20170330_103925.jpg

Tunafahamu dhamira njema ya serikali yetu lakini tujikite katika vipaumbele vichache vinavyotekelezeka,tutafanya tathimini 2020.

Karibuni kwa maoni.

mr mkiki.
Dar es salam.
 
Kasema yeye Ni Rais ambaye Anajiamini, Hua hapangiwi na mtu na wala haonyeshwi njia.

Mbona humuelewi Mkuu? Unataka akutukane hadharani ndio ujue kua hapendi? Acheni kumkera bwana aaaahhh.
 
asante mkuu.
Tutafute expert opinions kama Tanzania ya Kilimo na Tanzania Ya Viwanda ipi Ni faster train ya kutufikisha tuendako.
Niwakati wa kuangalia kwa jicho la kijani kibichi Maziwa,mito,mabonde,mabwawa yaliyotapakaa nchi nzima.

Ila naona watu tumeanza kwenye kujadili watu badala ya ideas
 
We unatafuta matatizo na mkubwa, kashakwambia yeye hashauriwi, haoneshwi, hatetereki anajiamini sasa unamshauri nn wakati kashakwambia hataki ushauri
 
Mkuu we unamjua vizuri rais wetu?
Yeye ndio anataka atushauri sisi sio sisi tutoe ushauri kwake
wewe shauri unaweka record ambazo kama zikipuuzwa leo zitakuwa na maana 2020 au 2025+
usijikatishe tamaa..., wenda mawazo yako yakachukuliwa hata Kenya,Uganda au popote duniani au kwa taasisi flani au mtu mmoja yakamkomboa bado utakuwa na mchango kwa dunia mkuu.
 
Sijui kama atachukua ushauri wako au ndio atasema udaku wa mitandaoni
 
Tukubaliane kama nchi kuwa tunajenga formal economy au informal economy.
Kama ni formal basi tufanye outsourcing ya Human Resource watusaidie kuhakiki upya vyeti vya kuanzia viongozi wa juu, maCEO, mameneja hadi makarani ili viwe ni halisi na wewe sehemu walipo kwa uwezo wao.
Mbali na hapo tukubaliane tu kuwa tunajenge informal economy na qualifications za wasimamizi iwe ni nani anamjua nani au nani kaota nini usiku. Na hapo haitategemea mwenye cheti bandia au halisi mradi tu kujua kushout.
 
Formal economy
 
Formal economy
Utaleta matatizo, hapa tunaoa waigizaji wanaojenga 'formal economy' lakini kiuhalisia walitakiwa wawe upande mwingine.
Sasa ukisema kuwapiga chingi ili waje wajuzi wa uchumi na wenye vyeti halisi itakuwa tabu, labda!
 
Nakubaliana wew lakini kuna kitu hapa nina nipa shida

GDP Asilimia 7 ni wastani mzuri lakni kwanin haiendani na hali halisi
IMG_20170330_143845.jpg
 
Back
Top Bottom