Hali ya uchafu Kijitonyama yawa kero kwa wananchi. Waitaka Serikali kuwajibika

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,677
2,000
WANANCHI wa kata ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam, wameitaka serikali kuchukua hatua za kukarabati baadhi ya barabara za Kata hiyo kutokana na chemba zinazotiririsha maji machafu katika barabara ya Kajenge kwa muda mrefu bila kukarabatiwa FikraPevu imebaini.


Wakazi hao wameiambia FikraPevu kuwa licha ya tatizo hilo wanaiomba Serikali kuchukuaa hatua ya kukarabati barabara zinazopita katika Kata hiyo kwani zimemeguka katika sehemu za pembezoni kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni katika jijini Dar es Salaam.


Chemba inayolalamikiwa Kijitonyama

Eneo lenye chemba ambayo inalalamikiwa na wakazi wa Kijitonyama kwa kutiririsha maji machafu katika eneo la Kajenge kwa muda mrefu bila kudhibitiwa


Aidha, wamesema kutokana na uwepo wa chemba zinazotiririsha maji machafu katika eneo hilo, pia barabara hizo kwa muda mrefu zimetelekezwa na serikali kwani hazi karabatiwi na kuwatia hofu wakazi hao kuwa na hofu ya kupata magonjwa ya milipuko yanayotokana na uchafu huo.


Mmoja wa wananchi hao, Amiri Yusuphu (54), amesema licha ya kero hizo kuripotiwa katika ngazi za Vijiji, Kata na Wilaya bado tatizo hilo limepuuzwa na wawakilishi wa wananchi, huku baadhi ya viongozi wa Serikali wakipita katika eneo hilo kila kuona umuhimu wa kufanya mabadiliko ya kusimamia utatuzi wa kero hiyo.


“Viongozi wa Serikali akiwemo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, wanapita hapa lakini wanashindwa kututatulia matatizo yetu na hii sio lazima tuwaambie wanatakiwa kuwa wazalendo na sio kutusubiri sisi kuwatafuta mara kwa mara” Yusuphu.


Kuhusu suala la barabara kuharibika katika Kata hiyo, wamesema mvua zilizonyesha zimesababisha barabara zilizo nyingi katika eneo hilo kuharibika kutokana na kujengwa chini ya kiwango, na hivyo zisipokarabatiwa zinaweza kusababisha ajali za mara kwa mara hususani nyakati za usiku kutokana na kumeguka sehemu za pembezoni na kuzifanya kuwa nyembamba.


Wakazi hao akiwemo, Salum Mponda, ambaye pia ni mkazi wa Kijitonyama amesema ujenzi wa barabara usiozingatia viwango, ndio sababu kubwa ya barabara nyingi kuharibika hasa nyakati za mvua na kuitaka serikali kubadilisha utaratibu wa kutoa tenda kwa Wakandarasi wa kufanya kazi na watu ambao ni waadilifu.


Jiji la Dar es Salaam ni moja kati ya miji nchini yenye mipango na kampeni za kufanya ukarabati wa kuboresha usafi katika maeneo hayo, licha ya miji hiyo kutajwa kuongoza kwa uchafu uliokithiri katika maeneo hayo.


Chanzo:Hali ya uchafu Kijitonyama yawa kero kwa wananchi. Waitaka Serikali kuwajibika
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
49,914
2,000
viongozi wenyewe they dont give a f..... khsu kuboresha makazi na sisi wananchi pia ni wachafuuuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom