Hali ya siasa za Tanzania kwa sasa inahitaji dirisha dogo la usajili

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,377
1,952
Ni mwanzo wa mwaka 2012,
Binafsi sina elimu yoyote ya unajimu,lau ningeweza kutoa tathmini ya mwaka ambao tarakimu zake(namba)zinaanzia na kuishia na namba hiyohiyo yaani 2(mbili).

Lakini kuna jambo moja ambalo nimeweza kuliona na kulitafakari bila majibu kamili,juu ya hali halisi ya kisiasa nchini hususan ndani ya vyama vyetu vya siasa nchini.

Kwa ujumla kuna walakini katika hali halisi ya maelewano ndani ya vilivo vingi kiutawala
Na ki-sera.
Habari kuu zilizotawala kuhusu siasa za ndani zinahusu migogoro ya ndani ya vyama na kwa uchache kama ifuatavyo.
*CCM wana mvutano mkubwa uliotokana na sera za kuvuana magamba,ikiwa pamoja na mbio za kuusaka urais 2015.
*NCCR wana mvutano unaomtaka mwenyekiti wao kun'atuka na kundi lingine likipinga na imepelekea kuvuana uanachama kwa baadhi yao hivi karibuni.
*CHADEMA bado hali si shwari kutokana na kesi iliyoko mahakamani kule mkoani Arusha ikiwahusisha madiwani wanaopinga kuenguliwa kwao toka ndani ya chama na hivyo kupelekea wao kupoteza u-diwani.
*CUF ndio kama tulivyoona na kusikia hapo jana,kwani bado mgogoro ndio umeanza pamba moto na wameendeleza utamaduni wao wa kuvuana uanachama.
Orodha hii ni kwa uchache tu, lakini yumkini hali si shwari katika vyama karibu vyote vya sias nchini.Kimsingi huu si wakati muafaka kuwa na migogoro ndani ya vyama vyetu vya siasa wakati taifa likikabiliana na changamoto kuelekea uundaji wa KATIBA mpya.
Suala ambalo linahitaji umakini,na utulivu wa kisiasa kwa ujumla wake

Ni kutokana na hali hiyo,ndio nimejikuta nikiwa na pendekezo la wazo mbadala,ya kwamba tuwe na Dirisha dogo la usajili kama wafanyavyo kwenye ligi ya mpira wa miguu.
Hii itatowa fursa kwa kila mwanasiasa kujipima na kujielewa kama pale alipo ni sahihi kwake au aondoke na kujipanga kwingineko kabla ya kuanza ngwe hii ya pili ya uundaji wa katiba mpya kuelekea uchaguzi wa 2015?
NAOMBA KUWAKILISHA
 
Back
Top Bottom