Hali ya sarafu yetu yazidi kuimarika, pongezi kwa serikali ya Magufuli

ELI-91

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
3,583
9,666
Pongezi kwako JPM na waliokupa taarifa na ushauri juu ya hatua za kuchukua. Sarafu yetu inapopoteza thamani ni mzigo kwetu sote. Mwanzoni mwa mwezi wa tatu hali ilikua mbaya sana na shilingi haikua 'stable' kabisa, ilikua kila siku mpya inazidi kuporomoka. Lakini kwa sasa hali imetengamaa, japo bado dola moja inauzwa karibu na 2360 lakini bei haipandi hovyohovyo kama mwanzoni mwa mwezi huu.
20190330_140853.png

penye kukosoa tutakosoa na penye kusifu tutasifu.
 
Hivi hapo kati kati ilifikia ngapi Mkuu?

maana Juzi nmesema zile kelele zimeisha nikajua imerudi kwenye 2200
iliuzwa hadi 2400 na zaidi, lakini baada ya zile hatua imeanza kuimarika taratibu, na kitu cha muhimu sana sio shilingi kupanda thamani bali ni stability, thamani isiporomoke au kupanda hovyo.
 
iliuzwa hadi 2400 na zaidi, lakini baada ya zile hatua imeanza kuimarika taratibu, na kitu cha muhimu sana sio shilingi kupanda thamani bali ni stability, thamani isiporomoke au kupanda hovyo.
Sawa Mkuu basi hongera zimwendee jiwe
 
Na mshukuru jpm kwa mvua ya jana uck ,cfa zngne nazishangaa saana,
hapo kwenye mvua sidhani kama JPM alifanya juhudi zozote :p
ila kwenye thamani ya shilingi sote tumeona alichokifanya
 
Ni kweli ila hebu aache uwanja sawa wa kufanya siasa bhana!
Binge live amezima ila yeye kila uchwao ata km anaapisha balozi mmoja LiVE!
Hajiamini sijui kwanini!
Ni kweli kabisa, siasa za ushindani ni muhimu sana hata kama unafanya mazuri, pasi na ushindani hakuna ubunifu wala uwajibikaji, hii ipo hata kwenye biashara na elimu.
 
Anaingia madarakani 2015 rate ya dola ilikua 2,160/=!

Nashangaa hiyo 2,315/= mnasema kasaidia nchi nashindwa kuwaelewa!

Rate imepanda kwa shilingi 155/= nzima!

Acheni umama nyie vichaa!
Screenshot 2019-03-30 14.45.21.png


Haya ndio mambo yale yale anayofanya kila siku.

Tengeneza tatizo wewe mwenyewe halafu jifanye unalitatua,halafu kula utukufu wote.

Hili swala kalijenga mwenyewe baada ya kuharibu Bureau De Changes zote,bei zikapanda sasa anajifanya kurekebisha na it will not quietly come back to normal..Not at all!

Tunamjua Jiwe!

Anavuruga kwa makusudi kabisa halafu anajifanya kurekebisha with no success!

Nonsense hizi!
 
Back
Top Bottom