Hali ya Ngorongoro na wanahabari wanaoshinikiza Wamasaai waondolewe hawajui chochote wanatumika vibaya bila kujua

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Nov 18, 2014
424
1,044
Wakati watu wanashinikiza wanangorongoro waondolewa nawakumbusha kuna amri ya mahakama ya Afrika Mashariki EACJ inaikataza Serikali kuwaondoa, na serikali imekuwa ikiheshimu amri hiyo toka Sept 2018, tunataka Serikali isiyo heshimu utawala wa sheria? #Ngorongoro

View attachment 2109658View attachment 2109660View attachment 2109661View attachment 2109662

Eneo la Ngorongoro asili, lilikuwa sehemu ya Serengeti National Park wakati linaundwa na waingereza 1951. Maasai waliendelea kuishi eneo hifadhi mpya hadi 1959, wakati mgogoro na mamlaka za hifadhi kuhusu matumizi ya ardhi, waingereza wakawahamishia Ngorongoro Conservation Area.

59% ya ardhi ya wilaya Ngorongoro ipo Ngorongoro Conservation Area, ambayo ilirasimishwa 1959 kuhusika na masuala ya conservation za rasilimali za wanyama pori, kukuza utalii na maendeleo ya wakazi ndani ya hifadhi, Maasai ambayo ni jamii ya wafugaji wenye kuhama kutafuta malisho.

NCA ni eneo la 8,292 km2 ndani ya wilaya ya Ngorongoro, mkoa wa Arusha. Kuna vijiji 14 ndani ya Ngorongoro Conservation Area (NCA), kata 6 za Kakesio, Orbalbal, Endulen, Nainokanoka, Ngorongoro na Naiyobi na kata hizo zina wakazi zaidi ya 50,000 kwa sensa ya 2002.

Loliondo, ambayo pia imegawanyika katika kata na vijiji kadhaa, ni asili ya Maasai ambao kwa asili ni wafugaji na sasa kwa mahitaji ya binadamu wanalima mazao. Pia kuna jamii ya Batemi (Sonjo) na jamii nyingine ambazo pia zinaishi Loliondo, ni wakulima na pia wafugaji.

Mgawanyo huo unatengeneza vijiji vya Loliondo, Sakala, Ngwarrwa/Enguserosambu, Ololosokwan, Oloipir, Arash na Maloni. Tinaga, Mgongo, Kisangiro, Samunge, Yasimdito, Digodigo, Malambo, Piyaya, Pinyinui na Engaresero. Wakazi wengi ni wafugaji na wakulima.

Mgawanyo wa makaazi unatofautishwa na tofauti yao ubora wa rasilimali, nyanja za uzalishaji mali, historia na mila za wakaazi. Kuna upinzani wa asili wa kiuchumi kati ya jamii za Maasai na Batemi (Sonjo) na Loliondo.

Pia soma > Nakuonya Maulid Kitenge , propaganda ulizotumwa kuzifanya kwa wana- Ngorongoro dhidi yao hazitakuacha salama.

20220206_084544.jpg
 
Wasiondolewe..ila iwepo population density inayoweza kuendana na eneo husika...tofauti na hapo hakuna uhai wa ngorongoro.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kama awali walikuwa eneo la Serengeti wakahamishwa na kusogezwa mbele na kuwa eneo la Ngorongoro kwa nini ishindikane kuhama kutoka Ngorongoro? Je, ikifanyika sensa ya kushtukiza (maana ikitolewa taarifa wanaweza kuondoka wengine kupisha sensa kisha warudi baadae) idadi ya watu waliokuwepo kipindi wanahamishwa miaka hiyo na leo ipo sawa? Hifadhi hiyo ni mali ya watanzania wote. Sasa hatuwezi kutulia tu tukiona hifadhi ipo hatarini.

Kwa kweli nilipata nafasi ya kuingia kutalii Ngorongoro, Serengeti, Manyara n.k; muingiliano wa watu, mifugo na wanyama pori ni mkubwa sn Ngorongoro. Mwisho itakuja kupoteza ule uasili wa wanyama pori.

Sent from my TECNO CC7 using JamiiForums mobile app
 
Kama awali walikuwa eneo la Serengeti wakahamishwa na kusogezwa mbele na kuwa eneo la Ngorongoro kwa nini ishindikane kuhama kutoka Ngorongoro? Je ikifanyika sensa ya kushtukiza (maana ikitolewa taarifa wanaweza kuondoka wengine kupisha sensa kisha warudi baadae) idadi ya watu waliokuwepo kipindi wanahamishwa miaka hiyo na leo ipo sawa? Hifadhi hiyo ni mali ya watanzania wote. Sasa hatuwezi kutulia tu tukiona hifadhi ipo hatarini.

Kwa kweli nilipata nafasi ya kuingia kutalii Ngorongoro, Serengeti, Manyara n.k; muingiliano wa watu, mifugo na wanyama pori ni mkubwa sn Ngorongoro. Mwisho itakuja kupoteza ule uasili wa wanyama pori.

Sent from my TECNO CC7 using JamiiForums mobile app
Tunajua mmetumwa lkn nikwambie tuu,hatuondoki n'gooo
 
Kwenye somo la maarifa ya jamii huwa kuna swali, hifadhi ya wanyama Tanzania ambayo huishi binadamu na wanyama jibu huwa Ngorongoro.
 
Nimefanikiwa kutembelea hii hifadhi kiuhalisia inaumiza sana. Unaenda umbali mrefu mno lkn huoni wanna wanyama pori zaidi ya zebra na nyumbu.

Ni kweli wanaishi kihalali lkn serikali ilifail kufanya forecasting hakuna jamii isiyokua.otherwise wamehasiwa.

Kanuni zitengenezwe

Kusupport hali iliyopo na watafute maeneo tengefu yatakayo wa accommodate na yatakayokuwa huduma zote muhimu za kijamii.
Ile sifa tena ya wanyama pori kuishi na binadamu inaumiza hifadhi
 
Watu hawaifahamu hiyo Mbuga asili yake wanaangalia tu clip za kitenge aliyezaliwa kariakoo

Hajawahi kufika hata porini bali kwa msaada wa mabeberu.
 
Watu hawaifahamu hiyo Mbuga asili yake wanaangalia tu clip za kitenge aliyezaliwa kariakoo

Hajawahi kufika hata porini bali kwa msaada wa mabeberu.
Kitenge mndengereko ,mndengereko na wanyama pori wapi na wapi ? yeye uwezo wake ni kuandika habari za ngoma za watu wa pwani za vigodoro , baikoko,kangamoko nk
 
Back
Top Bottom