SoC01 Hali ya mfumo wa elimu nchi na ni nini cha kufanya

Stories of Change - 2021 Competition
Aug 21, 2021
1
2
HALI YA MFUMO WA ELIMU NCHI NA NI NINI CHA KUFANYA.

Habari jamii forum na jukwaa zima la stories of change.

Utangulizi

Ndani ya andiko hili nitagusia mfumo mzima wa elimu jinsi unavyoendeshwa ndani ya nchi yetu ya Tanzania, na pia nitagusia ni jinsi gani tunapaswa kujiandaa na maisha baada ya masomo yetu tukiwa bado tuna soma hasa kwa wale wa vyuo na nini serikali inapaswa kukifanya na baada ya hapo ni hitimisho.

Mfumo wa elimu wa Tanzania unaendeshwa kwa njia ya nadharia Zaidi na sio vitendo na hii imepelekea Tanzania kuzalisha wataalamu wengi wasiokidhi vigezo katika soko la ajira kimataifa kwani ajira nyingi zinazo patikana kwa sasa zinategemea Zaidi vitendo juu ya taaluma husika na sio nadharia tu na jambo hili kupelekea elimu ndani ya Tanzania kuonekana kama imeshuka thamani. Na wengi wanalitazama jambo hili kama chanzo cha mlundikano wa wataalamu wengi waliohitimu vyuo kwa muda mrefu kubaki mtaani wakisubiri ajira za ndani kutokana na kukosa sifa za ushindani wa kuajiriwa kimataifa, na ndio sababu kubwa kuwa ni vigumu kumkuta mtanzania aliyeajiriwa nje ya nchi lakini pia hata ukiangalia waalamu wengi pamoja na viongozi wetu wa ngazi za juu za serikali ukifuatilia Zaidi kusoma kwao utakuta wengi wamehitimu katika vyuo vya nje ya Tanzania.

Hivyi basi kutokana na mfumo mzima wa elimu wa Tanzania kuonekana kutokuwa na matoke chanya Zaidi na kupelekea kuwa na watalaamu/wahitimu wengi mtaani wasio na ajira ni vizuri maandalizi ya kijana kisaikolojia yaanze mapema toka akiwa bado chuoni juu ya maisha atakayo kwenda kuishi mara baada ya kuhitimu na hapa anapaswa kutambua kuwa:-

Chuo ni sehemu(level) ya juu sana kimasomo lakini pia anapaswa kutambua kuwa chuo ni chekechea ya maisha, na kanuni ni zile zile kama tulivyokuwa kwenye chekechea za masoma A E I O U zinaendelea kutumika

A -Anza kupanga na kutekeleza mikakati na mipango yako itakayo kupelekea kutimiza ndoto ya maisha yako,

E -Endeleza mahusiano yote yenye kukupa motisha au changamoto zitakazopelekea kutimiza ndoto/maono yako,

I -Ishi vizuri na watu huku ukitengeneza miunganiko chanya yenye faida kwani kauli njema ya shinda tajiri,

O -Ondoa hofu, aibu na jiamini juu ya changamoto zote unazokutana nazo katika kutafuta kwako,

U -Usiache kumtanguliza Mungu mbele juu ya jambo lolote unaloliendea.

Endapo kijana ataenda sambamba na mpangilio mzima wa irabu hizo hapo juu toka akiwa shuleni atajikuta mwenye Amani na ataweza kuwaza Zaidi kujiajiri na kutumia fursa zilizopo kuliko kuwaza kuajiriwa tena na ataona elimu aliyoipata ni kama daraja la kumvusha yeye kufikia malengo yake na sio kigezo tena cha kuweza kuajiriwa.

Usione aibu kushiriki katika fursa zinazotokea mbele yako na uzichukulie kama sehemu ya kutokea kimaisha.

Jihusishe na shughuli tofauti tofauti za ujasiriamali toka ukiwa shule/chuo kwani ndio msingi wa kukujenga juu ya shughuli zako baada ya masomo na ndio sehemu ya kuchukulia uzoefu.

Jukwaa au sehemu yoyote itakayo kupa fursa ya kukionesha kile ulicho nacho yaweza kuwa kipaji pamoja na juzi mbalimbali usiogope ona kama ndio fursa pekee ya dunia kutambua kile ulicho nacho hivyo fanya kwa ustadi wa hali ya juu sana.

Jione wewe ni wathamani na ona kile unachokifanya chaweza kubadii hali ya maisha ya ulimwengu katika njia chanya.

Shiriki na fuatilia semina mbali mbali za ujasiriamali na vikundi.

JUKUMU LA SERIKALI KATIKA UBORESHAJI WA MIFUMO YA ELIMU PAMOJA NA UPUNGUZAJI WA WIMBI LA WATAALAMU MITAANI WASIOKUWA NA SHUGHULI MAALUMU.

Serikali inapaswa kuimarisha mfumo mzima wa elimu kwa kutoa elimu kwa njia ya vitendo Zaidi kuliko nadharia ili kuandaa wataalamu watakao kubalika sehemu mbali mbali hata nje ya nchi kwani watkuwa na uwezo mkubwa wa vitendo kuliko maelezo.

Serikali inapaswa kuwaamini na kuwatumia Zaidi waatalamu waliozalishwa ndani ya nchi katika ujenzi na uimarishaji wa miundombinu yake ikiwemo wahandisi.

Serikali inapaswa kutoa fursa mbalimbali kwa vijana ikiwa ni pamoja na utoaji wa mikopo itakayo wawezesha vijana kujiajiri na kuendesha shughuli zao za ujasiriamali

HITIMISHO

Kwahayo machache naomba kuwasilisha kwenu kwani naona yanaweza kuchangia kwakiasi kikubwa mabadiliko ya mifumo yetu ya elimu lakini pia yanaweza kumfungua kijana kifikra juu ya nini cha kufanya baada ya kumaliza masomo yake.

NIWATIE MOYO VIJANA WENZANGU TUPAMBANE IPO SIKU TUTAFANIKIWA KWANI MGAAGA NA UPWA HALI WALI MKAVU.
 
Back
Top Bottom