Hali ya maji wilayani Monduli ni tete, wananchi wanakunywa maji ya madimbwi na mifugo. Lowassa hadi Kalanga huraaaaaahhh.

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,310
6,605
Ktk pitapita zangu najikuta natua wilayani Monduli ambapo maji ni tabu kama Tabora na Mtwara ambapo pia nimepita. Kwa kweli wananchi ktk maeneo haya haswa Monduli wanachangia maji machafu ya madimbwi na mabwawa na mifugo.

Sasa najiuliza ile Monduli ya Lowassa ndiyo hii? Nikaambiwa kuna Mbunge kijana Kalanga Mkimbizi kutoka Chadema na sasa CCM, lakini hali ni ile ile. Tukiwa maeneo mbalimbali ya nchini mwetu tunasikia Monduli ni kama ulaya. Usidanganywe hakuna kitu pale. Kuanzia Makuyuni, selela, Nanja, Moita, Loksalie, Esilalei, Noolarami, Elwai nk maji ni shida tupu. Sijui kama nimeweza kutamka na kuandika vizuri majina ya maeneo haya kwani nimesaidiwa na wenyeji. Nitafanya utafiti kidogo juu ya waterborne diseases (magonjwa yaambukizwayo na maji) ktk hospital ya wilaya ya Monduli na vituo vyake vya Afya nije na mrejesho. Hata kijijini kwa Mbunge Kalanga na mstaafu Lowassa unaambiwa hakuna maji japo sijafika.
 
Hao wanacho jua ni ushabiki mkuu. Yaani na hio ndo mitaji ya watawala. Wacha tu waendelee kuwa hivyo.
 
Maeneo yote ya wamasai hali ni mbaya hasa huduma za kijamii nenda Longido nenda Simanjiro nenda Ngorongoro kote ni the same tu. Na hao ndo mitaji mikuu ya CCM.
Huku kwetu Engaruka ndio kabisaaa punda wetu wamechoka kufuata maji mbali.
Kalanga originally alikuwa CCM huko chadema alienda tu kutalii akimfuata Lowassa.
 
Kwani kwenye kampeni niliwaambia ntaleta ukame!? Hahaha niliwaambia CCM italeta ukame?! Acheni sisi tuwatumikie wananchi wetu maskini nyie kaeni tu kutumiwa na mabeberu.
 
Katika Kampeni CCM ilisema italeta Maji,na kwanini wananchi wetu ni Maskini?wakati hii Nchi ni Tajiri kama Mh Rais anavyotuambia ?Tunatakiwa tuwatumikie wananchi Matajiri kama Nchi yao ilivyo tajiri
 
Hee ndio hivyo kabisa nakuunga mkono lazima tuhakikishe tunakua DONA KANTRI. Na kutembea kifua mbereee
 
Ktk pitapita zangu najikuta natua wilayani Monduli ambapo maji ni tabu kama Tabora na Mtwara ambapo pia nimepita. Kwa kweli wananchi ktk maeneo haya haswa Monduli wanachangia maji machafu ya madimbwi na mabwawa na mifugo.

Sasa najiuliza ile Monduli ya Lowassa ndiyo hii? Nikaambiwa kuna Mbunge kijana Kalanga Mkimbizi kutoka Chadema na sasa CCM, lakini hali ni ile ile. Tukiwa maeneo mbalimbali ya nchini mwetu tunasikia Monduli ni kama ulaya. Usidanganywe hakuna kitu pale. Kuanzia Makuyuni, selela, Nanja, Moita, Loksalie, Esilalei, Noolarami, Elwai nk maji ni shida tupu. Sijui kama nimeweza kutamka na kuandika vizuri majina ya maeneo haya kwani nimesaidiwa na wenyeji. Nitafanya utafiti kidogo juu ya waterborne diseases (magonjwa yaambukizwayo na maji) ktk hospital ya wilaya ya Monduli na vituo vyake vya Afya nije na mrejesho. Hata kijijini kwa Mbunge Kalanga na mstaafu Lowassa unaambiwa hakuna maji japo sijafika.
Usitoe hoja ya jumla jumla. Angalia pia changamoto ya Monduli ya 1995 na changamoto za 2019. Kuna improvement ya hali ya juu. Lowassa hakupeleka nguvu sana kwenye swala la maji kwa sababu alifahamu ugumu wake. Nguvu kubwa alielekeza kwenye elimu na afya. Aliamini wananchi wa jimbo lake wakipata elimu wataweza kujiletea maendeleo na hata kudai huduma hiyo ya maji kwa serikali au kuomba kwa wadau.

Hata hivyo kwenye swala la maji juhudi nyingi zimefanyika lakini hatuwezi kumlaumu mbunge yeyote kwa sababu uwekezaji unaohitajika ili hivyo vijiji vipate mtandao wa maji, sio wa kitoto, sio swala la Mbunge. Ili hivyo vijiji vipate maji tunahitaji mradi mkubwa kama ule unaoendelea Arusha DC, Meru DC na Arusha CC yaani zaidi ya Tzs. 500 Bn.
 
Nilishawambia watanzania tembeeni kifua mbele, nyinyi ni matajirii. kama dege kubwa kama hili linaweza kushuka hapa na limenunuliwa kwa pesa zenu tena cash, hiiii bhagosha!
 
Back
Top Bottom