Uchaguzi 2020 Hali ya maisha mtaani ni ngumu mno

share

JF-Expert Member
Nov 22, 2008
6,062
10,461
Sasa ni dhahiri kuwa hali ya maisha Tanzania inakatisha tamaa. Ni ngumu mno kiwango cha juu kinachokera na kuumiza.

Pamoja na ulofa mtu aliokuwa nao lakini tangu aamke asubuhi mpaka jioni atakuwa amefuatwa na watu wasiopungua 5 waliomfuata wakiomba mkopo huku yeye mwenyewe pia akiwa katika msako wa mkopo.

Yaani kila mmoja anamfikiria mwenzake labda ana unafuu fulani, kumbe siyo.

Wote tupo kwenye msoto mkali. Miaka 5 ya utawala huu imetufikisha hapa! Sasa wanakuja tena kuomba kura eti wamenunua ndege!

Tuna JAMBO LETU 28/10/2020.
 
Maisha ni magumu, fedha haipatikani, vitu vinapanda bei, kodi kubwa na ajira hazipo. Halafu mtu anasema uchumi wa kati. Na Chanzo cha matatizo tunakifahamu na oktoba 28 inabidi tukitoe kwa kumpa kura Lissu.

Watanzania tuungane Oktoba 28 kumpa kura zote Lissu.
 
Nimeota ujue hata mkipiga kura, wasimamizi wa uchaguzi hawatatangaza mpinzani kama ilivyokuwa serikali za mitaa na chaguzi zilizorudiwa.

Ndoto yangu ni ya ukweli kwa hiyo tujiandae kisaikolojia miaka mingine 5 kuwa na huyu jamaa unless Mungu aingilie kati tu.

Na safari hii atafanya anachotaka, hata viboko mtapigwa heeeee
 
Nimeota ujue hata mkipiga kura ,wasimamizi wa uchaguzi hawatatangaza mpinzani kama ilivyokuwa serikali za mitaa na chaguzi zilizorudiwa.

Ndoto yangu niya ukweli kwa hiyo tujiandae kisaikologia miaka mingine 5 kuwa na huyu jamaa unless Mungu aingilie kati tu .

Na safari hii atafanya anachotaka ,hata viboko mtapigwa heeeee
Sure, round ya pili ataburuza watu sana kama kisasi cha kumshangilia Lissu.
 
Ni muhimu kuhakikisha unakwenda na mwenza wako kiliniki mara ahisipo kuwa mjamzito, mhimize atimize mahudhurio yote 8 (ikiwezekana) pia mkumbushe mtoa huduma swala la kupima HIV/AIDS

Ka ilivyokuwa utamu na karaha wakati mkiwa faragha, hali kadhalika ni muhimu kumuhudumia ktk nyanja zote, hata kumpikia kwa kipindi chote cha ujauzito na mara baada ya kujifungua

NB - I hate politics
 
Vyuma vilivyobana ndivyo vinampigia kampeni ya kisirisiri Tundu lissu maana watanzania wote tumeathirika na vyuma vilivyobana na watanzania tukilalamika hali ni ngumu tunaitwa wavivu na wapiga dili. Sasa sisi watanzania kwa umoja wetu tuungane kwa pamoja kumpa kura za kishindo Lissu ili atuokoe na hali ngumu.

Oktoba 28 tuna jambo letu, kura zote kwa lissu.
 
Ni muhimu kuhakikisha unakwenda na mwenza wako kiliniki mara ahisipo kuwa mjamzito, mhimize atimize mahudhurio yote 8 (ikiwezekana) pia mkumbushe mtoa huduma swala la kupima HIV/AIDS

Ka ilivyokuwa utamu na karaha wakati mkiwa faragha, hali kadhalika ni muhimu kumuhudumia ktk nyanja zote, hata kumpikia kwa kipindi chote cha ujauzito na mara baada ya kujifungua

NB - I hate politics
Mkishadekezwa badaye mnaota mapembe kabisa
 
Mjini mnatafuta nini wajameni? Acha kuishi mjini kwa kubangaiza mtu anatembeza mikanda 3 ya suruali, key holder kuanzia jua linachomoza hadi giza linaingia eti naye anasema vyuma vimekaza! Njoo huku kijijini maisha raha na hivi tumepatiwa umeme wa REA, barabara za lami na treni za umeme zinakaribia kuja, nk maziwa, viazi, mahindi, misosi ya kumwaga!

Nje ya mada: Kumbe Trump wa Marekani Tangu awe rais amelipa kodi ya US$ 750 tu? Urais ni dili!!
 
Back
Top Bottom