Hali ya kituo cha mabasi Makumbusho - Dar yazidi kuwa mbaya

kisiki kizito

JF-Expert Member
Jul 3, 2015
676
858
Habarii Wakuu!!!
Natumaimi mmeamka salama, Ila kuna kero moja imekuwa sugu sana katika jiji letu na sijui mamlaka zinazosimamia hususani Manispaa ya Kinondoni hazilioni hili tatizo...!?

Barabara za kuingia stand ya Makumbusho kwa wanaotokea Posta au Tegeta imekuwa ni mbaya sana na changamoto kubwa kwa abiria na pia inapelekea wananchi wanaounganisha magari kwenda sehemu mbalimbali kuingia gharama ya Muda na mali.

Tunaziomba hizi mamlaka zinazosimamia ujenzi wa Barabara hizi utusaidie wananchi kurekebisha kwa haraka matatizo haya kwani kunaondoa sifa na uzuri wa sehemu husika na pia kukwamisha biadhara za watu
FB_IMG_1495519900416.jpg
FB_IMG_1495519896895.jpg
FB_IMG_1495519893206.jpg
FB_IMG_1495519889336.jpg
FB_IMG_1495519885900.jpg
 
Hapo ni kilometa kadhaa tu kutoka Ikulu. Hilo Ndilo Jiji kuu Tanzania. Hapo ndipo kioo cha tanzania. Ni aibu kubwa sana sana. Moja ya sababu hadi inakuwa namna hii ni migongano na migogoro makazini
 
Ngoja wajenge nyumba za waheshimiwa walio na mahekalu, kununua ndege kwanza na mashangingi au BMWs, wakimaliza watakuja kurekebisha miundo mbinu!
 
Hapo ni kilometa kadhaa tu kutoka Ikulu. Hilo Ndilo Jiji kuu Tanzania. Hapo ndipo kioo cha tanzania. Ni aibu kubwa sana sana. Moja ya sababu hadi inakuwa namna hii ni migongano na migogoro makazini
Unayosema ni Kweli,,, wananchi wa chini tunadharaulika Sanaa,, ususani kwenye huduma zetu
 
barabara za pembezoni za kituo zote na za kuingilia zinatengenezwa kuna baadhi zimekamikika nusu nyingne bado nadhani ni kutokana mvua zinazoendelea imekuwa changamoto katika umariziaji ila hizo zote pichani na ulizosema zipo katika UJENZI sasa tena kiwango cha lami watumiaji na wakazi wa huku hatulalamiki usumbufu huu 7bu tunajua nini kinaendelea sasa na si kingine ni ujenzi ila mvua ndo zinayeyusha
 
Ila nadhani washaanza kukirekebisha hiki kituo... Ukitokea mwananyamala wametengeneza barabara nzuri kweli mpaka kituoni! Tusubiri tu watafika huko mbele
 
barabara za pembezoni za kituo zote na za kuingilia zinatengenezwa kuna baadhi zimekamikika nusu nyingne bado nadhani ni kutokana mvua zinazoendelea imekuwa changamoto katika umariziaji ila hizo zote pichani na ulizosema zipo katika UJENZI sasa tena kiwango cha lami watumiaji na wakazi wa huku hatulalamiki usumbufu huu 7bu tunajua nini kinaendelea sasa na si kingine ni ujenzi ila mvua ndo zinayeyusha
Tunashukuru kwa taarifa!! Ingawa mvua si sababu ya hiyo hali. Hata kuweka vifusi na kutengeneza mitaro ya maji yawe dispatched vizuri ili kuzuia matope yale nako inashindikana. Je, mvua hizi zikiendelea hadi december hali itakuwaje? Naimani hata nyie mnaokaa hayo maeneo mtalazimika kuhama ili kupisha maji na matope yatakayokuwa yanaingia hadi majumbani mwenu.
 
Back
Top Bottom