Hali ya kisiasa Tanzania ktk miezi tisa iliyopita ya mwaka 2012 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali ya kisiasa Tanzania ktk miezi tisa iliyopita ya mwaka 2012

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bagamoyo, Sep 25, 2012.

 1. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,519
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  WANABODI JAMIIFORUMS

  Hali ya Kisiasa Tanzania katika miezi 9 iliyopita inyaoishia September 30 mwaka 2012.

  CHAMA TAWALA (CCM) CHAPOTEZA NGUVU

  Chama tawala CCM yaani chama chenye serikali kiimezidi kupoteza hatamu ya ushawishi ktk maamuzi yote ya mihili minne ya nchi yaani Bunge, Mahakama, dola (executive) na Media (vyombo vya habari).

  BUNGENI
  Tumeshuhudia jinsi vyama vya upinzani hasahasa CHADEMA kikiweza kuongeza ushawishi wa hoja Bungeni na kukifanya chama tawala CCM kuonekana kama chama pinzani huku CHADEMA ikionekana mbele ya wananchi kuwa kina ajenda ya kweli ktk kutetea mustakabali wa nchi mbali ya kuwa CHADEMA kina idadi ndogo ya wabunge Bungeni.

  MAHAKAMA

  Kitendo cha CHADEMA kuonesha mapungufu ya baadhi ya majaji wateuliwa katika uwezo wao kitaaluma na kiutendaji ni pigo jingine kwa serikali ya CCM kuhusu umakini wa serikali ya CCM katika uteuzi wa baadhi ya majaji. Na mpaka sasa serikali ya CCM imeshindwa kutoa tamko kukazia uteuzi wa majaji hao au kutengua uteuzi wao.

  DOLA
  Katika siku za karibuni kelele za kuwa vyama vya upinzani vilikuwa havitendewi haki na POLISI katika kupewa nafasi ya kujitangaza kupitia maandamano, mikutano na ufunguzi wa matawi yao kama mujubi wa sheria na katiba unavyoruhusu, ghafla umebadilika.

  Na hali hivyo ya mabadiliko imetokana hasahasa na CHADEMA kuibinya serikali na POLISI kuheshimu sheria na katiba juu ya vyama vingi kupewa nafasi ya kujiimarisha. Tukio la kifo cha mwandishi wa habari huko Iringa katika ufunguzi wa tawi la CHADEMA ndiyo umeleta mabadiliko haya ya ghafla.

  Tunaona jumuiya mbalimbali za watanzania iwe kupitia vyama vya siasa au jumuiya za kidini wamepata nguvu ya kuweza kufanya maandamano, mikusanyiko huku wakilindwa na POLISI wakati miezi michache iliyopita POLISI walikuwa wakitumia nguvu kubwa kupitia kiasi kuhakikisha mikusanyiko, uzinduzi, maandamano hayafanyiki kwa vile Mkuu wa Wilaya DC, MKUU wa Mkoa RC au POLISI ambao wote ni wateuliwa wa serikali ya CCM walikuwa wanaona ni tishio kisiasa.


  MEDIA
  Vyombo vya habari kama vituo vya redio, televisheni, magazeti na mitandao ya jamii vimekuwa sasa vikiandika habari kwa uhuru kubwa zaidi ingawa bado vinajifanyia vyenyewe censorship kwa uwoga wa kuwa wataiudhi serikali. Lakini kwa uhakika vyombo hivi vya media taratibu vinaanza kuacha woga na ndiyo maana baadhi ya vyombo vya media vimepachikwa jina kuna vinashabikia 'CHADEMA'. Hali hii ni nzuri inaashiria watanzania wanaweza kutoa maoni yao jinsi wanavyoona bila woga.

  HITIMISHO
  Hali hii mpya ya kisiasa Tanzania imeanza kuiogopesha chama tawala na hata kama wanafanya mikutano ya NEC- CCM Dodoma lazima watamke CCM haiko mahututi na siyo katk ngazi ya NEC- CCM bali hata ngazi za CCM- MKOA, CCM-WILAYA, CCM-KATA, CCM-NYUMBA KUMI hofu hiyo ya mazoea ya kuona wanapoteza kushika hatamu ya ushawishi, uongozi n.k umetamalaki.

  VYANZO/SOURCE:
  Thread mbalimbali wa wanaJamiiforums, media za Tanzania, Matamko ya NEC-CCM, KAMATI KUU CHADEMA
   
 2. k

  kilaboy Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 25
  Na hii ni Sep 2012 sipati picha ifikapo October 2015,
  yani CCM itakuwa imepotea kabisa katika ulimwengu
  huu wa siasa za Tanzania.

  Hata uku vijijini kwa sasa CCM imepoteza mvuto kabisa
  tena si kwa vijana tu hata kwa wazee CCM haipo tena,
   
 3. Mhamiaji Haramu

  Mhamiaji Haramu Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bado jumanne malecela anaamini ccm itashinda kwa kishindo 2015, ana akili kama za mwanae
   
 4. t

  thatha JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Ulikuwa unalengo la kuelezea hali ya kisiasa nchini au kukandia Serikali iliyoko madarakani? Huna upeo wowote wa kuelezea hali ya kisiasa nchini wewe zaidi ya umbea 2. Sijaona ukisema siasa zilivyopelekea watu kupoteza maisha kwa sababu tu eti Vyama vya siasa vimekaidi amri ya kutofanya mikutano na maandamnano.

  Sijaona ukigusia namna ambavyo siasa zimechangia migomo ya wafanyakazi na hata kupelekea vifo vya wagonjwa ambao wangeweza kupona haraka tu. Sijaona ukielezea baadhi ya Wanasiasa waliingia mitafaruku na vyma vyao , mfano Hamad Rashid, ZITTO Kabwe, Kafurila na wengine wengi.

  Ni hali gani ya kisiasa wewe ulioongelea kama hujagusia utenguaji wa matokeo ya chaguzi mbalimbali nchini hasa za Ubunge?. JF lini tutakuwa na upeo wa kuwasilisha mada zenye kuendana na vichwa vya mada hizo? Lipi geni ambalo umelisema hapo,ambalo haliko katika nyimbo za kila siku za vyama vya siasa katika kujihakikisha uhao wake.

  Bila kujali vinapotosha wananchi na kurudisha nyumba juhudi za serikali za kuwaletea maendeleo wananchi na kuhatarisha amani tulioizoea?.
   
 5. t

  thatha JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hizi nyimbo hazina tofauti na zile za akina marijane Rajab, Moro Jaz, Tabora Jaz nyingine nyingi ambazo ni zilipendwa.
   
 6. t

  thatha JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hao ndo wazee wenyewe wenye kupima upepo wa kisiasa. Siyo pekee hata wananchi wa kawaida wameshawaona wapinzani ni wazushi tu.
   
 7. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Ccm imebaki ktk mdomo wa Nape tu,Mukama hajulikani alipo.
   
 8. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Mamaisara una juhudi kweli,nadhani wewe ni mmoja unaenufaika na mfumo.USIPAMBANE TU HUMU KUWATETEA MAGAMBA PIA ITISHA MIKUTANO wewe na Mukama tuone kukubalika kwenu.
   
 9. I

  Iramba Junior Member

  #9
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ama kweli leo nimeamini kweli mtaji wa CCM ni ujinga na umasikini wa watanzania kwani mtu mwenye akili timamu ambaye si mwehu ni vigumu ku argue kama hivi

  "Sijaona ukisema siasa zilivyopelekea watu kupoteza maisha kwa sababu tu eti Vyama vya siasa vimekaidi amri ya kutofanya mikutano na maandamnano"

   
 10. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 160
  ...mbona povu linakutoka hivyo...hauitaji nguvu nyiiingi kutetea jambo jema linaloonekana bayana...kama haukubaliani na huu uchambuzi leta wako...acha kupoteza muda wako mzuri kutetea ujinga...ni amri zipi za polisi zilizokaidiwa?,je ni zile za kuizuia Chadema kuendelea na M4C na kuiruhusu CCM kuzindua kampeni za uchaguzi mdogo wa Bububu!?...jaribu kuishirikisha akili yako katika kufikiri,hizo hoja zako mlegeza zinakudharaulisha...
   
 11. jason

  jason JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 295
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Na mamaisara naye bado yupo
   
 12. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2012
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,519
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mmoja wa wafuasi wa kikundi cha waislamu wenye imani kali akidhibitiwa na polisi mara baada ya kukamatwa leo 17/10/2012 katika kituo kikuu cha polisi Kati wakijaribu kuandamana ili kushinikiza kiongozi wao Katibu wa Taasisi za Kiislamu Shekh Ponda Issa Ponda kuachiwa na jeshi la polisi mara baada ya kukamatwa jijini Dar es salaam kwa kudaiwa kusababisha vurugujijini Dar es salaam.


  [​IMG]
  Polisi wakiwa tayari kwa kudhibiti maandamano hayo katika o kikuu cha Reli karibu na polisi kati jijini Dar es salaam leo mchana 17/10/2012

  HALI YA KISIASA DOLA IKIPEWA 'CHANGAMOTO' NA VIKUNDI MBALIMBALI

  Hali ya kisiasa ya dola (state) kutingishwa na madai mbalimbali toka kila aina ya vikundi vya kijamii Tanzania.

  Je, dola na serikali yake ya CCM ipotayari kukabiliana na hali hii mpya ya changamoto? Kwangu mie naona serikali ya CCM imejisahau katika ujenzi-endelevu wa Taifa la Tanzania.

  Mwalimu Nyerere alikuwa na uwezo wa kufanya maamuzi magumu kama kutaifisha shule za madhehebu ya Kikristo ila vijana wa ki-Tanzania waweze kuchanganyika. Mwalimu Nyerere na serikali yake aliweza kutoa warranti za usafiri wa bure ili kijana wa Mtwara akasome Bukoba na kijana wa Bukoba akasome Kilimanjaro. Mwalimu Nyerere aliwawezesha vijana wa ki-Tanzania kutambuana kwa kuwapeleka JKT kwa mujibu wa sheria.

  Tatizo la sasa ni kuwa dola imejisahau na kufikiri kazi ya ujenzi wa ki-Taifa alioufanya Mwalimu Nyerere kwa pamoja na viongozi wenzake kipindi cha TANU baada ya uhuru imemelizika.

  Tutaona dola ikitikiswa na vikundi vya kidini, dola kutokuwa tayari kupokezana uongozi wa nchi kama CCM ikishindwa uchaguzi, dola ikishindwa kuwa bunifu kuchochea ajira kwa vijana iwe ktk sekta ya umma, kujiajiri binafsi ktk biashara, uvuvi, kilimo n.k

  Hali hii siyo dalili nzuri kwa uwepo-endelevu wa Tanzania ya amani, utulivu na maisha bora kwa wote.

  [​IMG]
  Tarehe 27/09/2012 Polisi wakiwa kwenye magari yao wakifika na kuyaegesha magari yao upande wa pili wa barabara kwenye kituo cha mafuta kwa muda kabla ya kuondoka bila kufanya juhudi zozote za kuwazuia machinga hao kujitwalia eneo hilo.(Picha na Grace Macha)

  [​IMG]
  Septemba 2012, Wamachinga jiji la Arusha waliokosa eneo kwenye uwanja wa NMC jana wakigawana maeneo baada ya kuvunja uzio wa bati uliokuwa umezungushiwa kwenye uwanja ambao awali ulikuwa unamikiwa na Manispaa ya Arusha kabla ya kuuzwa kwa mtu binafsi karibu na Soko la Kilombero, Kata ya Ngarenaro
   
 13. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2012
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,519
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  Published on 17 Oct 2012 by ITV TANZANIAJeshi la polisi limetumia mabomu ya machozi kutawanya watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa katibu wa jumuiya na taasisi za Kiislam Tanzania sheikh Ponda Issa Ponda kushinikiza aachiwe huru baada ya kushikiliwa na jeshi la polisi kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo kudaiwa kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani jijini Dar Es Salaam.


  ITV TANZANIA youtube
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2012
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,519
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  Wananchi walia na jinsi serikali inavyofanya mambo chagalabaga ktk elimu, kilimo na ufugaji huko Mvomero, Morogoro

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2012
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,519
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  Tundiko la mdau Kiranja leo https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/340189-jopo-la-maaskofu-lakutana-mbagalai-latoa-tamko-zito.html:

  Nafikiri tamko la Maaskofu wa KKKT pia inatupa hali ya kisiasa nchini baada ya kuwa kimya wakitafakari mustakhabali wa nchi yetu na hatima ya uwezo wa viongozi wetu wa kisiasa ktk ujenzi wa umoja wakitaifa Tanzania:

  Jopo la Maaskofu lakutana Mbagalai, latoa tamko zito
  Maaskofu19 wa KKKT wanaongoza ibada maalum katika kanisa lao lililochomwa moto na wanatarajia kutoa tamko zito wakati wowote kuanzia sasa ambalo tutawaletea hapa.

  ============
  SALAAM ZA MAASKOFU WA KKKT KWA WATANZANIA WOTE KUHUSIANA NA MATUKIO YA KUCHOMA MOTO MAKANISA YA KIKRISTO ENEO LA MBAGALA – DSM.

  Wapendwa Katika Bwana,
  Waumini wa KKKT, Wakristo Wote na Watanzania kwa Ujumla.

  Neema na Iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu Kristo, Amina.

  Sisi maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za matukio ya uchomaji wa makanisa katika eneo hili la Mbagala. Tumekuwa katika mkutano wetu wa Mwaka wa Lutheran Mission Cooperation (LMC) huko Moshi pamoja na vyama vyote vya Kimissioni vya Ulaya na Marekani. Tumelazimika kukatisha mkutano huo ili kufika hapa Mbagala. Tumekuja kwa madhumuni makubwa matatu:


  1. Tumekuja kuwapa pole na kusimama pamoja nanyi katika uchungu mkubwa mlio nao. Machozi yenu ni machozi yetu. Machozi yetu ni machozi ya Kristo mwenyewe aliye Bwana wa kanisa linaloteswa. Jipeni moyo kwa kuwa yeye aliushinda ulimwengu (Yohana 16:33).
  2. Tumekuja kuonyesha majonzi yetu makubwa kwa vitendo vya uvunjifu wa amani, kuporomoka kwa umoja na mshikamano wa watanzania. Huu ni msiba mkubwa, na wenye msiba ni watanzania wote, wenye dini na wasio na dini.
  3. Tumekuja kushiriki pamoja nanyi kupokea matumaini ya Tanzania mpya. Katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa madhabahu ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa. Majivu haya na machozi yenu ni rutuba ya Tanzania mpya itakayojali upendo, uvumilivu, ustahimilivu, umoja, mshikamano, uhuru wa kuabudu na dola isiyo na dini.

  Katika ujio huu wa maaskofu hapa Mbagala, hatukuja hapa kufanya haya yafuatayo:


  1. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaokashifu dini za wenzao, wawe na ruhusa kutoka mamlaka zilizo juu au kama wanajituma wenyewe.
  2. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaodhalilisha misahafu ya dini; wawe wametumwa, kutegeshewa na mamlaka zozote au kwa misukumo ya utashi wao binafsi ili kupata kisingizo cha kugombanisha madhehebu ya dini.
  3. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaochoma makanisa na kuiba mali za makanisa kwa kisingizio cha kumtetea Mungu. Kisasi cha dhambi hiyo tunamwachia Mungu mwenyewe aliyedhihakiwa na walionajisi madhabahu yake.

  Wapendwa wana KKKT na watukuka sana, wana na mabinti wa Tanzania ya Julius Kambarage Nyerere; kilichotokea Mbagala katika wiki ya kuadhimisha siku ya Baba wa Taifa, ni kebehi si kwa Baba wa Taifa bali ni kebehi kwetu sisi wenyewe tunaokalia kiti alichokalia Baba wa Taifa. Yeye amelala baada ya kazi njema. Apumzike kwa amani na tunu zake zifufuke katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa amani na mshikamano wa Tanzania aliyoijenga.

  Kilichotokea Mbagala ni mateso ya kimbari, yaani mateso ya Kanisa (Persecution). Mateso haya ni matokeo ya mbegu ya magugu iliyopandwa katika bustani njema na sasa magugu hayo yanazaa matunda machungu. Dalili za mateso ya kimbari kama ilivyo kwa mateso ya kanisa; zilianza kitambo na hazikushughulikiwa na waliomrithi Baba wa Taifa. Dalili hizo ni kama hizi zifuatazo:


  • Uchochezi wa wazi kuwa taifa hili linaendeshwa na unaoitwa "mfumo Kristo", na kuwa Baba wa Taifa alaaniwe kwa yote aliyolitendea taifa hili.
  • Ubishi usio na tija juu ya idadi ya waumini wa dini mbalimbali hapa nchini na hata kudiriki kushawishi na kugomea zoezi la sensa ya watanzania. Lengo la ubishi huu ni mbegu inayoweza kuratibisha na kurasmisha mateso ya kimbari na mateso ya kanisa.
  • Matumizi mabaya ya baadhi vyombo vya habari, vyenye lengo la kujenga hofu ya kudumu na migawanyiko ya kidini miongoni mwa watanzania
  • Ukimya wa vyombo vya dola juu ya vitendo vya uvunjaji wa sheria ya matumizi ya vyombo vya habari. Kwa vyovyote vile, uvumilivu wa dola hauna maslahi mapana kwa mustakabali wa taifa letu na ni mateso ya kimbari, mateso kwa kanisa, na kwa wantanzania wote; wawe wengi dhidi ya wachache au wachache dhidi ya wengi.
  • Madai yasiyo ya kawaida na ya mara kwa mara kwa serikali inayodaiwa kutokuwa na dini. Madai hayo ni kama:
  1. Kulazimisha uvaaji wa alama za kidini katika taasisi za umma ili kurahisisha na kuratibisha tofauti za watanzania. Tunajiuliza: Likitokea la Mbagala katika mashule yetu na vyuo vya umma, watachomwa wangapi na kuuawa wangapi?
  2. Madai yanayojirudiarudia kutaka balozi za nchi fulani kufungwa hapa nchini. Madai haya yanaashiria kutaka balozi za nchi fulani tu ndiyo ziwe hapa nchini.
  3. Madai na mashinikizo ya Uanzishwaji wa mahakama za kidini hapa nchini
  4. Mashinikizo ya kidini yanayoingilia mifumo ya kitaaluma na kisheria.
  5. Mashinikizo ya kidini juu ya mfumo wa uteuzi wa watendaji wa serikali na katika ofisi za umma,
  6. Kuhoji na kupotosha juu ya ushirikiano wa serikali na mashirika ya dini katika utoaji wa huduma za kijamii hususan afya na elimu hapa nchini

  Wapendwa wana KKKT na Wapendwa watanzania wote. Hata kama wanaofanya mambo haya ya kusikitisha wametunukiwa hadhi ya kuitwa kuwa ni "wana harakati", tofauti na wanaharakati wanaotambuliwa na watanzania walio wengi, tunawiwa kuonya kwa uvumilivu wote kuwa uana harakati wao usitumike kuvunja nchi na sheria za nchi. Tanzania yenye amani na mshikamano ni tunda la dini zote, makabila yote, itikadi zote za vyama, rangi zote na hali zote za kiuchumi. Hata wasio na dini wanachangia amani ya nchi hii.

  Kwa macho na masikio yetu, tumeendelea kushuhudia vitendo vya uchomaji makanisa huko Zanzibar, Mwanza, Mdaula, Mto wa Mbu, Tunduru, Rufiji, Kigoma na sasa Mbagala. Wakati wote uvumilivu wa wakristo huenda umetafsiriwa kuwa ni unyonge na woga. Ikumbukwe kuwa hata wanyonge na waoga, hufika wakati wakasema "sasa basi" pale wanapodhalilishwa kupita kiasi. Hatuombei wakristo wafikishwe hapo.

  Tumeshuhudia wizara zetu zikivamiwa mchana kweupe na kushinikiza kuachiwa kwa watuhumiwa wa uhalifu; tumeshuhudia vituo vya polisi vikichomwa moto; mahakama zikilazimishwa kufunga shughuli zake, misikiti ikitekwa, uhai wa viongozi wa dini ukitishiwa hadharani na viongozi wastaafu wakizabwa vibao hadharani kwa sababu ya zinazoitwa harakati za kidini. Tumefikia kuhoji, watu hawa wavamie nini ndipo hatua zichukuliwe? Wachome nini ndipo viongozi wenye dhamana ya kulinda mali na uhai washtuke? Wamwue nani ndipo iaminike kuwa watu hawa ni tishio kwa usalama wa taifa letu?

  Sisi tulioitwa kwa njia ya nadhiri na viapo vitakatifu, tunawasihi sana waumini wa dini zetu na watanzania kwa ujumla, wenye wajibu wa kututii na wasiolazimika kututii, kuzingatia kuwa Mwenyezi Mungu analipenda taifa hili na watu wake. Kamwe hawezi kuliacha liangamie.

  Kwa Wakristo wote, huu ni wakati wa kuendelea kufunga na kuomba kwa ajili ya amani ya taifa hili. Mkristo wa kweli ni yule aliye tayari kuteswa kwa ajili ya Kristo na kanisa. Wakristo hatuko tayari kuua, kutesa, kulipiza kisasi ili kumtetea Kristo. Mungu wetu hatetewi kwa kuua wengine na kuchoma madhabahu ya dini nyingine.

  Katika mateso haya, kanisa litaimarika zaidi; na katika majivu haya ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa na ukombozi wa kweli utapatikana. Tunawataka wakiristo wote kusamehe na kuendelea kuwa raia wema. Kushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko ya kweli kwa kupitia njia sahihi zilizowekwa. Wakati wengine wanaweka mikakati ya kuchoma madhabahu, wakiristo tuweke mikakati ya kuomba na kushiriki vema katika haki zetu za uraia. Pamoja na kuwa wapole kama njiwa, imetupasa pia kuwa na busara kama nyoka (Mathayo 10:16).

  Daima tukumbuke kuwa, "KUSHINDANA KWETU SISI SI JUU YA DAMU NA NYAMA BALI NI JUU YA FALME NA MAMLAKA, JUU YA WAKUU WA GIZA HILI, JUU YA MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO" (Waefeso 6: 12).

  Ni sisi Maaskofu wenu kwa Neema ya Mungu,


  1. Askofu Dr. Alex G. Malasusa – Mkuu, KKKT na D/Mashariki na Pwani
  2. Askofu Dr. Stephen Munga –Mkuu, D/Kaskazini Mashariki
  3. Askofu Dr. Martin Shao – Mkuu, D/Kaskazini
  4. Askofu Dr. Thomas Laizer – Mkuu- D/Kaskazini Kati
  5. Askofu Dr. Benson Bagonza- Mkuu, D/Karagwe
  6. Askofu Isaya J. Mengele – Mkuu, D/Kusini
  7. Askofu Levis Sanga – Mkuu- D/Kusini Kati
  8. Askofu Elisa Buberwa – Mkuu –D/Kaskazini Magharibi
  9. Askofu Andrew Gulle – Mkuu, D/Mashariki ya Ziwa Victoria
  10. Askofu Michael Adam –Mkuu, D/Mkoani Mara
  11. Askofu Renard Mtenji – Mkuu, D/Ulanga-Kilombero
  12. Askofu Dr. Israel-Peter Mwakyolile – Mkuu, D/Konde
  13. Askofu Job Mbwilo – Mkuu, D/Kusini Magharibi
  14. Askofu Dr. Owdenburg Mdegella- Mkuu, D/Iringa
  15. Askofu Jacob Ole Mameo- Mkuu, D/Morogoro
  16. Askofu Zebedayo Daudi – Mkuu, D/Mbulu
  17. Askofu Paulo Akyoo – Mkuu, D/Meru
  18. Askofu Charles Mjema – Mkuu, D/Pare
  19. Askofu Mteule Amon Kinyunyu- Mkuu, D/Dodoma
  20. Askofu Mteule Dr. Alex Mkumbo- Mkuu, D/Kati  Mbagala, DSM, 18 Oktoba 2012.
   
 16. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2012
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,519
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  Hali ya kisiasa nchini yahitaji matamko rasmi toka kwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi Tanzania, Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete bila kuchelewa.

  Pia Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Rais Shein ambaye ni Mkuu wa Vikosi Maalum na Valantia, Zanzibar naye anatakiwa atoe tamko kuhusu hali hii ya vurugu.

  Wananchi wote wa bara na visiwani kwa sasa wana wasiwasi mkubwa na mstakabali wa maisha yao ya kila siku kwani kuna uwezekano ktokana na vurugu hizi hata wale wasio na hatia wanaweza kupata misukosuko kwa kuwa tu walikuwa wanapita nazao ktk maeneo ambayo ghafla yanakuwa uwanja wa fujo.
   
Loading...