Hali ya Kisiasa: Ridhiwan Kikwete anapumulia mashine Jimboni

hugochavez

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
1,907
1,009
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete anapumulia mashine Jimboni kutokana na hali mbaya ya kisiasa uchaguzi mkuu 2020 hali inayomfanya ashindwe kuhudhuria bunge la bajeti na kuweka kambi Jimboni kufanya kampeni .

Ridhiwan Kikwete amekosa uungwaji mkono kutokana na utendaji wake dhaifu na kushindwa kutelekeza ahadi alizotoa kwa wananchi wakati anachaguliwa mwaka 2015 . Utekelezaji wa ahadi zake ni sawa na asilimia 0.00000 , wakati anachaguliwa alitoa ahadi kumi zilizowavutia wananchi wakiamini huyu ni mtoto wa Rais hakuna kinachoshindikana , ahadi hizo ni ;
1. Kuifanya Chalinze kuwa Dubai
2. Kujenga soko la kimataifa
3. Kujenga stendi ya kisasa
4. Kugawa trekta moja kila kijiji
5. Kujenga uwanja wa mpira wa kisasa
6. Kutoa Ambulance moja kila kata
7. Kuwawezesha vijana wa bodaboda
8. Kuwawezesha wanawake
9. Kuwapa studio ya kisasa wasanii
10. Tatizo la maji kuwa historia

Mbunge huyo kwa Sasa ameacha vikao vya bunge na kujichimbia kuzunguka Jimboni kukutana na wajumbe wa mkutano mkuu akiwafuata na kufanya vikao , amenukuliwa akiwaomba msamaha ili aungwe mkono tena wakati wa kura za maoni . Kila anakopita wajumbe wamemhoji kwa ujasiri MWENZETU UMEKUJA KUAGA ? ULIKUWA WAPI MIAKA YOTE ? KWANINI HUPOKEI SIMU ZA WANANCHI ? OFISI YAKO IKO WAPI ?UMEFANYA NINI MIAKA MITANO ? KWANINI HAUKO BUNGENI NA BADALA YAKE UNAZURURA HUKU ?

Kwa hali ya kisiasa ilivyo Ridhiwan Kikwete hawezi kutetea nafasi yake kwakuwa hakuna alichokifanya , alitelekeza Jimbo kwa muda mrefu , pia anaponzwa kwa dharau na kiburi chake .

WANAOMNYIMA USINGIZI

kwa mujibu wa duru za siasa za Chalinze Kuna watia nia wawili wanaomfanya Ridhiwan Kikwete akose usingizi na kuhaha kama faru aliyejeruhiwa , watia nia hao ni pamoja na ;

1. SAIDI ZIKATIMU, huyu ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze anayetajwa kufanya kazi nzuri ya kusimamia Halmashauri kukusanya mapato ya kutosha na kutelekeza miradi mingi ya maendeleo kwa kutumia mapato ya ndani ikiwemo sekta ya Elimu , Afya na kutoa mikopo kwa wanawake na vijana .

ZIKATIMU anatajwa kufanya kazi nzuri mithili ya mbunge ikiwemo kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua na amekuwa kimbilio la wananchi wengi hivyo kuonekana anafaa kuinuliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Chalinze ili aweze kuwatumikia wananchi.

2. RAMADHANI MANENO ; huyu ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani na mbunge wa zamani wa Jimbo la Chalinze 2005-2010 . Maneno anatajwa kutia nia kugombea Ubunge kurejea kwenye kiti chake baada ya miaka kumi aliposhindwa kwenye uchaguzi wa kura za maoni ndani ya chama mwaka 2010 .

Jimbo limewaka moto !!!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chalinze ilikua na mama mbunge, mtoto mbunge na baba rais matatizo hayakuisha leo ndio yaje yaishe?

Ccm hata wakipewa hii nchi miaka 500 hakuna kitu watakachofanya cha maana kikaonekana.

Tuendelee kufanya uchaguzi kwa mazoea tu ila kitu kinaitwa maendeleo ni ndoto za alinacha.
 
Ridhiwani bado mdogo, ana elimu na amepata uzoefu wa uwongozi kupitia Bunge CZV imetulia. Akikosa ubunge ana options nyingine.

Riziki mafungu saba.
Sio rahisi kihivyo. Baba yake sio Rais tena, akikosa na ubunge atabaki na nini? Ni mwanasheria lakini sijui kama amewahi kuingia hata mahakama ya mwanzo kutetea mwizi wa kuku. Biashara zenyewe wakati huu ni changamoto, tena bila msaada wa cheo chake na cha baba yake, atapata tabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio rahisi kihivyo. Baba yake sio Rais tena, akikosa na ubunge atabaki na nini? Ni mwanasheria lakini sijui kama amewahi kuingia hata mahakama ya mwanzo kutetea mwizi wa kuku. Biashara zenyewe wakati huu ni changamoto, tena bila msaada wa cheo chake na cha baba yake, atapata tabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
hahaha dah

Hivi unamjua ridhiwan kweli wewe

Mkulima wa mahindi
 
Huwez jua labda baba yake alipo kua anamaliza alimkabidhi. Kwa Magufuli ili amsaidie kutimiza alio ahid siunajua CCM ilio kua ya wazee wetu hakuna linalo shindikana Ila mwamba Magufuli atakua kapangulia gia angani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom