Hali ya kisiasa ilivyo sasa hivi, CCM Vs Upinzani ni kama Yanga SC Vs Simba SC! Wabunge kama wachezaji

Chimo

JF-Expert Member
Aug 31, 2008
714
360
Inasikitisha kuona hali ya kisiasa inavyoendelea ni kama Vyama Vikuu vya Kisiasa Nchini vimegeuka kama vilabu vikubwa vya soka Nchini.
Naamanisha Simba, Yanga na Wakati Mwingine Azam. Ushindani wao wa kuibuwa Wabunge kutoka Upande moja kwenda kwingine hakuna tofauti na Niyonzima kwenda Simba na Ajib kwenda Yanga.

Angalia Ilivyoaanza Madiwani wa Arumeru kisha Kujivua Ubunge Nyarandu Halafu Mara Paaaaaaa Leo Mtulia Naona Kama Siasa za Soka zinakuja kwenye Vyama vinavyopaswa kuwa Seriously na issue za Maisha ya Kila Siku ya Mtanzania huku vikijitengenezea Heshima ya kuwa Taasisi Kubwa zenye Dhamana ya kuongoza Watanzania Kuliko kuanza Kuingia kwenye Ulinge wa Kutumia Mlungula kama Vilabu vya soka vinapoaanza kukusanya Saini za Wachezaji kwa mtindo huo vyama na vyenyewe Kumbe vina Dirisha Dogo?Vinasajili Wabunge na Madiwani?
 
Chimo,
Uongozi wa kipuuzi badala ya serikali kupambana kuondoa changamoto na kero za wananchi wamekazana kupoteza mabilion kujijenga kisiasa halafu wako bize kupambana na upinzani utadhan ndicho tulicho wapelekea ikulu,

halafu eti mmoja kanywa gongo zake huko anakuja kuniambia serikali ya CCM inania ya dhat kutatua kero za wananchi wakati kutwa kucha wako bize kutafuta wanachama wa kuwanunua kutoka upinzani

Nadhan hii ndio itakuwa serikali ya kwanza na polepole akiwemo kuongoza kwa kuingiza wanachama wapya na wazaman kurudi kuliko kutatua kero za wananchi wake ,
 
Kkimondoa,
Sasa kama waliokuwa wanazungumzia mabadiliko hawaishi mabadiliko hayo unategemea nini. Tujifunze kusimama katika misimamo tunayoamini imetukuka kwa ajili ya sustainability. The moment gear ilipobadilishiwa angani, ndiyo maangamizi yalipotokea. Hivi sasa tunaona tu matokeo.
 
Na Nyalandu alivyohamia CDM pia mlimnunua?
Mm naamin Nyalandu kahamia CDM kwa kaz maalum. Inawezekana katk haya mawili moja likawa ni lengo

1/ Ili kuhalalisha upumbavu wa ccm kununua madiwani ionekane hata upande wa ccm wanahama kuja upinzan kwahyo hilo ni kawaida.

2/ Kuja kuchunguza maswala nyeti ya CDM na kuyafichua kwa ccm.

Siamin kama Nyalandu kahama kwa moyo mmoja
 
Tulipofika sasa ni hatua kubwa ya demokrasia..watu sasa wanaangalia Sera!! Ukiona chama X kina sera za kipuuzi, unahama! No strings attached
Fanya utafiti kidogo wote waliohamia CCM ni kwa maslahi binafsi. Waulize Arusha juu ya Msando
 
Sasa kama waliokuwa wanazungumzia mabadiliko hawaishi mabadiliko hayo unategemea nini. Tujifunze kusimama katika misimamo tunayoamini imetukuka kwa ajili ya sustainability. The moment gear ilipobadilishiwa angani, ndiyo maangamizi yalipotokea. Hivi sasa tunaona tu matokeo.
Hata gia ingebadilishiwa ardhini hakuna mbinu za kuishinda ccm.
Ni nyie mnaotumia mitandao na kuyaelewa baadhi ya mambo na hasa mliopo mijini ndo mnaweza kuchagua upinzani.
Mnasahau kuwa tanzania ni pana na ina vijiji vingi na wanakijiji ni wapiga kura wazuri sana nao hawajafikiwa ipasavyo na upinzani.
Huku kwetu simiyu,bariadi-ikungulyabashashi ukiwa mpinzani unafukuzwa kijijin maana unapotosha watu na hatutumii kompyuta wala smart phn na wachache tunaotumia tunauogopa upinzani maana hawakawii kununuliwa isije wakatuuza nasi.
 
Mm naamin Nyalandu kahamia CDM kwa kaz maalum. Inawezekana katk haya mawili moja likawa ni lengo

1/ Ili kuhalalisha upumbavu wa ccm kununua madiwani ionekane hata upande wa ccm wanahama kuja upinzan kwahyo hilo ni kawaida.

2/ Kuja kuchunguza maswala nyeti ya CDM na kuyafichua kwa ccm.

Siamin kama Nyalandu kahama kwa moyo mmoja
Vipi kuhusu mh. saaaaaana rais wa mioyo ya watu Eddo naye pia alinunuliwa na CHADEMA au yuko nyumba hiyo kwa SPECIAL TASK akitumwa na CCM?
 
Back
Top Bottom