Hali ya kiafya ya mama mzazi wa mbunge Chiku Abwao si nzuri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali ya kiafya ya mama mzazi wa mbunge Chiku Abwao si nzuri

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Francis Godwin, Jun 30, 2011.

 1. Francis Godwin

  Francis Godwin Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=3][/h]
  [​IMG]Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Mhe.Chiku Abwao akimuuguza mama yake mzazi Tatu Abdallahman (79) ambaye amerejeshwa hospitali na kutibiwa nyumbani kwake Gangilonga mjini Iringa mgonjwa huyo anasumbuliwa na matatizo ya mshtuko wa moyo na kupelekea kupooza mguu wa kushoto na mkono hali iliyomlazimu mbunge Abwao kusitisha kuhudhuria kikao cha bunge Dodoma na kurudi kuuuguza mzazi wake huyo[​IMG]MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha Demokrasi na maendeleo (CHADEMA) Chiku Abwao amelazimika kuomba ruhusa bungeni na kurudi nyumbani Iringa kumuuguza mama yake mzazi Tatu Abdallahman (79) ambaye hali yake kiafya ni mbaya zaidi.

  Akizungumza na mtandao huu leo nyumbani kwa mbunge huyo eneo la Gangilonga ambako kwa sasa mama yake yupo baada ya kutolewa Hospital ,Abwao alisema hali ya mgonjwa wake si nzuri sana hali ilkiyomlazimu kurudi kutoka bungeni na kuja kumuuguza .

  Alisema kuwa mama yake ambaye wiki moja kabla alikuwa amezidiwa kupitia kiasi anasumbuliwa na tatizo la mshtuko wa moyo ambalo limepelekea kwa sasa baadhi ya viungo kupooza .

  Abwao alisema kuwa kabla ya kulazwa katika Hospital hali yake ilikuwa ni mbaya zaidi na kuwa kwa sasa hali yake japo imeendelea kuwa nzuri ila tayari amepooza mkono wa kushoto na mguu na kuwa amekuwa ni mtu wa kushinda amelala na akijitahidi sana amekuwa akiishia kukaa juu ya kitanda chake.

  Hata hivyo alisema kuwa hivi sasa daktari wake amekuwa akifika kumtibu nyumbani japo bado kupona kwake tatizo hilo anamtegemea zaidi mwenyezi Mungu.
   
 2. Jaxx

  Jaxx Senior Member

  #2
  Jun 30, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  What do you want to potray???!!!!, Jaribu jukwaa la afya
   
 3. p

  politiki JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Mungu awatie nguvu nyote mnaouguza na Mungu atawalipa. Mungu kwa majaliwa yake atamponya na kurudi tena kufanya kazi zake.
   
 4. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole mama abwao, Mungu akitie nguvu na mgonjwa apone
   
 5. KIMBURU

  KIMBURU JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 210
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  We kweli kilaza! siku nyingine uwe unajipanga kabla ya kucomment. Chiku ni mpiganaji mwenzetu so taarifa kama hii lazima iwepo hapa ili tumtie nguvu mwenzetu katika kipindi hiki kigumu.
   
 6. KIMBURU

  KIMBURU JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 210
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hypocrisy!!!!
   
 7. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pole sana mama,ila usivae tena nguo ya rangi za magamba.
   
Loading...