Hali ya hatari kwa maeneo ya vyuo vikuu vyote vilivyopo Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali ya hatari kwa maeneo ya vyuo vikuu vyote vilivyopo Dodoma

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Kidoma, May 30, 2012.

 1. K

  Kidoma Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kumetokea hali ya ukosefu wa amani katika maeneo yote yanayozunguka vyuo vikuu vya mkoa wa Dodoma. Matokeo hayo yanahususha matukio ya ujambazi, ubakaji, uvamizi, uporaji na mengi yanayofanana na hayo. ninaporipoti taarifa nipo chuo cha St John's ambapo wanachuo pamoja na mkuu wa polisi wailaya ya Dodoma mjini ambaye amejitambulisha kuwa anahamia Katavi na tayari ameambatana na yule atakayechukua nafasi yake.
  wananchuo wanaanza kutoa madukuduku na matukio ambayo yamekuwa yakiwapata!

  [​IMG] By msoroka [​IMG]
  Hebu visit Ranking Web of World universities: Top Africa ili kuona rank za vyuo vikuu bora 100 katika Africa pamoja na ranks zake katika dunia. Pia visit Top Colleges & Universities in Tanzania | 2012 University Web Rankings ili kuona vyuo vikuu bora katika Tanzania.  kwa kweli great thinker wa leo mmeniudhi, awali niliona niwaache kwa style ya kuhama kwenu mada but itz useless. qoute hapo juu inatosha kumaliza mada ya listing za vyuo vikuu na ubora wake with reference kwa vyuo vya Tz, ni kweli vyuo vyetu vingi ubora wake uko chini, kuna vyuo vinavyojidhani ni vya kitaifa, kimkoa na vya kata. kuna vyuo vina miundo mbinu dhaifu na vingine vya wastani; hata hivyo miundombinu cyo kigezo kikuu cha utowaji wa kiwango cha elimu, say chuo no.2 tz ni cha kiwango cha chuo cha kata kama kilivyo hiki kinachojadiliwa!

  sasa turudi kwenye mada, uporaji umekithiri vyuo vya Dodoma, case study ni SJUT, wanafunzi wengi wanaishi hosteli binafsi zinazozungukwa na chuo; huko wanavamiwa usiku wa kuanzia saa 4 wanapotoka kusoma mpaka saa 11 alfajiri vibaka wanafanya wanavyotaka!

  matukio zaidi ya 10 yameripotiwa polisi wilaya, hakuna juhudi zozote zilizochukuliwa na hivyo wameamua kuacha kuripoti maana hakuna maana ya kwenda polisi. matukio ya kuanzia ijumaa ya wk jana, nyumba ina geti na drill vibaka walivamia chumba cha wasichana 2 wakaiba laptop2, simu5, pesa, modem2, flash nguo za thaman nakila ki2 kidogo cha thamani walichoona na kisha kufanya ubakaji!

  pamoja na kuripotiwa polisi, kesho walifanya doria mpaka saa 4 na baaday ya hapo vibaka wakavamia wa2 wengine chumba cha hostel jiran wakaiba laptop 3, pamoja na nguo wakawafunga kamba wasichana 2 na mmoja wakawa tayari kumbaka attempt ikashindikana maana alikimbia na wakamkimbiza kama mwizi but wa2 wakaamka kumuokoa, hata hivyo walishindwa kuiba sehemu nyinginezo jirani japo na zingine walikua tayari wameshachukua vitu vidogo!

  jana walivamia hostel ya wasichana chumba kwa chumba wakawaibia kila kitu pamoja na nguo, wakavamia nyumba nyingine wakabaka wasichan baaadaya kuwaibia vtu vyao vyote na kuwaacha uchi.

  orodha ni ndefu mno. kinachoudhi, polisi hawaonyeshi kuguswa na tatizo hili na yamkini uongozi wilaya unahusika na matukio haya kwa sababu:

  • pamoja na kutolea taarifa na kufunguliwa majalada na kupeleka majina ya wahusika na wanaoshukiwa hakuna hatua zilizochukuliwa
  • katika karibu kila tukio polisi wamepigiwa simu hawafiki eneo la tukio. mfano tukio la ijumaa polisi walipigiwa simu mara 18 bila kupokelewa, ikapigwa simu dar na kisha RPC dar akapata taarifa akampigia cm RPC Dom ndo asubuhi polisi wakafika kwenye tukio
  • tukio la juzi OCD alipigiwa cm namajibu yake yalichefua; anauliza kwa nini msimkamate huyo mwizi, lindeni wenyewe, tuko kwenye doria maeneo hayohayo msiwe na wasiwasi na majibu ya kisiasa ya namna hiyo
  • matukio mengi akipigiwa OCD no action mpaka apigiwe RPC ndo atleast baada ya muda polisi watafika

  wanajamii. matukio nimengi na action ndo hizi! huu ndo mjadala, kama una ndugu kwenye vyuo hivi mnavyoviita vya kata hii ndo hali halisi

  TUJADILI HILO!
   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Kuna chuo kikuu kinaitwa St. John hapa tanzania?

  Kweli elimu imeshuka kiwango, vyuo vikuu kama uyoga? na mkimaliza mnakuwa na degree? Inatambulika pia?

  Hii ni hatari sana kwa ustawi wa taifa!
   
 3. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  T
  ww bwana unamatatizo gani mbona unafuatilia sn mambo ya tanganyika?,komaa na visiwani kwenu.
   
 4. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kwahiyo kama wewe hujakisikia hiko chuo ndio ni cha kiwango cha chini?

  Ni kitu gani kinakufanya ufikirie kuwa Tanzania kuna vyuo vikuu vingi? Nenda ukahesabu Kenya na Uganda halafu ulinganishe na population size
   
 5. Dangire

  Dangire JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  inaonekana bado unaishi enzi za nyerere! Kwani unataka tubaki na chuo cha udsm pekee?
   
 6. Ben Mugashe

  Ben Mugashe Verified User

  #6
  May 30, 2012
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 939
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Mkuu Hii ndo ilikuwa Mazengo High School, ama kwa wakongwe kama mimi tuliita Mazengo Complex..Iko Iringa Road Dodoma..:ranger:
   
 7. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #7
  May 30, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Hivi hiko zenji kuna chuo kikuu?
   
 8. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Wakuu mbona mna jazba, mi nilitaka kujua maana nijuavyo mie vyuo vikuu tanzania ni UD,SUA,MZUMBE na UDOM. ukisoam huko ndio unapata degree zinazotambulika,

  Vlivyobaki ni vyeti na diploma.

  Pia ukilinganisha na idadi ya wanaopata div 1 na 2 kimsingi wote wanaishia UDSM na wachache kwenye hivyo nilivyoviaja hapo juu, sasa najiuliza hivi vyuo vingine wanapata wapi wanafunzi wenye sifa?

  Mkuu elimu inachakachuliwa sana
   
 9. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #9
  May 30, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Acha ubaguzi
   
 10. Omonto wa-hene

  Omonto wa-hene Senior Member

  #10
  May 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 179
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Tume ya Katiba anaweza kuwa ana hoja nzuri. Tuchambue hoja yake na tuisahihishe kwa hoja. Siyo kumshambulia yeye binafsi. Tukimshambulia tutazidi kuthibitisha wasiwasi wake kwamba ninyi msomao huko huenda ni vodafsta, no ku-argue!
   
 11. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Watu wengine inaonekana sijui mnaishi dunia gani! Yaani wewe vyuo vikuu kwako ni hivi vya serikali tu???Mbona serikali ilisharuhusu vyuo vikuu vya binafsi chungu nzima na vimesajiliwa rasmi na Tume ya Vyuo Vikuu(TCU)nchi nzima? Nendeni TCU mkapate orodha kamili ya vyuo vikuu vilivyosajiliwa na vinapewa fedha ya mikopo na Bodi ya Mikopo kama kawaida.

  Hivyo acheni kupotosha umma.
   
 12. F

  FJM JF-Expert Member

  #12
  May 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Utajuje wakati unakesha kwenye mihadhara?
   
 13. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #13
  May 30, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Tume ya katiba bwana ana mambo!! Vyuo viko vingi mkuu hata kuvihesabu huwezi. Juzi nilikuwa Tanga nikakutana na chuo kikuu kinaitwa Eckenford! Nikapita Bagamoyo nikakutana na Bagamoyo University sijakaa sawa nikaenda huko Mbeya nao wana vya kwao kimoja kinaitwa sijui askofu nani University!! Bukoba tuna cha kwetu kwa kweri chinaitwa Bukoba University. Vyuo lukuki kila mtu ana degree mkuu! kazi kwako
   
 14. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #14
  May 30, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Mkuu nini maana ya mihadhara? una maana lecture?
   
 15. t

  tony25 Member

  #15
  May 30, 2012
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 52
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Siku hizi hamna shida, division III mbona university unatinga kama kawaida. Enzi zetu ukiwa na III ujue tu ni Diploma ya Ualimu Marangu na vyuo vingine tena unaona umepata bonge la course.
   
 16. C

  CANCER Member

  #16
  May 30, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Wewe ni mbuzi kama unasoma chuo mpaka karne hii unaamini watu wanaosoma chuo ni UDSM , UDOM ,MZUMBE NA SUA TU .Hivi husomi mwongozo wa TCU kujua vyuo vilivyopo Kwa taarifa yako kuna vyuo vinadahili wanafunzi kwa passmark za juu kuliko hivyo ulivyotaja Vyuo kama MUHAS(Muhimbili) , ardhi ,BUGANDO ,KCMC ST AUGUSTIN ,IFM Kwako sio vyuo andika mtu uliyenda shule sio kukurupuka hivi wewe ni TCU unayejua ubora wa elimu ya vyuo .hivi kama vyuo ni hivyo ulivyotaja chuo cha ubora kutokana tathimini ya 2011 ni kipi kama sio MUHAS.USIPENDE KUTUKUZA CHAKO NA KUONA WENGINE WAMEPOTEA WEWE NA PAMOJA NA KUSOMA CHUO UNACHOONA BORA NI MZEE WA MADESA.
   
 17. N

  Ntu JF-Expert Member

  #17
  May 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 564
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 60
  Mkuu nakuunga mkono! Kuna jamaa nlikua nae hapa Chalinze km miaka 4 hivi imepita, kapata kazi kwenye hicho chuo, alikua ni F4 ya div 4, leo hii kaniambia anamalizia bachelor degree hapo SJUT??? Not even f6 or diploma holder???? Alafu mnatuambia kuna TCU na Quality assurance....???? Shame upon you MAGAMBA Govt.....???
   
 18. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #18
  May 30, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  acha kuwa na ufinyu wa fikira: kinachoangaliwa sasa hivi ni FANI/COURSE inayoitajika na inayoweza kukupatia ajira katika soko la ajira na siyo chuo kitakachokufanya upate ajira:

  ziko COURSE muhimu sana zinazoitajika hapa nchini na ziko Hot cake lkn ukienda UDSM, SUA au MU huwezi kuzipata: we unafikiri ''Bachelor Degree in Industrial Relations'' unaweza kuipata wapi kati ya hivyo vikuu unavyosema ndo unavitambua??

  Acha kuwa na mawazo mgando bwana.
   
 19. m

  mmanga mswahili Member

  #19
  May 30, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Makanisa yanakuwezesheni kuwa na vyuo vikuu vingi ambavyo ni biashara tu wala hakuna kompitance huku bongo ila zanzibar heshima kwenu na elimu iko juu kwani wazanzibar hasa kutoka pemba munaongoza kla mnapokua katika elimu ya juu huku dar ni fijing na usanii mtupu
  hongereni zanzibar kwa kiwangop bora cha elimu.
   
 20. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #20
  May 30, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Pendekeza ungependelea kiitweje: Al shabaab University?, el halamain University?! Au?!. Rafiki, yaani wewe hujui kusoma, hata picha inakushinda kutambua?!. Hebu google "St. Johns University" uone acreditation yake ilivyo.
   
Loading...