wanafunzi wahanga
New Member
- Feb 20, 2016
- 3
- 1
Barua ya wazi kwa mheshimiwa waziri wa elimu, sayansi, teknolojia na ufundi
YAH: HALI YA HATARI INAYOWAKABILI WANAFUNZI WATANZANIA WA
SHAHADA YA UZAMILI NCHINI ALGERIA
1. Shule imeanza mnamo mwezi wa tisa mwaka 2015 na mpaka sasa mwezi wa kwanza
mwaka 2016 wanafunzi hawa hawana pesa za kumudu gharama za kila siku za masomo
yao hali inayohatarisha mwendeleo wao kimasomo.
2. Ukosefu wa mkopo umetupelekea kukosa pesa za kujikimu kimaisha na
hivyo kuwepo katika hali ngumu ya kimaisha ugenini kwa kukosa pesa ya chakula, tiba na gharama za masomo.
3. Ukosefu wa pesa za kujikimu umetupelekea kuingia madeni yaliyokithiri
madukani na kwa wanafunzi wenzetu wa kigeni ili kukidhi mahitaji ya lazima ya kila siku
na hii imepelekea vitambulisho (passports) via baadhi yetu kushikiliwa na wadeni
wao kwa sababu ya kukosekana kwa uhakika wa ulipaji wa madeni hayo. Pia wadeni
wengine wamefikia hatua ya kutishia kuwafikisha wanafunzi wadaiwa kwenye vyombo
vya sheria.
4. Tumekata tamaa kimaisha na tunasumbuliwa na misongo ya mawazo
(Depressions), hali ambayo ni hatari kwa afya zetu za akili na maisha yetu kwani inaweza
tupelekea kupata magonjwa ya akili.
Mheshimiwa waziri tunaomba utusaidie kutatua tatizo hili ndani ya muda mfupi kadri iwezekanavyo ili kuzuia madhara yanayoweza kutufika kwani hali tuliyonayo inahatarisha maisha yetu.
NB: Sababu zetu za kuendelea na shahada ya uzamili ni ulazima uliowekwa na mabadiliko ya elimu haha nchini Algeria na wizara ya elimu ina taarifa na afisa wa bodi ya mikopo alipotembelea wizara ya elimu ya hapa nchini Algeria alielezwa na pia baadhi ya wakuu wa vyuo alioonana nao wamemueleza suala hilo.

Tafadhali rejea kichwa cha barua hapo juu. Wanafunzi wa kitanzania wa shahada ya
uzamili nchini Algeria tunakabiliwa na hali ya hatari kutokana na kutopata mkopo wa masomo
kwa mwaka wa masomo 2015/2016.
Hali hii ya hatari ni kutokana na sababu kuu zifuatazo:-