Hali ya fwedha Portsmouth ni ngumu. First 1X jana hawakulipwa mishahara! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali ya fwedha Portsmouth ni ngumu. First 1X jana hawakulipwa mishahara!

Discussion in 'Sports' started by Richard, Oct 1, 2009.

 1. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Wachezaji wote wa timu ya kwanza ya Portsmouth inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza jana hawakulipwa mishahara yao kama kawaida, jambo ambalo likezua utata mkubwa.

  Meneja mkuu wa timu hio Paul Hart asubuhi hii amekalishwa kikao na wachezaji wakidai majibu ya kwanini mishiko yao haijaingizwa kwenye akaunti zao jana.

  Timu hio ya Portsmouth yenye makazi yake katika mji wenye bandari ya Portsmouth kusini mwa Uingereza kwa sasa inamilikiwa na Sulaiman Al FahiM baada ya kufanikiwa kuinunua kutoka kwa mwekezaji mwingine Alexandre Gaydamak kwa kiasi cha paundi milioni 60.

  Sulaiman Al FahiM mwenye asili ya uarabuni aliinunua timu hiyo mwishoni mwa mwezi June mwaka huu huku akiahidi kuwekeza kiasi cha paundi milioni 50 na kuinyanyua kimapato timu hio na kuhakikisha kwamba timu hio inakwa na uwanja mpya na mkubwa kuaidia mapato kutoka ule wa Fratton Park.

  Lakini hadi sasa bwana Sulaiman Al FahiM ameshindwa kupata paundi milioni 2 ili kuweza kulipa mishahara hio na wachezaji hasa wale wageni wamechukizwa sana na mtindo huu.

  Haya hivyo taarifa za ndani ya timu hiyo zinasema kwamba wachezaji watalipwa ndani ya masaa 48 yajayo.

  Timu hiyo inachezewa na kipa wa Uingereza David James ambae ni mkongwe kwa sasa pia na nahodha wa timu ya taifa ya South Africa Aaron Makoena ambae ndie mkoba, mshambuliaji Nwanko Kanu ambae pia anazungumzia kuhamia Australia kucheza soka la kulipwa, Younes Kaboul ambae alitemwa na Tottenham, mchezaji mpya Tommy Smith ambae ametokea Watford na Aruna Dindane ambae ni kiungo wa timu ya taifa ya Ivory Coast.

  Wengine ni pamoja na Muisraeli Tal Ben Haim na Kevin-Prince Boateng ambae ni Mjerumani mwenye asili ya Ghana na mwenye uraia wa nchi mbili ambae ametokea timu ya Hertha Berlin ya Ujerumani.

  Timu ya Portsmouth katika msimu wa usajili mwaka huu ilikuwa ni timu iliokuwa "busy" sana kuuza wachezaji wake wakiwemo washabuliaji wawili Peter Crouch na Jermain Defoe ambao pamoja na mchezaji wa kiungo Nico Kranjcar walijiunga na timu ya Tottenham Hotspur ya Kaskazini Mashariki mwa London ambayo kocha wake Harry Redknapp aliwahi kuifundisha Portsmouth.

  Mchezaji mwingine ni Glen Johnson ambae ni beki wa kulia wa timu ya taia ya Uingereza ambae alinunuliwa na timu ya Liverpool kwa kiasi kisichopungua milioni 25.

  Mshahara kwa ujumla kwa wachezaji ni si chini ya paundi milioni 30 na mpaka sasa kunahitajika kiasi cha paundi milioni 75 ili kukidhi mahitaji yote ya mishahara na biashara zingine.
   
  Last edited: Oct 5, 2009
 2. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Mmiliki wa timu ya Portsmouth Sulaiman Al Fahim amefanyiwa upasuaji wa figo siku ya Ijumaa na hali yake inaendelea uzuri.

  Mwekezaji huyo amefanyiwa upasuaji kwenye hospitali moja mjini Dubai.

  Kumekuwa na hali ya wasiwasi kwa wapenzi wa timu hio tangu mmiliki huyo mpya aitwae timu hio kwa kiasi cha paundi milioni 60 kutoka kwa mwekezaji aliekuwepo bwana Alexandre Gaydamak.

  Na habari za mwishoni mwa wiki zimezagaa kwamba huenda mfanyabiashara huyo akaiuza timu hio kwa mwekezaji mwingine wa kutoka hukohuko Dubai bwana Ali Al Faraj.

  Mpaka sasa timu ya Portsmouth inashikilia mkia katika ligi kuu ya Uingereza ikiwa na pointi 3 ambazo imezipata kwa kuifunga timu ya Wolverhampton siku ya Jumamosi.
   
  Last edited: Oct 5, 2009
 3. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Mwekezaji mwingine kutoka Saudi Arabia bwana Ali Al Faraj huenda akaitwaa timu hio na kuwa mwenyekiti mtendaji baada ya kufanya mazungumzo na mwekezaji mwingine Sulaiman Al Fahim leo mchana.

  Kwenye duru la wanamichezo nchini Uingereza inaaminika kwamba bwana Al Fahim atakubali kumuuzia bwana Al Faraj karibu asilimia tisini ya mrahaba wa mapato ya uendeshaji wa timu hiyo na pia kuondolewa katika bodi ya timu hiyo.

  Bwana Al Faraj alikwenda mjini London kukutana na maofisa wa ligi kuu ya Uingereza kwa ajili ya kutathminiwa uwezo wake wa kumiliki timu.

  Pia inaaminika kuwa bwana Al Faraj ametoa kitita cha paundi milioni 5 ili kusaidia kulipa mishahara ya wachezaji ambao mpaka sasa bado hawajalipwa chochote.

  Timu ya Portsmouth inatarajiwa kutoa maelezo ya mkutano uliofanyika leo baina ya wafanyabiashara hao wakati wowote usiku huu.
   
Loading...