Hali ya chakula Tanzania imekuwa mbaya sana

girgirmo

Member
Jan 11, 2017
44
32
Nimetembelea kijiji moja wilaya ya Hanang jamii ya wafugaji wana hali mbaya sana ya chakula.

Mmoja kati yao anasema nilipeleka mfugo wake mnadani hawauziki imebidi aishi kwa kunywa uji na kula mbogamboga zinazouzwa mtaani. Wengine wanasema kuwa wapo wenye fedha lakini mahindi hayapatikani.

Uncle wetu ukimwambia kuna njaa anagomba sasa watz tufanyaje. Viongozi wetu wakuu wa wilaya ukimwambia hali ya njaa vijijini watakuua. Jamani ukitaka kujua njaa ipo kijijini.

Mjini mtu anaweza kununua mchele, unga kilokilo, makaroni. siku zinasogea . sasa huku wenzangu wanaishi na maziwa na nyama.

Kama kuna mtu anaghala la mahindi aje awauzie huku watu wanapesa lakini wanakosa mahindi yakununua!
 
jamani jamii inajionyesha.watu wantembea na punda kuhemea chakula watu sasa watawakimbia watoto wao
 
mkulu anaishi ikulu yeye akihitaji chakula cha kwake wewe masikini unamnunulia.
 
Nani awaletee mahindi? Njoo arusha uone, mahindi yanasombwa na malori kwenda kenya ,Sudan kusini na somalia. Walio na mahindi wameyaficha ili njaa ikiwa kubwa wauze kwa sh laki mbili kwa gunia
 
jamani nimetembelea kijiji moja wilaya ya Hanang jamii ya wafugaji wanahali mbaya sana ya chakula. mmoja kati yao anasema nilipeleka mfugo wake mnadani hawauziki imebidi aishi kwa kunywa uji na kula mbogamboga zinazouzwa mtaani.wengine wanasema kuwa wapo wenye fedha lakini mahindi hayapatikani. uncle wetu ukimwambia kuna njaa anagomba sasa watz tufanyaje. viongozi wetu wakuu wa wilaya ukimwambia hali ya njaa vijijin watakuua. jamani ukitaka kujua njaa ipo kijijini. mjini mtu anaweza kununua mchele, unga kilokilo, makaroni. siku zinasogea . sasa huku wenzangu wanaishi na maziwa na nyama.kama kuna mtu anaghala la mahindi aje awauzie huku watu wanapesa lakini wanakosa mahindi yakununua!!!
kijiji kimoja tu ndio imekuwa Tanzania yote? Tanzania hakuna njaa ,kwetu the big 4 hatuna soko la kuuza mahindi.Mahindi yamejaa kila store
 
Hao hao ndo wanasema ccm imewazaa ngoja iwanyooshe! Kipnd hiki mpaka wajue kuwa walizaliwa na baba na mama zao na sio ccm!
 
Back
Top Bottom