Hali ya barabara kona za Iyovi inatishia usalama barabarani

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,532
I wonder hata kama kuna agency ya kusimamia barabara kama inaiona hatari kwenye hizi kona za Iyovi.

Kwani eti nyie TANROADS kufyeka nyasi shilingi ngapi hasa.

Nimekutana na Malori matatu yamemwaga kwenye hizi kona na possibility ya magari kugongana ni kubwa mno.

Safisheni hicho kipande. Kina hatari sana na majani marefu kwenye kona na ni kipande kirefu tu.

Hapo bado sijazungumzia matobo mengi mno yaliyomo kwenye kipande cha ndani ya hifadhi Mikumi.

Sitaki kuamini kwamba kuna kikwazo chochote kurekebisha hivi vipande vya barabara vinagharimu maisha ya watu.

Hapo Iyovi nyasi zimeota kiasi kwamba hata watembea kwa miguu hawana mahala pa kutembelea au kujitetea gari linapokuja.

Mwaka jana nilipita hapo mtoto mwanafunzi akawa kagongwa eneo hilo la Iyovi wenyeji wanasema inaonekana semi upepo ulimvuta maana alijitetea akiwa jirani sana na barabara sababu ya manyasi. Kalikuwa katoto kadogo.

Nasikitika kuona kwamba kila mwaka msimu wa mvua hamtoi haya majani kwa wakati.

TANROADS eeh hili ni jambo dogo sana. You can do it. Muwe mnatoa hizo nyasi Iyovi kwa wakati zinasababisha ajali sana.

INAUDHI!

I'm the witness.

IMG-20200418-WA0001.jpg
IMG-20200418-WA0002.jpg
IMG-20200418-WA0003.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku Iringa ofisi za TANROADS zipo njia ya Dodoma mbele ya uwanja wa ndege, nje ya ofisi zao barabarani kuna mashimo unaweza kupanda hadi migomba na ikastawi vizuri tu lakini ofisi zina management na wanapatazama tu, Hadi ajali itokee pale ndio watajifanya wanarekebisha, mimi huwaga sielewi utashi wao unatumika kufanya nini aiseee!
 
Huku Iringa ofisi za TANROADS zipo njia ya Dodoma mbele ya uwanja wa ndege, nje ya ofisi zao barabarani kuna mashimo unaweza kupanda hadi migomba na ikastawi vizuri tu lakini ofisi zina management na wanapatazama tu, Hadi ajali itokee pale ndio watajifanya wanarekebisha, mimi huwaga sielewi utashi wao unatumika kufanya nini aiseee!
Lubede yaani wanaudhi kinoma...yaani nimenusurika kugongana uso na uso hapo Iyovi jamaa wa basi anaovateki kona sio kali sana ila sababu ya manyasi alikuwa haonekani wakati anakuja...ikabidi nikimbilie pembeni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu watatoa siku JPM akiwaambia..taasisi za serikali ni uozo,kila kitu mpaka Rais atoe tamko,sijui huwa wanaajiriwa kwa vigezo gani..smh!
Wanatuna matumbo tu ofisini sasa hata kuziba viraka nalo jambo kubwa kiasi gani....bado nawakumbuka waliopoteza maisha Majinja bus Mafinga sababu ya tobo kwenye lami ya hawa jamaa. Nawamaindi kinoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom