Hali tete mtaani. Baa zazidi kufungwa kwa kukosa wateja!

Rais mwenyewe akisikia au kuona hivyo ndi anashangilia na kucheka, bila kujua bajeti yake inategemea hizo pombe baada ya bandari kukimbiwa na vijana wake wengi wanaajiriwa kuwa mabaamedi na wakaanga chipsi, wachoma nyama wakishapata divisheni 4 na digrii uchwara kwenye mashule na mavyuo yao yasiyo na viwango....huo ndio upeo wa rais wetu na watanzania anaowaongoza
Hujui unachosema. Kodi sasa inakusanywa kwenye biashara zote na siyo pombe na sigara tu. Pia wanywaji wengi wa pombe walikuwa watumishi wa umma ambao wamenyimwa posho bandia na matumizi ya serikali yamepungua. Bandarini pia mizigo mingi ilikuwa ya mafisadi wasioilipia ushuru na kodi ndiyo maana mapato ya TRA hayajaathirika. Wenye kiu wanywe maji yana afya zaidi.
 
Siwalisema watakuwa wanakama na wateja biashara lazima idorore.
 
Hali tete unaongea kuhusu Bar? Bar ndio chanzo kikuu cha maisha ya ovyo kwenye jamii zetu, ikiwezekana zifungwe zote hata viwanda vigeuzwe karakana. Nchi haiwezi kujisifia kwa kipato cha Pombe, wakati athari ya pombe ni kubwa zaidi kuliko faida.
 
Hujui unachosema. Kodi sasa inakusanywa kwenye biashara zote na siyo pombe na sigara tu. Pia wanywaji wengi wa pombe walikuwa watumishi wa umma ambao wamenyimwa posho bandia na matumizi ya serikali yamepungua. Bandarini pia mizigo mingi ilikuwa ya mafisadi wasioilipia ushuru na kodi ndiyo maana mapato ya TRA hayajaathirika. Wenye kiu wanywe maji yana afya zaidi.
Mapato ya TRA hayajaathirika? Wewe nae bhana, mwambie uliemwazima akili akurudishie!
 
Walevi utawajua tuu.
Sasa hauoni kama ni neema hiyo,watu muache kufanya kazi mkalie ulevi tuuuu
Wenye hela wanaendelea na starehe zao,we unalewa halafu kesho unasema maisha magum
 
Kuna athari kubwa kiuchumi na mzunguko wa pesa
Mkuu nimekusoma lakini kote duniani ni kawaida serikali mpya inapoingia madarakani,mzunguuko wa pesa unakuwa mgumu,sema kwa sababu nchi ilibatizwa siasa kila kitu kisiasa!
 
pesa inapatikana kwa heshima ndo maana watu wanaogopa matumizi ya ajabu
 
Sio bar Tu hata Maduka mengi na biashara nyingine zimefungwa kwa kiasi kikubwa, cha kushangaza hadi wauzaji WA maduka ya vyakula kama mchele, sukari,mafuta ya kupikia nao wanalalamika biashara mbaya, na wengi wamefunga biashara
 
Hujui unachosema. Kodi sasa inakusanywa kwenye biashara zote na siyo pombe na sigara tu. Pia wanywaji wengi wa pombe walikuwa watumishi wa umma ambao wamenyimwa posho bandia na matumizi ya serikali yamepungua. Bandarini pia mizigo mingi ilikuwa ya mafisadi wasioilipia ushuru na kodi ndiyo maana mapato ya TRA hayajaathirika. Wenye kiu wanywe maji yana afya zaidi.
Mapato hayajaathirika? unaishi wapi mkuu? au unasikia hayo maneno ya wana siasa wanaojikanyaga kila siku unawaamini? kama unafahamu mtu anayefanya kazi TICTS au kwenye kampuni yoyote ya clearing au ICD au shipping line yotote mwambie akuelezee ukweli sio kusikia maneno ya majukwaani tu....

mwanzoni walisema mizigo imepungua kwa sababu ya uchumi wa dunia, wakaja wakasema tena tatizo ni uchumi wa china, wakarudi tena wakasema bandari ilikuwa ni uchochoro, wewe unawaamini watu kama hao? hujaona walivyojichanganya pia hata kwenye tozo ya VAT kwenye mihamala ya ma benk?
Na kwenye pombe kama ulikuwa hujui pombe inachangia sana kwenye kodi kama hujui fanya utafiti sio kusikiliza watu wa upande mmoja
 
Back
Top Bottom