Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 46,892
- 32,308
Wanabodi.
Kuingia kwa Abdulrahaman Kinana na Philip Mangula katika timu ya uongozi wa CCM, kunasafisha kabisa matumaini ya Chadema kuingia Ikulu ifikapo mwaka 2015. Ni jambo lililo wazi Kinana, heshima aliyojijengea mkoani Arusha na mikoa mingine ya kaskazini, kila Mtanzania mkweli anajua.
Heshima aliyojijengea Mangula Iringa na mikoa mingine ya Nyanda za Juu Kusini, kila Mtanzania mkweli anajua. Kutokana na sababu hizo kiongozi au mwanasiasa yeyote makini ndani ya Chadema, atakubaliana na ukweli kwamba chama hicho sasa hakitakuwa na chake tena kanda ya kaskazini na nyanda za juu kusini mwaka 2015.
Chadema kama ina viongozi wanaona mbali wanaweza wakaanza kuitumia ruzuku wanaoipata sasa kwa umakini wa hali ya juu, ikiwa ni pamoja na ruzuku hiyo kutumika kujenga vitega uchumi vya baadae vya chama hicho baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, cha hicho hakitapata tena ruzuku. Hakuna kipindi kigumu ambacho Chadema itapitia kama kipindi hicho kwenye historia ya chama hicho.
Pamoja na kwamba hakuna kiongozi yeyote ndani ya Chadema anayeweza kwenda kinyume na amri ya Mbowe kuhusu matumizi ya ruzuku ya chama hicho, lakini mwelekeo wa sasa utakuwa tofauti, Chadema sasa wana hiyari ama kuacha hazina ya ruzuku yao kidogo kutoka serikalini inayopatikana sasa iendelee kuboresha maisha ya viongozi na familia zao, au waseme hapana, sasa tuanze kujenga ofisi za chama chetu kila mkoa na wilaya ili pindi ruzuku hiyo itakapopungua baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 walau chama kibakiwe na ofisi.
Mbowe na Dr Slaa sidhani kama watakubali wazo hilo lenye maana moja ya kupunguza maisha yao kifahari waliyonayo sasa hawatakubali kuona wanaachana na mipango yao ya kujiwekea hazina ya baadaye ya maisha ndani ya chama ambayo haitakuwa na ruzuku.