Hali tete: BOT yashusha viwango vya uwekezaji wa Dhamana & Hati fungani kuanzia Februari 21,2018

Kutokana na kutofanya vizuri kwa mikopo ya biashara kwa benki za biashara kwa watu kutokukopesheka, mabenki yaliamua kuwekeza benki kuu kwa rate ya 13%-17% hadi kufikia tarehe 20/02/2018.

Kuanzia tarehe 21/02/2018 uwekezaji wa tresury bill (hati fungani) na bonds (dhamana) umeshuka hadi kufika kati ya 4%-6% hili ni anguko la kiuchumi ikimaanisha BoT hawana pa kuwekeza wala benki za biashara hana wa kuwekeza.

Tutarajie anguko kubwa la mabenki, SACCOS, Microfinance, hata hivyo vikoba maana biashara ya kumpa asiye nacho inakufa na aliyenacho hamwamini mkopaji maana hajui kama zitarudishwa.

=====

UPDATE

b7c24de051388742f04b25387fc0e6a9.jpg
Wewe ni mjinga na hujuwi uchumi... Waliokupa like 39% pia wajinga....
Kiufupi serikali sasa inapesa kiasi kwamba badala ya bank kuweka fedha bank kuu sasa wataenda kuzikopesha kwa wananchi.
Kiufupi kwa mtu mjanja hapa ndipo pakutokea maana automatical bank zitashusha interes nakufanya watu wakope kwa urahis. Kiufupi mpaka muda huu wafanyakaz mikopo wanapata mpaka 18% na uwenda ikashuka kutoka rate ya 22-26.... Mungu atupe nini? Ujinga upo wa aina nyingi
 
nijuavyo mimi ni kwamba riba ikishuka ni kwamba hali imekua tete huko mtaani na watu hawana hela ya kulipa riba za mikopo.hivyo ukopeshaji kwa kiwango kikubwa hushuka koz wakopaji huogopa kukopa na mwishowe wakose hela za kulipa.na pia wakopeshaji huhofia hela zao kupotea.na pili hawatopenda kukopesha kwa riba ndogo kwasababu hazitoweza kuwalipa gharama za kuendeshea mabenki..hivyo kiufupi tumerudi nyuma kiuchumi
 
Kichekesho hamna mtu ameongelea jinsi BOT na hizi private banks walivyoharibu uchumi kwa kutojikita kusaidia private sector badala yake walikuwa busy wanafanya biashara na serikali at the expense ya walipa kodi na pesa za misaada. Haitaji akili nyingi kujua Tanzania hatujawahi kuwa na uchumi wa kueleweka.
Sijui nyie mnaosimamia argument hii mna evidence gani kuthibitisha hili. Mabenki yanalia NPL, ni NPL kutoka kwa hizo private sector zinazoshindwa kurudisha kutokana na changed business environment. Performance ya uchumi ni productivity yake (How much we produce and how much we consume). Kweli, mzunguko wetu wa uchumi uliathiriwa sana na massive imports hivyo kusema tumekuwa tukifaidisha zaidi mataifa ya nje kuliko sisi wenyewe. Lakini badala ya kufanya intervention ya ku-discourage imports, tumeenda ku-discourage kila kitu katika uchumi ikiwemo ku-discourage uzalishaji wa ndani, matokeo yake both imports na economic activity za ndani zimekufa.

Financial sector ni more delicate kuliko sector nyingine za uchumi hivyo reforms katika eneo hilo zinahitaji umakini sana.

Kwa mfano katika hili kuna implications 3 zaweza tokea,

1. Tunatarajia benks hazitaenda kununua dhamana za Serikali na badala yake kufanya biashara na private sectors zaidi.
2. Domestic private sectors ima wataweka fedha benki binafsi (kama returns ni kubwa kuliko central bank) au wata invest kwenye mabenki ya nje ikiwa rate ni za juu kuliko za BOT(capital outflows; subject na country' degree of financial integration). Kwa msingi huu commercial banks zitakuwa na ukwasi lakini ukwasi huu hautakuwa na maana kama hakutakuwa wakopaji; kwa maana banks ni financial intermediaries.(collect money from those who have and lend them to those who need). So ni uamuzi mzuri subject na business environment iliyopo.

3. Hii haitarajiwa kupata foreign private capital inflows kwa kuwa hawa wanacheza sana na rate hizi za serikali (pia inategemea na degree of financial integration).

Lakini swali kubwa la kujiuliza ni je, rate (au money factors) ndio sababu pekee ya kudorora kwa economic activities au kuna elements za fiscal issues? If no, hii kitu haitakuwa na manufaa tarajiwa, na najiuliza which next weapon baada ya hii?

Naogopa huenda policy predictability ikawa na umuhimu wake hapa. Kama kuna elements za policy unpredictability na massive fiscal constraints and government over intervention katika nguvu za soko, investors hawataenda kukopa katika mabenki hata na hatimaye commercial banks zitayumba kwa sababu ile element ya intermediaries haitakuwepo kivile.

Nini kilitakiwa kifanyike ikiwa hali hii ipo?
Serikali ilipaswa kutumia zaidi fiscal policies na indirect subsidies katika sekta zenye returns za haraka na soko la uhakika nje ya nchi. Na policy hii ya serikali ilibidi itekelezwe kitambo kabla mazingira ya biashara hayajabadilika sana.
 
its true economically, Tz now moving backward!
Kiuchumi tz tunaenda kuzalisha maskini wengi zaidi mbeleni kuliko kipind cha mkapa, kikwete
Umaskini uliokidhiri husababsha watu kukataa tamaa kisiasa na maisha kwa ujumla
Uchumi wa kupikwa na jiko moja umepitwa na wakati

Ambao mtukufu anawapenda Na ndio watampigia kura. Acha azalishe wengi zaidi.
 
Mkuu joseverest Hati fungani au Bond(kwa kiingereza) ni utaratibu unaotumiwa na makampuni au serikali kukopa pesa kutoka kwa wananchi. Wale wanaonunua hizi hati wanakuwa wakopeshaji wa hiyo kampuni, kwa maana kwamba badala ya kampuni kukopa pesa benki, wanaweka utaratibu wa kuwawezesha wananchi kutoa pesa kwa makubaliano ya kuwarudishia hiyo pesa yao pamoja na riba kwa muda maalum.

Hati fungani inaweza ikatolewa na serikali kuu(Government bond), serikali za mitaa( Municipal bond), kampuni(corporate bond) au serikali ya nchi za nje(Euro bond).

Hati fungani utofautiana na hisa(share) kwa maana kwamba wenye hisa ndo wenye kampuni(debtors) kwa hiyo wao wanalipwa faida pale ambapo kampuni imepata faida na pesa yao hukatwa pale ambapo kampuni imepata hasara wakati wenye hati fungani ni wakopeshaji(creditors) kwa hiyo wao kulipwa faida haijalishi kampuni imepata hasara au la.
Tunashukuru kwa elimu yako umenifanya nielewe. Lakin wengine ni kujitapa tu wachumi hata shule hawatoi. Anyway tutawabana na ss kwenye kada zetu
Umeona eeh.
 
.....nikwambie tuu kitu kidogo kuwa hapo ni ahueni kwa wakopaji na mabenki maana viwango vya dhamana na hati fungani vimepungua.... Hivyo tunategemea mabenki yata himarika zaidi au kuanzishwa zaidi....

Kwa hiyo hizo pesa zingine zitakwenda kwa watu kwa njia ya mikopo.....
Sasa hapo hali tete inatoka wapi? benki itaanguka vipi wakati viwango vya dhamana na hati fungani vimeshushwa kuwasaidia? Vipi mwenzetu dish limeyumba?
Hii ni kicheko na furaha kwa mabenki na taasisi za kifedha....
Wakati mwingine kujitoa akili kunapitiliza kiasi kwamba hata anayekulipa anakuwa na wasiwasi kwa umekuwa chizi kweli!
 
Kutokana na kutofanya vizuri kwa mikopo ya biashara kwa benki za biashara kwa watu kutokukopesheka, mabenki yaliamua kuwekeza benki kuu kwa rate ya 13%-17% hadi kufikia tarehe 20/02/2018.

Kuanzia tarehe 21/02/2018 uwekezaji wa tresury bill (hati fungani) na bonds (dhamana) umeshuka hadi kufika kati ya 4%-6% hili ni anguko la kiuchumi ikimaanisha BoT hawana pa kuwekeza wala benki za biashara hana wa kuwekeza.

Tutarajie anguko kubwa la mabenki, SACCOS, Microfinance, hata hivyo vikoba maana biashara ya kumpa asiye nacho inakufa na aliyenacho hamwamini mkopaji maana hajui kama zitarudishwa.

=====

UPDATE

b7c24de051388742f04b25387fc0e6a9.jpg
Hali imekuaje tete Tumekuwa tukipiga kelele kwamba uchumi una dorola wamekuwa wakijinasibu Uchumi unakua kushinda nchi nyingi Africa
 
ATM zinazomilikiwa na UMOJA nyingi zimeanza kuondolewa mitaani. Je hili lina uhusiano wa mbali na hali hii
 
yaani BOT ilikuwa ikitoa riba ya 13- hadi 17% kwa benk za kibiashara zilizokuwa zikinunua T Bills zake, sasa hivi riba ndio imeshushwa hadi 4-6% sasa benki private zitakosa mapato kwa sababu watu mtaani hawakopesheki pia
Tutakopesheka tu washushe riba tu
 
Naomba kuelemishwa. Kama ulinunua Treasury bills na kuwekeana mkataba na Serikali kuwa interest rate ni 12%, Je leo wakishusha interest rate kuwa 4-6% Je utaathirika?.
 
.....nikwambie tuu kitu kidogo kuwa hapo ni ahueni kwa wakopaji na mabenki maana viwango vya dhamana na hati fungani vimepungua.... Hivyo tunategemea mabenki yata himarika zaidi au kuanzishwa zaidi....

Kwa hiyo hizo pesa zingine zitakwenda kwa watu kwa njia ya mikopo.....
Sasa hapo hali tete inatoka wapi? benki itaanguka vipi wakati viwango vya dhamana na hati fungani vimeshushwa kuwasaidia? Vipi mwenzetu dish limeyumba?
Hii ni kicheko na furaha kwa mabenki na taasisi za kifedha....
sasa mbona matawi madogomado ya bank tuliyoiamini kama crdb yanafungwa ndio kusema pesa sasa ndio zimeenda kwa wanaokopeshwa!?
 
.....nikwambie tuu kitu kidogo kuwa hapo ni ahueni kwa wakopaji na mabenki maana viwango vya dhamana na hati fungani vimepungua.... Hivyo tunategemea mabenki yata himarika zaidi au kuanzishwa zaidi....

Kwa hiyo hizo pesa zingine zitakwenda kwa watu kwa njia ya mikopo.....
Sasa hapo hali tete inatoka wapi? benki itaanguka vipi wakati viwango vya dhamana na hati fungani vimeshushwa kuwasaidia? Vipi mwenzetu dish limeyumba?
Hii ni kicheko na furaha kwa mabenki na taasisi za kifedha....

Mmmm! Yaani ilikuwa sio lazima uchangie!!
 
Bado naendelea kuwasoma, hayo maneno hati fungati et al hata siyaelewi vizuri, hivyo ni ngumu kupinga au kusifia, endeleeni kutoa shule hata sisi bush financial analysts tujifunze
 
Inaelekea huelewi biashara ya Treasury bills na Bonds ilivyo. Hapa hawazungumzii Repo rates!!

Serikali huwa inapata pesa za kujiendesha kwa kuuza hizo T/Bills au Bonds ....... kwa vile rate zimepunguzwa, Mabenki, na wenye pesa hawatakuwa attracted kuwekeza kwenye hizo rate ambazo ziko almost the same as the inflation rate ya sasa. Hakuna mwnye akili yake anayeweza kuweza long term (7 to 15 yrs) kwa rate ya 6 - 7 %!!

Kama T/Bills and Bond hazitauzika, basi serikali pia itapungukiwa pesa za kujiendesha!!
Fact
 
Back
Top Bottom