BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,792
- 287,994
Hahahahahahaha angemnasa na kibao kingine mpumbavu huyo.
Kuna kiongozi wa CCM kaniuzia shamba lake la ekari 30 kwa sh 6m baada ya kuhangaika kuuza kwa muda mrefu, na kutopata mteja.
Mimi sikuwa na haja ya shamba, akazidi kubembeleza kuwa nimsaidie ili angalao afanikishe kuwafanya watoto wake wawili waliopo chuoni wamalizie masomo.
Siku ya pili akiwa na viongozi wenzie wa CCM, akaja kijana mmoja aishie Dar, alipoona wamekaa viongozi wa CCM, akaanza kumsifie jiwe, wengi walimpinha lakini jamaa aliyeniuzia shamba ambaye ni Mwenyekiti wa kata alikaa kimya. Baadaye akasimama, alimlamba kofi kijana usoni kijana aliyekuwa anamsifia jiwe, kijana anguka kwa nyuma, akatoka anakimbia huku akianguka na kusimama maana yule Mwenyekiti wa kata siyo mtu wa mchezo. Ni giant hasa, na kiganja chake kimoja ni sawa na viganja vya watu wawili wa kawaida. Kisha akaanza kulalamika, 'huyu hana akili, mahindi yangu niliyotarajia kupata sh milioni 72, nimepata milipni nane wakati bank na watu wa pembejeo wananidai sh 18m. Halafu anakuja kuleta upumb.avu wa huyo mtu wake'.
Katibu mwenezi wake ameniuzia kiwanja kilichopimwa kwa sh 1.7m. Nimemlipa sh 1m. Hali ni mbaya kwa watu wengi. Na hawa wa CCM, mimi sina huruma nao. Akiwa na property, unaichukua ili jamaa atakapoondoka, wengi watakuwa wamesalia watupu kabisa.
Mjeda, naye kwa wiki zima amekuwa akinibembeleza sana. Kiwanja alichokinunua mika 6 iliyopita kwa sh 5.5m, kaniuzia kwa sh 2.1m huku akinikabidhi hati na karatasi alizokuwa amenunulia.
Wengime watatu, nimewakatalia.
Jamani, siyo utani - mambo ni magumu sana. Na inavyoonekana hali itazidi kuwa ngumu. Namshukuru Mungu mapato yangu siyo yategemeayo mapato ya hapa nyumbani, japo shughuli za hapa nyumbani zimeathirika sana.
Huku mtaani kama hali yako ni ya unafuu kidogo, utakuwa na bahati sana kama utamaliza wiki bila kupokea maombi mbalimbali toka kwa ndugu, makanisa, vikundi, mashuleni, marafiki na hata viongozi waliopo serikalini.