Hali si swari mkutano wa CHADEMA kata ya Ndago (Singida); watu 2 wafariki

Wewe mtu wa ajabu sana! Je kuna mwenye hakimiliki ya kuwa mbunge mpaka kufa? Ni dhambi gani Dr. Mkumbo kumpinga Mh. Mwiguru kwa hoja kupitia kipindi cha this week in perspective? Hembu oanisha kimantinki uwepo wa Dr.Mkumbo na vurugu zilizotokea, ukishindwa tutaamini wewe ni mmoja wea wachumia tumbo katika siasa chafu za kisisiemu!

Hujanielewa nasema approach yake sio nzuri inaleta chuki na ndiyo maana anasababisha ndugu zake wanaanza kuchinjana!
 
mimi nilijua haya yatakuja wanajaributu kufurukuta m4c imebana mpaka mbavu.ngoja nipite coz sikuepo mjini nasikia makamanda kina miliya walikua nmc ngoja nikajue yaliyojiri
 
Hujanielewa nasema approach yake sio nzuri inaleta chuki na ndiyo maana anasababisha ndugu zake wanaanza kuchinjana!

mwigulu umejitakia mwenyewe m4c haiachi mtu, ungetulia kama wenzako labda ungepata huruma ya m4c
 
Kawaida kila mkusanyiko au mkutano ni lazima upate kibali cha polisi ili kutoa ulinzi, je kwenye mkutano huo hakukuwa na ulinzi?na chanzo cha kazia hii lazima kijulikane, je walioanzisha walikuwa na nia gani?na kama hakuna mbona hakuna vyombo vya habari havijatoa taarifa hiyo?nafikiri kuna haja ya kuirenovate hii thread

Polisi hawana ubavu wa kukabiliana na wana ccm walidhamiria kimkakati kuisambaratisha nchi hii. Wanajua wananchi wamewakataa, sasa wanafanya vurugu ili ionekane CDM ndo wakorofi. Mpango wa kufanya vurugu katika mikutano ya Chadema unaratibiwa na uongozi wa juu wa ccm na kutekelezwa na UVCCM.
 
Avanti naona wewe na Mama Porojo mmejipanga.

Naweka taarifa toka kwa Tumaini Makene.


Wakuu na Mods

Njia ya muongoni fupi sana. Wabunge wa CHADEMA wasiokuwa na majina wamefika Ndago saa 8.30 mchana?????!!!!!!

Wakuu, kuna Operesheni ndogo kwa Mkoa wa Singida yakiwa ni maandalizi ya operesheni kubwa kwa mikoa mitano, Singida, Iringa, Dodoma, Manyara na Morogoro, kama ilivyoazimiwa na Kamati Kuu mapema wiki hii.

Kazi hiyo iko chini ya timu inayoongozwa na Kamanda Mwita Mwikabwe Waitara, yeye ndiye mratibu wa ziara hii fupi na leo ilianzia katika Wilaya ya Iramba, Jimbo la Iramba Magharibi, ambapo mikutano ya hadhara imefanyika katika maeneo ya Ndago na Kinampanda.

Kulikuwa na taarifa tangu siku tatu zilizopita, timu ikiwa bado Dar es Salaam, kuwa kuna kikundi cha vijana wamekodiwa, wananunuliwa pombe, wakiandaliwa kufanya fujo ili mkutano huo usifanyike kisha ionekane CHADEMA wameshindwa kufanya mkutano kwa Mwigulu Nchemba. Bahati mbaya sana kitumbua chao kimeingia mchanga. Nafikiri hata huyu mleta maada ni sehemu ya hiyo propaganda.

Sasa wakati mkutano umefunguliwa tu, Kamanda Mwita akawa-preempty kwa kuwaambia kuwa taarifa hizo tayari zinajulikana na polisi wawe makini. Haa! Jamaa waka-panic. Walikuwa mbele kabisa pale. Wakaanza kurusha maneno, wanapiga makelele, wanazunguka zunguka pale mbele ya hadhara. Mbele ya polisi. No action.

Kelele za kundi lile, hazikuwa zikivumilika. Wananchi hawakukubali uvunjifu wa amani wa makusudi uliokuw aukifanywa mbele ya polisi. Yaani sinema ile ilikuwa Ilemela-type, kule ambako wabunge wa CHADEMA walivamiwa, kukatwa mapanga mbele ya polisi wenye silaha. Brothers, huwezi kuamini lile kundi likajitenga pembeni na kuanza kurusha mawe.

Wananchi wengi waliokuwa pale mkutanoni kwa mamia, hawakukubali ufidhuli ule. Wakawafukuzilia mbali wale wahuni. Mkutano ukaendelea kwa amani kabisa, kisha tukaelekea mkutano wa pili Kinampanda, ambako John Mnyika, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi na Mbunge wa Ubungo, amemaliza kupiga nondo kama alivyopiga Ndago.

Wananchi wamemskiliza John kwa makini, sasa kazi zinanunuliwa. Nondo zinawagusa wananchi wa Iramba Mashariki, yakiwa ni maandalizi ya Opereseheni kubwa inayokuja mikoa hii muda si mrefu

by Tumaini Makene.

This is a sided one, kujikosha huko ina maana hujui mmeua?
 
Hujanielewa nasema approach yake sio nzuri inaleta chuki na ndiyo maana anasababisha ndugu zake wanaanza kuchinjana!
Kwa nini Mwigulu hapewi mialiko kwenye hicho kipindi cha this week in perspective?
 
kimsingi mkumbo hajaua ndugu zake, hapa ni chama cha chadema kilikuwa kinafanya kazi ya kisiasa, na haki yake kufanya kazi kama chama cha siasa.sababu uhai wa kisiasa ni kuwasilina na wanachma wake ili kujenga chama.Kma kuna wafuasi wamefanya hivyo ni kivyao.Rejea kesi ya mauaji wakati wa kampeni za uchaguzi 2010, wakati shibuda anagombea kwa tiketi ya chadema-maswa, ccm na mkuu wa polisi alishadadia kuwa shubuda alihusika, baada ya uchunguzi kaonekana hajaua.atakuwa amefanya hivyo kama aliagiza wafanye hivyo, lakini kama walijichukulia sheria mkunoni, ni wale tu waliohusika ndo watashitakiwa.hata hivyo polisi walikuwa wapi wakati matukio hayo yanatokea?
 
hii habari bado sijajua ukweli wake lkn kwa jinis ilivyo naweza kusema kwamba kama mnyika amekwenda ktk jimbo la nchemba katika kipindi ambacho wana uhasama na kesi bungeni, atakua amefanya kosa.

Mnyka ana haki ya kwenda popote hapa TZ lkn kwa mtu mwenye busara asingekwenda kwa nchemba muda huu. sijaweka siasa mbele bali utanzania wangu!

ndugu zanguni maswala kama haya tuwe tunayajadili kwa kuweka ubinadamu na utanzania mbele
wakuziba wewe kweli unafaa kuzibwa maana you are an empty hole! Aliyempa Mwigulu sovereign power mtaa wowote kwenye nchi hii ni nani? Kwa akili yako unahalalisha yeye kufanyia watu fujo simply because yuko jimboni kwake? Kwa maana yako hiyo watanzania wote wasiokubaliana na sera za JK ambaye kwa sasa ndiye raisi wa eneo lote lililo ndani ya mipaka ya nchi hii waende wakafanyie siasa nchi gani?

Hadi tuje tutoke kwenye matongotongo ya watu kama wewe bado tuna safari ndefu kweli!
 
Last edited by a moderator:
This is a sided one, kujikosha huko ina maana hujui mmeua?

Kitila Mkumbo yuko online kwenye ule uzi mwingine wa Mama Porojo. Njia ya mwongo kweli fupi au wafanyavyo wachumi daraja la kwanza?
 
​mwigulu na ccm wake ni majambazi wastahili adhabu ya kifo na siku zao zinahesabiwa kama wamemtuma mkenya sisi tutatuma mcongo
 
Katika kile kinachoonekana kukomaa kwa uahasama kati ya Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika, na Mbunge wa Iramba magharibi, mtu mmoja mpaka sasa amethibitishwa kufariki na wengine 3 wapo mahututi baada ya Kikundi kinachosadikiwa kuwa kilikodishwa na Mwigulu Nchemba ili kwenda kuleta fujo katika mkutano wa Mnyika. Mnyika kama kawaida yake kwa upole wake hakukimbia eneo hilo na watu hawakumpiga. Ila wafuasi wa CCM waliotumwa kufanya fujo ndio walianza kurusha mawe hata kabla ya Mnyika kuwasili eneo hilo. Nitaendelea kuwajulisha yanyojiri. Ila viongozi wetu wapo Salama. Nchemba ametufanyia mambo ya hali ya chini sana ambayo hatukuyatarajia kwa siasa za Singida. Kununua watu, kuwapa pombe na kuwafundisha kwenda Mikutanoni kupiga watu mawe. Ikumbukwe kuwa hata Kikosi maalumu kwa ajili ya fujo za Uchaguzi wa Igunga ziliratibiwa katika jimbo lake, Kijiji cha Ulemo, kikosi hicho kilikuwa kinapatiwa mafunzo ya Kijeshi. Huyo ndo Mwigulu Nchemba.
 
.... Kwa kuwa pia wanaCCM walisikia maneno makali ya chuki toka kwa Mnyika yakienda kwa Mwigulu na wanaCCM basi baadhi yao ambao walikuwa wamejichanganya katika mkutano wa Chadema walianza kuguna. Katika hali hiyo wale wa CCM wakawa wametambulika kuwa wamo na wamevamia mkutano wa Chadema na hivyo wakaanza kupigwa. Wakati huo huo wale waliokuwa wakitoka uchaguzini nao wakaanza kukimbizwa na mmoja wao kuingia ndani ya nyumba jirani ambapo alitolewa na nje na kupigwa mpaka kifo, Mwingine alipigwa na haijulikana ana hali gani.

My take: Inasemekana Kitila Mkumbo alikuwepo katika mkutano huo ikiwa ni jitihada za kuanza kumnadi ili akamn'goe Mwigulu. Pamoja na kussupport move yake naona tayari ameshaanza kuingia dosari. Sijui anajisikiaje kusababisha watu wake kufa. Siku zote namwona anajaribu kumpinga Mwigulu, lakini njia anazotumia sio sahahi, mfano siku moja katika kipindi cha "This week perspective" nilmwona alivyokuwa akihangaika kupinga hoja za Mwigulu bungeni. Kikubwa bwana Kitila Mkumbo nadhani unaanza kujichafua sasa wenzako wanaktumia wewe hadi unaua ndugu zako kwa sababu ya siasa tu. Tunakusubiri!

Inawezekana hujatofautisha maneno makali na ya chuki na maneno ambayo ni Critical.Critics ni sehemu ya muhimu ya jamii.Holywood kabla hawajatoa movie huwa wanazipeleka kwa critics.Ndio maana zikitoka zinawashika mpaka waichukiayo marekani na utamaduni wa magharibi.

Kama kweli palitokea vurugu si Kitila alijiharibia bali ni CCM kwa kuingilia mkutano.Hapo juu umesema kuwa kuna wana ccm walikuwa ndani ya office na waliokuwepo katika umati wa wana CDM.Na hao waliokuwa ndani ndio waliojikuta ktk vurugu.

My take:CCM wanajiweka pabaya sana, na kitendo cha kuwatuma wafuasi wao katika mahubiri mazuri ya CDM ni kuwafanya wa retard as time goes by.Na Mwigulu kajiweka pabaya sana kuingia katika malumbano na CDM.
 
HEARSAY EVIDENCE IS NEVER ADMISSIBLE! ASANTE TUMAINI MAKENE...INAONYESHA ULISHUHUDIA INGAwa sio lazima kuwa ni ukweli!
 
Back
Top Bottom