Tetesi: Hali si shwari SGR muda huu. Wafanyakazi wanadaiwa kuanzisha mgomo

IPTL

JF-Expert Member
May 12, 2014
226
172
Hali si shwari katika mradi wa SGR unaojengwa na Mkandarasi Yapi Merkez kutoka Uturuki kutokana na mgomo ulioanza leo wa Wakandarasi wa Kitanzania kusimamisha Construction equipments, Tipper, mabasi ya kubeba Wafanyakazi na Pick-Ups kwa ajili ya kubeba Ma enginia kuwapeleka site.

Habari za ndani kutoka katika kikubwa cha Soga ni kwamba kwa sasa kazi zimesimama na viongozi wa Yapi Merkez wamekusanyika kwa ajili ya kikao ili kutafuta suluhu ya jambo hilo.

Hata hivyo Rais Magufuli aliwahi kutoa maelekezo na kuagiza kwamba hao Wakandarasi wa hapa nchini walipwe fedha zao wanazodai kwa muda mrefu, lakini hadi sasa Yapi Merkezi hawajatekeleza agizo hilo la Rais.
 
Kiukweli huo mradi umejaa usanii, mradi ilikua ukamilike mwezi wa 2 mwaka huu, Serikali ikawaongezea miezi 6 wakiwa na maana mradi ukamilike mwezi wa nane.Sasa mwezi wa nane ndio huu na mradi hauna dalili za kukamilika, kuna kampuni moja iliwafanyia calibration ya baadhi ya vifaa kufanya malipo imewachukua miezi 8, walivyorudi wafanyiwe calibration tena kampuni ikagoma kuwafanyia.

Sasa walichokuja nacho nikufukuza baadhi ya watu iliowaajiri ili kupunguza matumizi, Zaidi ya robo tatu ya waajiriwa wamefukuzwa, kisha kazi wamepewa subcontractors. Lakini kwa bahati mbaya wameshindwa walipa subcontractors hata robo ya fedha wanazodai kiukweli inaumiza na kusikitisha sana.

Huu mradi Dar-Moro utaisha 2022 ,sasa huko kwingine itachukua zaidi ya miaka 15 kumalizika.
 
KWANI TATIZO KAMA RAIS ALISHASEMA WALIPWE INAMAANA PESA IPO KWANINI YAPI HAWALIPI WAKANDARASI?
Rais alishatoa maagizo hela hizo zilipwe lakini hawa Waturuki wahuni tu. Leo acha washikishwe adabu kazi zimesimama hakuna kinachoendelea mashine zimesimama, ma tipper, mabasi na pick ups zote zimesimama. hakuna kinachoendelea leo. madereva na waendesha mashine wamekaa.
 

Attachments

  • PHOTO-2020-08-03-09-54-54.jpg
    PHOTO-2020-08-03-09-54-54.jpg
    117.9 KB · Views: 2
  • PHOTO-2020-08-03-10-09-26-1.jpg
    PHOTO-2020-08-03-10-09-26-1.jpg
    54.1 KB · Views: 2
Ukisoma uzi hapo kwa umakini utaona tayari JPM alitoa maelekezo watu walipwe madeni yao,nadhani kinachofuatia ni utuambuaji tu.,
Msikilize JPM alivyotoa maagizo ambayo Waturuki hawakuyatekeleza. Haya Waturuki wanatuchezea sana sisi Watanzania wanatuona wapole, sasa ngoja waonje joto ya WaTZ. Hivi kweli sisi tungefanya hivi nchini kwao wangekubali unatumia vifaa vya watu miezi yote hiyo karibu mwaka hulipi hata senti.
 

Attachments

  • VIDEO-2020-08-03-09-54-54.mp4
    14.4 MB
Sasa Kama pesa hawana wanafanyaje
Walisaini vipi mradi ambao mchina kakataa kuufanya kwa tril 7, watulipe kiukweli baadhi ya waturuki walikamatwa wanatorosha mamilion airport, hizo fedha wanazotorosha siwangezitumia kulipa subcontractors?.
 
Msikilize JPM alivyotoa maagizo ambayo Waturuki hawakuyatekeleza. Haya Waturuki wanatuchezea sana sisi Watanzania wanatuona wapole, sasa ngoja waonje joto ya WaTZ. Hivi kweli sisi tungefanya hivi nchini kwao wangekubali unatumia vifaa vya watu miezi yote hiyo karibu mwaka hulipi hata senti.
Si angefanya tu safari ya kushitukiza akaenda kulipa mwenyewe,mbona anatembeaga na maburutu ya pesa
 
Mimi nipo site na hakuna mgomo wala dalili ya mgomo. Hivi huu umbeaumbea Chadema mtaacha lini
 
Kazi ya taifa tufanye kazi kizalendo si busara kuwagomea wageni wanaotujengea miundo mbinu ya uchumi wa kati .. ...tuwe na subira 😂😂
 
Back
Top Bottom