Uchaguzi 2020 Hali si hali: Katambi 'akataliwa' na 'kugomewa' Shinyanga Mjini, Masele aombwa kumsaidia. Ahaidiwa Ubalozi

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Hali ni tete kwa mgombea wetu wa CCM hapa katika Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi. Katambi ambaye alikataliwa na 'Wajumbe' wakati wa kura za maoni ndani ya CCM, alipitishwa 'kibabe' na Kamati Kuu na NEC ya CCM kule Dodoma. Katambi, katika kura za maoni, aliachwa mbali mno na aliyekuwa Mbunge wa hapa Steven Masele ambaye jina lake lilikatwa Dodoma.

Katika kuonesha kinyongo kisicho na uongo, makada wa CCM hapa Shinyanga Mjini wamekuwa wakijitenga na Katambi hadharani na sirini. Katika harakati za kuokoa jahazi na kuulinda ushindi wa CCM, Mbunge wa zamani Masele 'ameombwa' na viongozi waandamizi wa CCM Taifa kumsaidia Katambi katika kampeni zake. Ameahidiwa kuwa endapo CCM ikishinda Urais atapatiwa nafasi ya Ubalozi au nyingine tamutamu.

Masele hana tatizo na hilo. Lakini, wafuasi na wasukamipango wake wamegoma 'kumruhusu' kumsaidia Katambi wakidai kuwa Katambi hauziki hata kama utapigwa na muziki. Pamoja na kwamba CCM ndiyo watetezi wa hapa Shinyanga Mjini, hali yetu si nzuri kulingana na taswira iliyochorwa ya mgombea wetu. Katambi anatajwa kama asiye na ushawishi wowote na kusemwa kuwa 'anatakiwa' tu Bungeni kwenda kuwaongelea mbovu wapinzani.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Shinyanga Mjini)
 
CCM ina miaka michache sana ya kuishi hapa Tanzania. Ukija kwa Mwenyekiti wao, naye kwa sasa anatembelea tu nyota ya wasanii wa bongo fleva!

Wasingekua hao wasanii, hakuna Mtanzania ambaye angeenda kusikiliza hotuba zao! Maana hawana jipya la kutuambia.

Stori zao ni zile zile! Tunatoa Elimu Bure, tumenunua ndege, nk. Huku maisha ya Watanzania walio wengi yakiendelea kuwa magumu kutokana na sera zao mbovu.
 
Hali halisi haipo hivo usemavyo,,,

Ni kama umetumwa kuchafua huku ukijifanya wewe ni wa cCm,,.
 
Back
Top Bottom