Hali niliyoiona Moshi-Kilimanjaro inatisha muda huu

Akilitime

JF-Expert Member
Dec 27, 2017
581
757
Wasalaam,

Leo nimebahatika kupita stand kuu pamoja na mitaa inayouzunguka Mji wa Moshi.

Aisee bado Watanzania hatujachukulia corona katika uzito wa juu! Kiukweli ugonjwa huu Kama upo mitaani Basi sambaa yake itakuwa mithili ya 5G.

Yani nimejionea watu stand wakiishi kana kwamba hakuna kinachochoendelea dhidi ya corona, nimejionea vijana wadogo wa shule wakinunua mahindi ovyo ovyo stand na kula , huku wateja wengine wakigusagusa hayo mahindi na kuyaacha pale na wengine wanakuja wananunua hayo hayo.

Saivi zoezi la kunawa mikono halitiliwi tena maanani, mji mzima nimewaona watu wawili tu wakiwa wamevalia viziba midomo.

Kwakwel kwa jinsi corona inavosambaa afu ukitizama na mienendo tuliyonayo mda huu, Basi utabakia kusema bado Mungu ameweka mkono wake juu ya Tanzania.
 
Mizaha bado ni MINGI MNO kuhusiana na suala hili. Sijui tunataka tufe kwa kiwango kipi kabla hatujaanza kuchukua tahadhari. ELIMU bado inahitajika sana ikibidi vyombo vya dola viigilie kati haraka na kudhibiti hali.

Kwenye sekta ya usafirishaji abiria (hasa mikoa isiyo na maambukizi) suala la Covid 19 bado linachukuliwa kama stori za bibi za usiku!! Kinachokuja Mungu atusimamie tu aisee, maana lockdown kwa taifa kama letu hili ni zaidi ya janga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hapo bado tunatangaza idadi ya maambukizi, vipi tukinyamaza kama tulivyoshauriwa na waziri mstaafu wa mambo ya ndani?

Mkuu ni hatari sana, kwa nchi ya Kenya confirmed cases zinaenda 250.

Lakini sababu ya idadi kuonekana kubwa ushaijua?

Jibu ni kwamba kwa leo tu tayari wananchi karibia 820 walikuwa wamepimwa kwa siku moja tu.
 
Mkuu ni hatari sana, kwa nchi ya Kenya confirmed cases zinaenda 250.

Lakini sababu ya idadi kuonekana kubwa ushaijua?

Jibu ni kwamba kwa leo tu tayari wananchi karibia 820 walikuwa wamepimwa kwa siku moja tu.
Yah! Mtu akijua hali yake mapema ni bora kabisa, kwani ataanza tiba mapema na pia atawakinga na wengine wasiambukizwe kupitia yeye
 
Corona ipo Arusha.. dar.. mwanza.. bukoba.. Moshi hakuna Corona tafadhal Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Taarifa ya Leo,Kilimanjaro amepatikana
IMG_20200415_174536.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom