Hali ni tofauti ya Katiba Mpya, Wananchi wadai Tanganyika yao, Toa maoni yako miaka ya 51 ya uhuru

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,006
[h=1]Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni sawa na ndoa ya mkeka’[/h]
ico_plus.png
Share
ico_bookmark.png
bookmark
ico_print.png
Print
ico_email.png
Email Rating

katiba.jpg
Geremia Kulwa (45) mkazi wa Kata ya Kunduchi Jijini Dar es Salaam akitoa maoni yake mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Amependekeza watendaji katika ofisi za umma wasizigeuze ofisi hizo kama kampuni zao binafsi bali wawahudumie wananchi kwa haki (Picha na Matern Kayera)


Posted Jumapili,Decemba9 2012 saa 10:20 AM
Kwa ufupi
“Hakujawahi kuwepo kwa nchi inayoitwa Tanzania Bara wala Tanzania Visiwani. Haya ni mapungufu ambayo Katiba Mpya inatakiwa kuyarekebisha ili historia ibaki kama ilivyokuwa. Tanganyika itambulike kwa kuwa Muungano uliopo ni kati ya nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar,” anasema Adventina Ndibalema mkazi wa Kimara Korogwe.


MCHAKATO wa utoaji wa maoni ya Katiba Mpya unaendelea kwenye mikoa sita katika awamu hii ya nne. Mikoa ambayo Tume iko katika kuchukua maoni ya wananchi ni Arusha, Dar es Salaam, Mara, Simiyu, Geita pamoja na Zanzibar Mjini Magharibi. Katika mikutano hiyo ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wananchi wamekuwa wakitoa maoni mengi yenye hoja tofauti.



Katika mikutano hiyo, wajumbe wa Tume wamekuwa wakiwahimiza wananchi kushiriki kwa uhuru katika kutoa maoni yao bila hofu. Wito huo wa Tume umekuwa ni jambo la msingi ikizingatiwa kwamba Watanzania wengi wamekuwa na tabia ya kuogopa na hata kukosa ujasiri wa kuzungumza hadharani kwa kuikosoa ama Serikali au viongozi wake kwa hofu ya kuogopa kukamatwa au kufuatiliwa na vyombo vya usalama.

Katika mchakato unaoendelea wa ukusanyaji wa maoni ya wananchi, imeshuhudiwa wananchi hao wakijieleza kwa uhuru bila hofu kwenye mikutano mbalimbali ya Tume.

Hii ni haki yao ya kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Kitu ambacho wananchi kwenye kila mkutano wa Tume wamekizungumzia ni suala la Muungano wa Serikali tatu.

Wananchi wengi wamekuwa wakisisitiza kuwa Katiba Mpya haina budi kuitambua na kuirejesha Serikali ya Tanganyika. Wananchi hao wamesema kuwa Serikali ya Tanganyika ni haki ya Watanganyika kama ilivyo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

“Watanganyika tumekosa fursa ya kuwa na Serikali tofauti na wenzetu Wazinzibari ambao wao wanayo Serikali. Kwa hiyo nataka kuona kuwa Katiba Mpya inairejesha Serikali ya Tanganyika ili kuleta uwiano sawa kati ya pande mbili za Muungano,” anasema Haji Juma mkazi wa Kata ya Jangwani Jijini Dar es Salaam.



Hoja hiyo inaungwa mkono na Thadeus Mangia mkazi wa Tabata Kimanga ambaye ameufananisha muundo wa Muungano uliopo kuwa sawa na ndoa ya mkeka. Anasema kuwa Katiba Mpya inapaswa kuheshimu uamuzi wa wananchi juu ya aina gani ya Muungano wanaoutaka na siyo kulazimishwa waishi kwenye Muungano wasioutaka. Mangia anasema kuwa muundo unaowafaa Watanzania kwa sasa ni Muungano wa Serikali tatu.

Mangia anasema kuwa Muungano wa Serikali tatu utaondoa manung’uniko yaliyopo miongoni mwa wananchi kuwa upande fulani unaonewa na upande fulani wa Muungano ndiyo unaofaidika.

Anasema suluhu ya matatizo ya Muungano ni kuirejesha Serikali ya Tanganyika kama ilivyo kwa Serikali ya Zanzibar kisha iundwe Serikali ya Jamhuri ya Muungano.



Wananchi hao wanasisitiza kuwa katika Muungano huo walioathirika ni Watanganyika kwa kupoteza Serikali yao. Wanasema Wazanzibari wana Rais na Serikali tangu mwanzo wa Muungano, lakini Watanganyika wamepoteza vyote, yaani Rais na Serikali. Kutokana na hali hiyo, Mwalimu Florah Ishengoma (50) kutoka Tabata Kimanga anasema kuwa Muungano uwe wa Serikali moja na hilo likishindikana basi Serikali ziwe tatu ili na Watanganyika nao wapate haki yao.

“Kila siku wenzetu Wazanzibari wanalalamika kuwa wao wamemezwa na muundo wa Muungano huu.

Sasa ili kuondoa malalamiko, napendekeza kuwapo Serikali tatu, yaani ya Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Kama hilo haliwezekani napendekeza tuwe na Serikali moja, Rais mmoja na mawaziri wakuu wawili, mmoja wa Zanzibar na mwingine wa Tanganyika, na hao mawaziri wakuu wachaguliwe na Bunge,” anasema Hamad Tao mkazi wa Kata ya Ilala.



Wananchi hao wamezidi kusisitiza kuwa Katiba iliyopo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inapotosha historia kuhusu suala la Muungano kwa kuwa imeiua Tanganyika na badala yake imeanzisha kitu kinachoitwa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani. Wanasema kuwa hakuna nchi inayoitwa Tanzania Bara iliyoungana na Tanzania Visiwani ikatokea Tanzania.





Hakujawahi kuwepo kwa nchi inayoitwa Tanzania Bara wala Tanzania Visiwani. Haya ni mapungufu ambayo Katiba Mpya inatakiwa kuyarekebisha ili historia ibaki kama ilivyokuwa. Tanganyika itambulike kwa kuwa Muungano uliopo ni kati ya nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar,” anasema Adventina Ndibalema mkazi wa Kimara Korogwe.

Katika Sura ya Kwanza, Ibara ya (1) na Ibara ya 2(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 zinaeleza maana ya Muungano. Ibara hizo kwa pamoja zinasema kuwa Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano. Inaendelea kufafanua kuwa eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.

Ibara hizi hazisemi chochote kuhusu nchi za Tanganyika na Zanzibar, bali zimebadilishwa jina na kuitwa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Hapa ndipo wananchi wengi kwenye mikutano ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba wanapotaka Serikali ya Tanganyika irejeshwe kama ilivyokuwa kwa Serikali ya Zanzibar ambayo ipo tangu Muungano uanzishwe, Aprili 26, 1964.


Mwenyekiti wa Chama cha NLD (National League for Democracy) Dk Emmanuel Makaidi ameiambia Tume kuwa Serikali ya Tanganyika iliyouawa wakati wa Muungano inatakiwa kurejeshwa kupitia Katiba ijayo. Dk Makaidi anasema kuwa Wazanzibari katika Katiba yao, wanaitambua nchi yao, lakini Tanganyika haitambuliki mahali popote.



Kutokana na sintofahamu iliyopo kuhusu Tanganyika, Dk Makaidi kama ilivyo kwa wananchi wengine anaona kuwa Serikali ya Tanganyika ni haki ya Watanganyika ambayo hainabudi kurejeshwa kupitia mchakato huu wa kurekebisha Katiba ya nchi. Anasema kuwa kuuawa kwa Serikali ya Tanganyika ni kesi ambayo kwa muda mrefu haikupata majibu, lakini sasa majibu yake yapatikane kupitia Katiba ijayo.



“Haiwezekani tuwe kwenye Muungano ambao unaruhusu upande mmoja wa Muungano kuwa na Serikali yake, Bunge lake na kila kitu, halafu upande mwingine uwe umepoteza Serikali na mambo yake yote. Wenzetu wa Zanzibar wanayo Serikali lakini Tanganyika haijulikani iko wapi, ni bora tuungane na Burundi kuliko kuendelea kuwa kwenye Muungano huu,” anasema Abeid Rutozi ambaye kitaaluma ni mkalimani kutoka Kata ya Saranga jijini Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom