Hali ni tete mkoani Manyara; mwekezaji achinjwa!

kipindupindu

JF-Expert Member
Dec 16, 2010
1,053
170
Inasemekana ule mgogoro unaoendelea mkoani Manyara umezidi kushika kasi baada ya mwekezaji mmoja kuwekewa kizuizi na hatimaye kushambuliwa kwa mapanga mpaka kufa na watu wasiojulikana.

Polisi wameweka kambi eneo la tukio kuwasaka wahusika.

Source: Usiku wa habari TBC.
 
Mbona heading yako ni kama unataarifa za uhakika, kumbe unaulizia?

Fanya uchunguzi mdau kisha tumwagia taarifa
 
Inasemekana ule mgogoro unaoendelea mkoani manyara umezidi kushika kasi baada ya mwekezaji mmoja kuwekewa kizuizi na hatimaye kushambuliwa kwa mapanga mpaka kufa na watu wasiojulikana.polisi wameweka kambi eneo la tukio kuwasaka wahusika.

Source:usiku wa habari TBC.
 
Inasemekana ule mgogoro unaoendelea mkoani manyara umezidi kushika kasi baada ya mwekezaji mmoja kuwekewa kizuizi na hatimaye kushambuliwa kwa mapanga mpaka kufa na watu wasiojulikana.polisi wameweka kambi eneo la tukio kuwasaka wahusika.

Source:usiku wa habari TBC.
Mkuu,
Du!...Nimekubali REPORTING ni taaluma ya watu!..
Au mkuu kuna mtu anatumia ID yako kisiri nini?
 
Kila tukiishauri serikali itatue vyanzo na sio matokeo tunaambiwa sisi wanacdm? watu washachoka jamani na tusipo angalia hili wimbi litasambaa nchini!
 
Wananchi wamepata mwamko,wanataka AZIMIO LA ARUSHA,lirudi kwa vitendo,kwa muda mrefu watanzania wanateseka,ile hali rasilimali zinawanufaisha wageni,hao wawekezaji hapo,walimilikishwa hayo mashamba isivyo halali,na wenye mashamba wakatimuliwa,wanateseka na familia zao,mbaya zaid wanacholima huwa kinavunwa na kusafirishwa nje ya nchi,pasipo hata mamlaka husika kuelewa lolote!!
 
sasa kama wananchi wanzulumiwa haki yao na wageni na serikali inatizama sasa wafanye nini nikujichukulia maamzi mkononi
 
Kwa mbali naona kama yale ya zimbabwe ya kugombana na wawekezaji inainyemelea tanzania yetu
 
Hatari hii maana tumeanza kuuana wenyewe kwa wenyewe. Hilo jina la Kitanzania. Mbona wawekezaji wazungu hamuwaui mnawaua watanzania? Hii balaa!!!
 
Back
Top Bottom