Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,729
- 524
Nimefika Arusha mida ya saa 10 jioni ya leo. Kawaida yangu huwa nanunua magazeti 3 kila Jumapili, mawili kati ya hayo ni Mwananchi na Tanzania Daima, naweza kuvumilia kukosa Taznania Daima lakini huwa ni vigumu sana kulikosa Mwananchi. Nilipoingia Arusha nilipata magazeti mawili tu mojawapo Tanzania Daima lakini Mwananchi lilikuwa limeisha.
Kwa kuwa huwa sivumilii kokosa Mwananchi, ilipbidi nianze kulisaka maeneo yote ya mjini bila mafanikio! Nilipowauliza wauzaji kulikoni? Wakaniambia habari ya Ledma ndiyo imesababisha Mwananchi liwe lulu leo; muuzaji wa mwisho aliniambia wala nisijisumbue, siwezi kulipata Mwananchi Jumapili kwa sababu ya habari ya Mbunge Lema na picha yake (akiwa amelazwa hospitalini).
Wadau, Jeshi la Polisi Arusha linaweka mji wetu katika ali tete kwa sababu ya utendaji wake wa kisiasa. Kabla ya ACP RPC Matei hajaondolewa mambo yalotendeka yasingeweza kutokea maana kama angekuwa juha kama alivyo huyu OCD aliyeongoza Polisi kumpiga Lema basi siku ya kutangaza matokeo kungetokea vurugu ambayo haijapata kuonekana. Inasemekana RPC Matei ndiye aliyemlazimisha Mkurugenzi wa Manispaa kutangaza matokeo kama yalivyo kuwa (Lema kushinda) na hilo ndilo lililomgharimu hadi kuondolewa Ukamanda wa Polisi Arusha.
Watendaji kama RPC, OCD na Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha wanachochea vurugu hapa Arusha maana watu elfu 56 waliompa Lema kura zao, ikiwa wataingia mtaani basi itabidi Polisi wa Kilimanjaro na Manyara wahamie Arusha kwa muda.
Wito wangu kwa Serikali- KJ na Pinda ni kuwaonya watendaji wa serikali kuachana na kufanya kazi kwa ushabiki na badala yake waheshimu misingi ya kisheria kwenye utekelezaji wa kazi zao vinginevyo wasishangae kuona amani inapotea mikononi mwao.