Hali ni mbaya mno nini kifanyike kuwanusuru wajasiliamali wasifilisiwe na mabenki?

Bizney

JF-Expert Member
Aug 2, 2013
454
48
Poleni na majukumu wana JF

Pamoja na kuambiwa kuwa uchumi wetu umepanda lakini hali ni mbaya mno, nasema hali ni mbaya tena mno wafanyabiashara/wajasiliamali wa kada zote wanalalamikia ugumu wa hali kibiashara, wengi wetu mnajua kuwa wafanyabiashara/wajasiliamali wengi wanaendesha shuguli zao kupitia taasisi za mikopo hususani mabenki. Sasa kuna tishio la watu kufilisiwa mali zao kwani wengi wao wamekopa na wameshindwa kulipa kutokana na ugumu wa hali.

Swali ni Je! nini kifanyike ili kwanusuru watu hawa?
 
Hakuna ujanja zaidi ya kulipa maana wasipolipa hiyo hali inayowapata wajasiliamali itarudi kwa bank.
 
Hilo ni kweli kabisa,biashara ina changamoto nyingi sana na hasa ukizingatia source of fund ya kuendesha hizo biashara ni mikopo ya kibenki,mbali na hilo pango za frame nazo zinachangia sana maana wenye frame zao wanapandisha kodi kiholela pasi na kuzingatia hali halisi ya kibiashara.
Kuna kipindi nilipanga kabisa kufanya biashara ila sasa mtaji ulikuwa haujitoshelezi kutokana na kiasi kikubwa kwenda kwenye pango na nimeamua kufanya Plan B ktk kilimo cha alizeti.
Hapo kwa walio ktk dhahama hiyo hawana budi kubadilisha biashara ama hata mahali pa biashara na kutafuta sehemu yenye customers wa kutosha.
 
Wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo wadogo waungane wao kwa wao kisha washirikiane kukuza mitaji ya pamoja, hapo hata kukopeshana kwa riba ndogo na masharti nafuu inakuwa rahisi sana. Pia wakiwa na ushirikiano wataweza hata kunasuana dhidi ya mali zao kuchukuliwa na mabenki ili kufidia madeni yao, watasaidiana kulipa kwa urahisi zaidi
 
amchukue mkewe amkabidhi kwa meneja wa benki ili amuhudumie meneja huyo labda ataburudika na kumpunguzia riba kidogo.
 
Usikope kuanzisha biashara, kopa kukuza biashara ambayo changamoto sake ulishazijua kitambo na ufumbizi wake unaujua. Ukikurupuka, imekula kwako
 
Hapa ndo wabongo mnapojichanganya, wachuuzi mnawaita wajasiliamali! hahahaaa, muuza vitumbua na mmiliki wa shirika la ndege wote mnawaweka pamoja. Mjasiliamali wa kweli anaanza kuwekeza kwenye elimu anajua ni wapi akope na kwa riba gani na lazima anakuwa amejipnga kimkakati (strategic).

Wanaofilisika na kushindwa kulipa madeni ni wachuuzi sio wajasiliamali.
 
Wafanya biashara ni wachache sana Tanzania na wajasiliamali ni wachache sana
 
Pole Kuna tatizo kubwa sana nchi zetu wengi wanao itwa wajasiliamali hawajafundishwa kufanya biashara wala namna ya kuanza biashara. Kama ungefundishwa vizuri pengine usinge hitaji hata kukopa ili uanzishe biashara.Naomba ijulikane kuwa biashara nayo ni taaluma. Kwanza benki nyingi hazikopeshi ili kuanzisha biashara bali kuendeleza biashara hizo. Wanaojua namna ya kuanzisha biashra huwa wanaanzisha biashara hata bila kuwa na pesa. Kabla ya kuanzisha biashara tafuteni wataalamu wawafundishe hilo kwanza.lakini tahadhari usitafute watalamu wa darasani tu, tafuta watalamu ambao wao nao wanafanya biashara hiyo maana wengi wanajua biashara ya vitabuni tu sio practice. Tatizo ligie kubwa mno ambalo halizungumzi sana. Hili linafanya wengi wasifike mbali kwenye biashara ni kwamba wajasiliamali wengi hawajui namna ya kutafuta masoko. kama hujui kutafuta masoko hutafika mbali kwenye biashara. Watalamu wa biasshara wanasema kujua namna ya kutafuta masoko ni ujuzi namba moja. (knowing how to find markets or sell is skill number one). You can call me for free advice. Huwa nawasaidi wajasiliamali kuanzisha biashara bure.+255 689 417 472
 
Poleni na majukumu wana JF

Pamoja na kuambiwa kuwa uchumi wetu umepanda lakini hali ni mbaya mno, nasema hali ni mbaya tena mno wafanyabiashara/wajasiliamali wa kada zote wanalalamikia ugumu wa hali kibiashara, wengi wetu mnajua kuwa wafanyabiashara/wajasiliamali wengi wanaendesha shuguli zao kupitia taasisi za mikopo hususani mabenki. Sasa kuna tishio la watu kufilisiwa mali zao kwani wengi wao wamekopa na wameshindwa kulipa kutokana na ugumu wa hali.

Swali ni Je! nini kifanyike ili kwanusuru watu hawa?

Waache wenye fedha wazichukue si mlizikopa?
 
Ni kuanzisha SACCOS yao
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom