juve2012
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 3,343
- 2,022
Ni saa kumi jioni, Natoka zangu taratibu kuelekea mazoezini. Inanibidi nipande daladala na kusafiri umbali wa kilomita tano kufika uwanjani maana huku kwetu hakuna viwanja vya michezo. Hata shule zilizopo karibu hazina viwanja.
Maeneo ya wazi yote yamejengwa nyumba na mabanda ya biashara.wakati nakaribia kituoni,nakutana na jamaa yangu mmoja akiwa anatoka mjini. Tunasalimiana, namuuliza "vipi hujapata tu?"ananijibu"ah,mie naona sasa niende mkoa tu,huu mji wenu umenishinda,watu wanapeana kazi kiukoo bwana!". Namtazama usoni, ingawa anaongea kwa utani,lakini anaonekana kumaanisha anachokiongea. Namuonea huruma jamaa huyu. Ana miaka miwili amemaliza UDSM shahada ya kwanza na bado anatafuta kazi!Tunaagana,naondoka.
Njiani nakutana na foleni kubwa ya magari isiyotembea, kuna ujenzi unaendelea na hivyo gari zote zinatumia njia moja.Wamekutana madereva wabishi,kila mtu anataka kuwa wa kwanza kupita,wamezibiana njia gari haziendi.Nafika kituoni nakuta hamna daladala maana gari zote zipo pale kwenye foleni isiyotembea! Ni sie tunaotambua umuhimu wa mazoezi ndio bado tunadiriki kupanda daladala kutafuta viwanja!wengi walishaacha tayari.
Siku hizi wakazi wa dsm wanafanya safari muhimu saaana tu,kama vile kwenda ofisini,hospitali,kununua mahitaji basi!Kwa nini,hali ni mbaya.Dsm hii ya leo sio ile ya mwaka 1986 wakati napanda UDA kwenda shule.Hii ni DSM nyingine kabisa! Joto kali na hili la mwaka huu hasa kuanzia mwezi October sijawahi kuliona kwa muda mrefu sana. Yaani ikishafika saa saba mchana unatamani tu jioni ifike uondokane na jehanam hii ya joto kali! Hatujaona mvua mwaka huu za maana. Tunasikia tu kutoka mikoani. Hali ya maisha ni juu.Hicho kilichopo watu hupigania hicho hicho na ndio sababu hupeana kwa kujuana.
Usipokuwa na mtandao utaiona dar chungu kama ndugu yangu huyu.Hali ya usafiri ni mbaya,miundombinu mingi imefumuliwa kwa ajili ya ukarabati,na hivyo dar ya sasa hutakiwi kuwa na haraka kabisa! Maadili ya jamii iliyopo yameporomoka vibaya. Hakuna upendo ule wa zamani. Kuna maeneo ukiibiwa utaita mwizii na watu watakutazama tu kama vile hawakusikii, huduma za kijamii ndio usiseme. Kila mahali foleni si hospitali,si maofisini. Sina haja ya kuzungumzia maji na umeme.Sina haja ya kuzungumzia kodi za nyumba! Mnaelewa vizuri sana balaa lake hapa dar.
Nawatazama watoto wetu wakigombania daladala kwenda shule,najiuliza ni mambo mangapi wanakutana nayo on the way to school and back home?!
Naikumbuka Dar ile ya mwaka 86 wakati nikiwa nyumbani Upanga,nikiwa na marafiki zangu tunacheza mpira hapo nje ya nyumba,Mzee anatunyamazisha ili asikie tangazo la kifo cha Samora Machel,halafu naitazama dar hii ya sasa,najiuliza,hivi hii bado ni bandari ya salama kweli?