Hali ngumu ya maisha kumng'oa JK Jumapili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali ngumu ya maisha kumng'oa JK Jumapili

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Oct 27, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hali ngumu ya maisha kwa Watanzania wengi kunatajwa kuwa ndiyo sababu kubwa ya msingi ya kumn'goa JK Jumapili ijayo.

  Kwa mfano tu -- kama alivyosema Dr Slaa jana kwamba zaidi ya nusu ya Watz waliokuwa wanakunywa chai mwaka 2005, sasa hivi hawanywi chai kwa kushindwa kumudu bei ya sukari.

  Hali kadhalika bei za mababati na saruji zitachangia sana kumpa Dr wa ukweli kura za kuingia Ikulu.
   
 2. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,319
  Likes Received: 840
  Trophy Points: 280
  Hasira za watz iko zaidi kwenye hali ngumu,serikali kushindwa kulinda fedha za umma, mafisadi kuungwa mkono,ahdi za uongo, kupeana madaraka kiuswahiba zaidi,

  Chagua chadema na DR.Slaa tumaini lililorudi kwa watz.
   
 3. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Hali ngumu ya Maisha imesababishwa na watu wachache walioko madarakani kujiona wao ndo wenye haki ya kuishi vizuri tu na kwamba wengine ni wa kupigiwa honi wakae pembeni na kurushiwa matope na magari yao ya kifahari wakati wa Masika.

  We are INDEED TIRED' MUNGU TUNUSURU NA HUYU MTESI '"CCM"
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Huu ndio ukweli wa JK na CCM yake na aache mara moja kutafuta visingizio vya udini/ ukabila na akiri haraka iwezekanavyo ya kuwa uchumi umempiga chenga ya mwili akisema hivyo ataanza kurudisha imani kidogo kidogo kulikoni hivi sasa asemavyo kuwa ni udini na ukabila wakati ambapo mwaka 2005 tulipomchagua kwa nini udini na ukabila vilijificha wapi?
   
 5. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hasira zipo hasa huku vyuo vikuu, kwani tangu tuambiwe kuna salary mpya ya KCC ni Tsh 135,000/= basi kwetu imekuwa ndoto kwani huu ni mwezi wa nne hatujaona ongezeko la mshahara wala hata yale malipo yetu ya promotion au hata ongezeko la mwaka, kwa mtindo huu tumekata tamaa kabisa na utawala huu wa JK tumedharauliwa vya kutosha na kunyanyaswa nya kutosha tunahitaji mabadiliko ya kweli, kwa hio tunampa rais Slaa atayekuwa anatujali na kutupenda.Tumechoka kabisaa, hii inajidhihilisha wazi kuwa JK hakwenda shule zaidi ya kutunukiwa degree na sasa anaitwa Dr, kama angekuwa anajua uchungu na maana ya elimu nchini angewajali wanotoa elimu yaani walimu wa vyuo vikuu nk na asingesema ELIMU BURE HAIWEZEKANI.Pia najiuliuliza tangu lini nchi hii watu wakalipwa mishahara hasa hii mipya kwa mafungu? Maana wengine kama watumishi wa halmashauri wamelipwa mishahara mipya ila wengine kama watumishi wa vyuo, muhimbili nk bado kulipwa,TUMECHOKA NA HASIRA ZETU TUTAZITOA OKTOBA 31 KWA KUMCHAGUA DR SLAA.
   
 6. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Na uvivu pia tuupige vita maana wa tz tunasifa hizo starehe mbele kazi kiduchu !Piga kura yako na wewe uzaliwe upya ufanye kazi kwa bidii acha uvivu!
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mmeangalia mishahara na posho wanazolipwa watumishi wa vyombo vya DOLA? Ndugu zetu hawa wamepewa mishahara na posho nzuri sana kipindi hiki kama alivyofanyiwa Rooney wa ManU! Sasa hivi JWTZ, UwT, Police, Magereza na JKT hakuna anayepokea "take home" chini ya laki sita kwa mwezi. Wao sasa hivi wanajipanga kuhakikisha JK anaendelea kuwa Rais wa JMT kwa namna yoyote ile. Kama mliwaona jana akina IGP, DCP Kova, DCP Tossi ni muendelezo wa yale alioyatamka Lt Gen Shimbo.
  Dr Slaa ni tishio sio tu kwa WANASIASA wetu bali hata wakuu vyombo vya dola, Taasisi za serikali, Mashirika ya UMMA na walafi wengi tu wa nchi hii. Hakuna mwanya utakaoachwa awe RAIS na hasa baada kuonyesha wazi hatua anazotaka kuchukua dhidi yao.
   
 8. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Hii si kweli mimi ninaye mama yangu mdogo ni askari analalamika hata mwezi september mshahara wake alipata pungufu hakuna hata lile ongezeko la rushwa walilopewa kinyemela.Pili mama huyo mwanaye kafukuzwa shule kwa kutolipa ada ya muhula, imebidi auze mbuzi wake ndo kija akarudi.Hawajalipwa wansubiri kuihukumu CCM 31/oct. Serikali ya JK haina kitu hazina HOI
   
Loading...