Hali muhimbili sio shwali,mgomo baridi umechukua sura mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali muhimbili sio shwali,mgomo baridi umechukua sura mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mbwembwekali, Jul 21, 2012.

 1. m

  mbwembwekali Member

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 4, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Saturday ,21 July 2012 06:17
  [​IMG]


  Hali ya utoaji wa huduma katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili inaendelea kuwa mbaya siku hadi siku toka madaktari katika hospitali hiyo warudi kazini kufuatia hotuba ya vitisho kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa mwishoni mwa mwezi Juni.
  Uchunguzi uliofanywa na www.nyumbanidoctor.com umebaini kuwepo na hali mbaya kwenye vitengo vyote vya utoaji wa huduma za upasuaji usio wa dharura(Elective operation) huku ndugu wa wagonjwa na wagonjwa wakiilalamikia hali hiyo.
  Taarifa za uhakika kutoka ndani ya hospitali hiyo zinasema tokea madaktari warudi kazini kufuatia hotuba ya vitisho iliyotolewa na Rais,kumekuwepo na mgomo baridi wa madaktari na hali ya utoaji huduma imeendelea kuwa mbaya siku hadi siku tofauti na jinsi ambavyo vyombo vya habari na serikali inavyolizungumzia suala hili.
  Taarifa tulizozipata ni kwamba hali ya utoaji huduma Muhimbili ni mbaya na tayari madaktari bingwa wa hospitali hiyo wanakutana leo(jana) katika kikao chao cha dharura ili kuijadili hali hiyo,kilisema chanzo chetu kimoja cha habari ndani ya hospitali hiyo.
  Juhudi za kumpata Msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Bw Eligaeshi kwa njia ya simu ili aweze kuthibitisha taarifa hizi ziligonga mwamba baada ya kupokea simu yake na kusema kuwa yupo kwenye kikao hivyo asingeweza kuzungumzia suala hilo kwa wakati huo.
  www.nyumbanidoctor.comilifanya jitihada za kumtafuta Mwenyekiti wa madaktari bingwa Kanda ya Dar es salaam,Dr Catherine Mng`ong`o ili kuthibitisha kuwepo kwa kikao cha madaktari bingwa wa hospitali ya Muhimbili kujadili kudolola kwa utoaji huduma hospitalini hapo lakini simu yake ilita na kupokelewa na mtu mwingine ambaye alimjibu mwandishi wetu kuwa muhusika yupo anakazi anafanya kwa wakati huo.
  Tuliwasiliana pia na Dr Edwin Chitage ambaye yeye alisema kuwa amepokea taarifa za kuwepo kwa hali mbaya ya utoaji wa huduma katika vitengo karibu vyote vya Hospitali ya Muhimbili na Taasisi ya mifupa MOI,ila utoaji huduma za kinamama wanaokuja kujifungua kwa njia ya kawaida na upasuajina zinaendelea vizuri.
  Dr Edwin Chitage alisema upasuaji usio wa dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Taasisi ya Mifupa(MOI ) umekuwa ni wakusuasua kama sio kusimama kabisa na kusema kuwa kama Serikali haitachukua hali ya taadhari upo uwezekano mkubwa wa huduma hizo kusimama kabisa siku za usoni.
  Dr Chitage alisema kuwa hali hii inatokana na madaktari wengi kuwa kwenye mgomo baridi kufuatia wengi wao kurudi kazini huku kukiwa hakuna makubaliano baina ya serikali na madaktari katika madai yao ya msingi ya uboreshaji wa maslai ya madaktari na mazingira bora ya utoaji huduma kwa wagonjwa.
  Dr Chitage alisema kuwa zaidi ya madai yao ya awali pia madaktari hao bado wanataka wenzao waliosimamishwa kazi na Intern waliofutiwa usajili warudishwe kazini na kurudishiwa usajili wao ili kuweka hali ya utulivu na kurudisha moyo wa ufanyaji kazi kwa madaktari waliorudi kazini.
  Hata hivyo Dr Chitage alisema yeye binafsi na madaktari wenzake awafurahishwi kuona hali ya utoaji huduma za afya nchini zikiendelea kudolola kufuatia vitendo vya serikali kupuuza madai ya msingi ya madaktari na kisha kutumia nguvu na vitisho kuwashinikiza madaktari warudi kazini ikiwa ni pamoja na kuwasimamisha madaktari wenzao na kuwafutia baadhi ya Intern usajili wao.
  Dr Chitage alisema njia iliyotumiwa na Serikali kutatua mgogoro huu haitaweza kurudisha hali ya utoaji huduma ya afya nchini kama ilivyokuwa hapo awali badala yake alipendekeza Serikali kurudi katika meza ya mazungumzo kama njia pekee ya kufikia muafaka.
  Hata hivyo alisema tayari jitihada za kuhakikisha kuwa pande mbili zinazovutana zinarudi kwenye meza ya mazungumzo,zimeshafanyika na zipo dalili kuwa muda wowote kuanzia wiki ijayo wanaweza kukutana na Serikali kwenye meza ya mazungumzo.
  “Upo uwezekani mkubwa kuanzia wiki ijayo tukarudi kwenye meza ya mazungumzo na Waziri mkuu lakini jambo la msingi kabisa katika mazungumzo yetu ni maslai ya madaktari na mazingira bora ya utoaji wa huduma za afya kwa wagonjwa nchini”
  Hata hivyo Dr Chitage alisema suala la kusimamishwa kazi kwa baadhi ya madaktari,kufutiwa usajili kwa baadhi ya Intern na kufunguliwa kwa kesi mahakamani dhidi ya MAT na Mwenyekiti wa MAT,Dr Namala Mkopi ni matokeo ya harakati zao za kudai haki za msingi za madaktari hivyo aliwaomba madaktari wote waliokubwa na madhara hayo ya mgomo,waondoe wasiwasi katika kipindi hiki ambacho viongozi wanaendelea na juhudi mbalimbali za kuhakikisha kuwa kila kitu kinakwenda kama kilivyotarajiwa pasipo kumpoteza daktari hata mmoja.
  Dr Chitage alisema tayari uongozi wa MAT uliandika barua kwenda kwenye Baraza la Madaktari Tanganyika kupinga uwamuzi wa kuwafutia usajili wa muda Intern 319.
  Katika barua hiyo viongozi wa MAT chini ya ushauri wa mwanasheria,wamebainisha taratibu na sheria zilizokiukwa na Baraza la Madaktari Tanganyika katika kufikia uwamuzi wa kuwafutia usajili Intern.
  Hata hivyo Dr Chitage alisema kwa kuwa Baraza la Madaktari Tanganyika lina hadhi ya mahakama ya wilaya hivyo kama awatakubali kutengua uwamuzi wao huo wa kuwafutia usajili wa muda Intern,upo uwezekano wa MAT kukata rufaa katika Mahakama kuu,hata hivyo alisema kutokana na kesi nyingi kuchukua muda mrefu kumalizika,jitihada za kurudi kwenye meza ya mazungumzo zinazingatiwa ili kulitatua tatizo hili kwa haraka,inayotazamiwa na wengi.
  Alisema kuwa tayari MAT wamepata mwanasheria anayewashauri kuhusu mambo mbalimbali ya kisheria na taratibu zinazotakiwa kufuatwa katika kufikia lengo la kuhakikisha kuwa masuala yote yaliyojitokea kipindi cha mgomo yanapatiwa ufumbuzi wa haraka.
  Dr Chitage alisema leo (jana) kuanzia saa 9:00 alasiri anakikao na viongozi wenzake wa Jumuia na wale wa MAT kujadili mwenendo mzima wa madai ya msingi ya madaktari nchini na chochote kitakachokua kinaendelea tutaendelea kuwafahamisha madaktari wote nchini.
  Hata hivyo aliwataka madaktari nchini kutorudi nyuma,kuwa na umoja na kuonyesha nguvu na kiu ya kudai haki zao za msingi kama zilivyoorodheshwa kwenye madai yaliyopelekwa serikali ili waweze kushinda vita hii na kuachwa kurudishwa nyuma na vitisho vya kufukuzwa kazi,kufutiwa usajili na vingine vya kutishiwa kuuwawa kwani alisema vitisho kama hivyo lazima vitokee katika harakati zozote za kupigania haki.


   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Muhimbili ni shwali huduma zimerejea kama kawa. mainterns njaa imewakaba mitaan hawana pa kuishi baada ya kutimuliwa kwenye nyumba za serikali, wanakopa hadi vocha za simu. na kwa taarifa yako, wapo walioandika barua za kuomba msamaha na kutaja waliokuwa wakiwaburuza.
   
 3. Codon

  Codon JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2012
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tuwe macho nahili,Tuache mambo yakisiasa hapa!Watanzania wanaumia,watu wenye fikra zamasaburi wanatoa kauli zaajabuajabu!
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Ujinga unawaumiza watanzania, walipaswa kama nalivyowashauri hapo awal, wawaunge mkono madaktari, wakaangukia kuiunga mkono serikatili, sasa leo wameshavunjia miguu kwa ajali za bodaboda wanawataka wale waliowapinga kwenye harakati zao eti wawatibu kwa moyo mkunjufu 100%(sukari yenye thamani ya 3000 kwa kilo haiwezi kununuliwa kwa nusu ya thamani yake!!!) huduma mnazopata kwa sasa ndio thamani ya mishahara wanayolipwa madaktari. WATANZANIA msiwalaum madaktari. Hata kwa hii huduma ilinganayo na thamani ya mishahara yao NAWAUNGA MKONO MADAKTARI. Serikali ilipie thamani halisi ya udaktari ndipo tudai huduma stahiki.
   
 5. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  hakuna intern aliyelazimishwa kugoma, wote waligoma kwa hiari..mambo si rahisi kama kuandika barua na kurudishwa kazini..maana ya kuandika barua ni kukubali umekosa, kuwa tayari kupata adhabu yeyote, kuahidi kutofanya mgomo tena hata kama hali ni mbaya zaidi ya sasa...na ni kweli MNH na MOI hali si nzuri!!
   
 6. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  wapenda migomo utawatambua kwa matendo yao
   
 7. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,278
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Endelea kujidanganya,peleka mgojwa wako pale ndo utaelewa kinachoendelea
   
 8. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
   
 9. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mi naona muhimbili iwe privatised maana serikali imeshindwa kuiendesha
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  napenda kufaham,,,,maelezo unayoyatoa ni kama msemaji wa MUHAS,MOI,MNH au wizara ya afya,au msemaj wa MAT
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Stay tune,bajet ya wizara ya afya itakaposomwa WABUNGE WATAZUIWA KUJADILI SUALA LA MADAKTARI,...................
   
 12. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  hali shwari hayo ni maneno ya kujifariji. hali ya kurejea kwa huduma baada ulimboka kuondoka ni dalili kwamba alikuwa anawachochea madaktari kugoma. hali ni nzuri ikilinganishwa na enzi za uongozi wa ulimboka. kama mgomo usingekuwa wa ulimboka madakari wasingemsaliti kipindi hiki akiwa anapata tiba nje ya nchi
   
 13. Small Boy

  Small Boy Senior Member

  #13
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sio Muhimbili peke yake, hata huku Mbeya nako Mgomo baridi wanakaa canteen zaidi ya saa 4 wakipiga story then mgonjwa mmoja anahudumiwa dk 45 . kwa siku daktari anaona wastani wa wagonjwa watano tuu....
  Tunakufa jamani, serikali tusaidieni
   
 14. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #14
  Jul 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hii nayo tutaifumbia macho kama mgomo baridi wa waalimu unavyoendelea huku tukiendelea kudhurika. Sijui ni lini tutafunguka na kuyakataa mambo ya namna hii?
   
 15. k

  kimeloki JF-Expert Member

  #15
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 1,931
  Likes Received: 954
  Trophy Points: 280
  pamoja na kwamba sikubaliani na mgomo ila upo na mgomo baridi ni hatari kuliko wa wazi.
   
 16. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #16
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Napenda kuwajulisha watanzania wenzangu wenye wagonjwa na wenye magonjwa mbalimbali kwamba hospitali ya jeshi ya lugalo kwa sasa ni ya rufaa na hivyo inatoa huduma sawa na au zaidi ya muhimbili,muende lugalo kwa huduma bora.
   
 17. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #17
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna watu ni wazushi sana humu jukwaani,nadhani ndio wale wale wanaotumia vichwa kufuga nywele badala ya akili na fikira.huduma mhimbili zinaendelea kama kawaida na hakuna mgomo.kinachoendelea kwa sasa on other side of the coin ni juhudi za serikali kuendelea na mazungumzo na madaktari ili kumalizia makubaliano ya madai yaliyosalia.hii imekuja baada ya madaktari kuiomba serikali kufanya hivyo badala ya kuchukua hatua kali za kisheria mfano kufutilia mbali usajili wa interns na kufukuza kazi baadhi ya doctors.
   
 18. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #18
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata hivyo huduma zimeboreshwa maradufu katika hospitali za temeke,mwananyamala na amana hivyo si lazima kwenda mhimbili.
   
 19. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #19
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hospitali za binafsi ambazo ni ccbrt,tmj,hindu mandal,regency na aga khan pia zinapokea wagonjwa kwa masharti nafuu ya gharama kama ilivyo hospitali za umma.tusisite kwenda huko kwa wale wanapenda kufanya hivyo.
   
 20. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #20
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  muuaji mkubwa weee,lione lilivo na roho mbaya,si ufe tu?
   
Loading...