Hali mbaya ya Njaa nchini: Mifugo inakufa, Mvua hakuna na Viongozi wanaogopa kusema!

Waterloo

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
25,360
38,869
Habari za muda Wadau,

Jana nilikuwa nafuatilia taarifa ya Habari Mkoani morogoro nilichokiona kwakweli hali si shwari.

Mifugo inaanguka kwa kukosa chakula, hali ya wakulima ni mbaya kuliko maelezo, nimejaribu kufuatilia Mikoa ya Tabora, Shinyanga , Dodoma , Singida , Manyara na Kilimanjaro mpaka sasa hakuna mvua.

Viongozi wa maeneo husika sijawasikia wakitoa tamko lolote na hali ya chakula ni mbaya sana katika maeneo hayo kuna njaa ya kutisha si kwa mkulima wala mfugaji.

Nilichokiona ni kwamba viongozi wanaogopa kusema kwamba kuna njaa katika maeneo yao kwa sababu Agizo lilishatolewa na Mh. Rais kwamba hakuna chakula cha misaada.

Sasa nilikuwa nashauri serikali ijaribu kufuatilia hali si shwari maeneo mengi nchini watu wanakufa kwa njaa Viongozi wanaogopa kusema.
 
Ukame unapoingia siyo kwamba Njaa inaanza wakati huohuo, athari zake ni baada ya msimu kuisha,
Mkuu sasa hivi gunia la mahindi la kg 100 ni Tsh. 130,000 kwa Dar je tutafika? Na mikoani hakuna mvua.
 
Habari za muda Wadau,
Jana nilikuwa nafuatilia taarifa ya Habari Mkoani morogoro nilichokiona kwakweli hali si shwari.
Mifugo inaanguka kwa kukosa chakula, hali ya wakulima ni mbaya kuliko maelezo, nimejaribu kufuatilia Mikoa ya Tabora, Shinyanga , Dodoma , Singida , Manyara na Kilimanjaro mpaka sasa hakuna mvua.

Viongozi wa maeneo husika sijawasikia wakitoa tamko lolote na hali ya chakula ni mbaya sana katika maeneo hayo kuna njaa ya kutisha si kwa mkulima wala mfugaji.
Nilichokiona ni kwamba viongozi wanaogopa kusema kwamba kuna njaa katika maeneo yao kwa sababu Agizo lilishatolewa na Mh.Rais kwamba hakuna chakula cha misaada.
Sasa nilikuwa nashauri serikali ijaribu kufuatilia hali si shwari maeneo mengi nchini watu wanakufa kwa njaa Viongozi wanaogopa kusema.
wanaopa kutumbuliwa na kwa taarifa ushawaweka tumbo joto
 
Naomba viongozi wa maeneo husika kabla hawajatangaza kuwa kuna NJAA wawasiliane na Dr. Malecela na Muhandisi Mramba ili wapate uzoefu kabla ya kutungaza njaa kwenye maeneo yao.
 
Hivi acheni UPUUUZI.....hivi hii hali ni mara ya kwanza kutokea nchini mwetu??????Aiseeh tatzo kila kitu mnageuza ni mambo ya kisiasa......
Usitulaumu ndiyo serikali yako ilivyo siasa imetawala kupindukia ukweli unawekwa pembeni ili unafiki utawale
 
Habari za muda Wadau,
Jana nilikuwa nafuatilia taarifa ya Habari Mkoani morogoro nilichokiona kwakweli hali si shwari.
Mifugo inaanguka kwa kukosa chakula, hali ya wakulima ni mbaya kuliko maelezo, nimejaribu kufuatilia Mikoa ya Tabora, Shinyanga , Dodoma , Singida , Manyara na Kilimanjaro mpaka sasa hakuna mvua.

Viongozi wa maeneo husika sijawasikia wakitoa tamko lolote na hali ya chakula ni mbaya sana katika maeneo hayo kuna njaa ya kutisha si kwa mkulima wala mfugaji.
Nilichokiona ni kwamba viongozi wanaogopa kusema kwamba kuna njaa katika maeneo yao kwa sababu Agizo lilishatolewa na Mh.Rais kwamba hakuna chakula cha misaada.
Sasa nilikuwa nashauri serikali ijaribu kufuatilia hali si shwari maeneo mengi nchini watu wanakufa kwa njaa Viongozi wanaogopa kusema.
mvua inanyesha japo sio kubwa kivile!
Kule simiyu,katika wilaya zote mvua inanyesha!na hata jana kule meatu ilinyesha wakati najiandaa kwenda bukoba!
Mvua zinanyesha!nenda singida,dodoma,ila sio kubwa kivile!
Njaa siyo kukosa mahindi kuna Mchele Sumbawanga na Mpanda Mchele ni 1250/= kwa kilo hivi sasa Viazi na Mihogo ni mingi.
mkuu,kule meatu kabla ya kuondoka bei ya kilo moja ikirandaranda kati ya 1200 mpaka 1400!
Na mvua inanyesha japo sio kubwa!
 
Umesema umefuatilia hali si shwari,mwisho umemaliza kwa kusema watu wengi wanakufa kwa njaa viongozi wanaogopa kusema.
Hebu leta ushahidi ni sehemu gani kwenye jamhuri hii kuna watu wamekufa njaa?
Mkuu mimi siyo mwanasiasa. Nachokiongea hapa ndio uhalisia watu wanalazwa mahospitalini unadhani ni malaria kumbe mtu kafa kwa njaa. Mifugo haitazamiki imekonda kwa kukosa chakula. Sikulazimishi uamini mkuu unaweza kuacha kama ilivyo.
 
Da yaani megusia mada nyeti mno huku Dom vjjni hali c yakuzungumzia na nikweli viongozi wa maeneo Hucka kimya kama wamemeza tambala.Leo huku kjjn kwetu walikua wanagawa mbegu za mtama robo kilo kwa kila kaya ambayo shamba athiriwa na ndege
 
Viongozi wanaogopa kutumbuliwa,maana yake njaa ikisikika eneo lako hicho kinakuwa ni kigezo cha kukufanya utumbuliwe.
 
mvua inanyesha japo sio kubwa kivile!
Kule simiyu,katika wilaya zote mvua inanyesha!na hata jana kule meatu ilinyesha wakati najiandaa kwenda bukoba!
Mvua zinanyesha!nenda singida,dodoma,ila sio kubwa kivile!

mkuu,kule meatu kabla ya kuondoka bei ya kilo moja ikirandaranda kati ya 1200 mpaka 1400!
Na mvua inanyesha japo sio kubwa!
Mkuu mvua inanyesha ndio lakini siyo mvua ya kukidhi uzalishaji wa mazao. Kiukweli ni rasha rasha wakati kipindi kama hiki tulizoea mvua za msimu sasa mkuu huoni hiyo hali ni mbaya? Na hata hizo mvua za rasha rasha siyo sehemu zote. Kwakweli serikali nisaidie chakula watu wengi watapoteza maisha.
 
Hivi acheni UPUUUZI.....hivi hii hali ni mara ya kwanza kutokea nchini mwetu??????Aiseeh tatzo kila kitu mnageuza ni mambo ya kisiasa......
mvua zinanyesha ila ni chache!ila najiuliza ikiamua kunyesha na watu wakavuna,hawa wasio na jema,sura zao wataziweka wapi?na ni ajenda gani nyingine watakaoipata?maana kila siku imekuwa:ukame!ukame!ukame!njaa!njaa!njaa!
 
Back
Top Bottom