Hali mbaya ya maisha wengi tunayopitia ni mapito kuelekea maendeleo ya kweli au tunapotezeana malengo na muda?

Elythrobacter

Member
Sep 29, 2020
47
94
Nina miaka kadhaa inayoniruhusu kuwa na familia, lakini pamoja na elimu yangu, sina hela ila nina deni kama la milion 14 hivi ninazodaiwa na bodi ya mikopo, hapo sijaweka zaka ambazo sijui nilitoa lini? Kiukweli moja haikai wala mbili haisimami, Maisha ni magumu, rafiki yangu mwajiriwa na mnazi wa chama tawala alinambia kuwa hali hii ya maisha ni mpito tu afu kimasihara.

Kuwa katika historia aliyosoma na inayompa ugali, inasema kuwa ili maendeleo ya kweli yatokee katika nchi ni lazima kizazi fulani wafunge mkanda kwa ajili ya kizazi kijacho. Nimekubali hoja yake lakini nani atuthibitishie kuwa hii hali kweli ni ya mpito maana kama vile inapita na umri wetu, kizazi chetu pia maleongo yetu.

Sasa najiuliza haya maswali;
Je, kama maendeleo na hali nzuri tunayoahidiwa yasipopatikana, nani aulizwe?
Je, kama miundombinu inayojengwa isipotunzwa na baada ya mda mfupi shida ikarudi palepale itakuwaje?
Nithibitishie ili siku ya uchaguzi nifanye kazi yangu vizuri.

#ability without opportunity is nothing.
 
Kivipi ili hali wengi tunalalama hali mbaya? Thibitisha
Sio kweli kwamba wengi wanalaani hali mbaya. Wengi wanafurahia huduma za afya, elimu zilivyoboreshwa. Pia wanafurahia jinsi usafiri wa abiria na mizigo ulivyorahisishwa. Upatikanaji wa maji vijijini na mijini unawapa faraja akinamama wote. Nidhamu ya utumishi wa umma imeongeza tija na kukonga nyoyo za wananchi.
Maendeleo ni hatua. Tunaendelea vizuri.
 
Ushauri wangu kwako, pambana na khari yako. Hawa wanasiasa saizi wanatafuta uhalali wa kikatiba kwa maslahi yao binafsi kwanza, pambana tafuta pesa kidhi mahitaji yako, ongeza juhudi kwenye Kutafuta Mungu atakufungulia Njia ya mafanikio
 
Soma kuhusu udikteta na ujamaa ndio utajua Kama upo kwenye right track
 
Hakuna maendeleo ya kutesa wananchi mkanda wafunge wananchi watawala wao walegeze, kuwekeza kwenye white elephant project kwa mawazo ya kijima kunaleta vipi maendeleo.
 
Maendeleo ya vitu Kama hayachochei kuinua maisha ya watu ni kuumiza watu.
 
Ushauri wangu kwako, pambana na khari yako. Hawa wanasiasa saizi wanatafuta uhalali wa kikatiba kwa maslahi yao binafsi kwanza, pambana tafuta pesa kidhi mahitaji yako, ongeza juhudi kwenye Kutafuta Mungu atakufungulia Njia ya mafanikio
Unapatia wapi Hali wanasiasa wameweka mifumo ili usitoboe uwe masikini ili utawaliwe
 
Sio kweli kwamba wengi wanalaani hali mbaya. Wengi wanafurahia huduma za afya, elimu zilivyoboreshwa. Pia wanafurahia jinsi usafiri wa abiria na mizigo ulivyorahisishwa. Upatikanaji wa maji vijijini na mijini unawapa faraja akinamama wote. Nidhamu ya utumishi wa umma imeongeza tija na kukonga nyoyo za wananchi.
Maendeleo ni hatua. Tunaendelea vizuri.
Kama kweli tunaendelea vizuri? Baada ya elimu, wahitimu wengi wanapata nini? Garama za hospitali tunazimudu tulio wengi? wanasafirisha mizigo ipi? Na kwa garama ipi? Kama maji safi na salama vichocho vinatoka wap?
 
Sio kweli kwamba wengi wanalaani hali mbaya. Wengi wanafurahia huduma za afya, elimu zilivyoboreshwa. Pia wanafurahia jinsi usafiri wa abiria na mizigo ulivyorahisishwa. Upatikanaji wa maji vijijini na mijini unawapa faraja akinamama wote. Nidhamu ya utumishi wa umma imeongeza tija na kukonga nyoyo za wananchi.
Maendeleo ni hatua. Tunaendelea vizuri.
Labda wanufaika Kama wewe, elimu Bora mbona wao hawasomeshi kwenye hizo shule. Umewahi kwenda hospitali, watumishi gani Wana nidhamu ya kazi hawa wanaoshindia mihogo ambao hawajaongezewa mishahara 5 yrs. Au kwako una TBC pekee imekupropaganda
 
Sekta binafsi imevurugwa na iko mahututi, hayo maendeleo ya baadae ni yapi? Mzunguko wa fedha ni mdogo sana huku mauzo ya bidhaa yameshuka, bidhaa nazo kama vifaa vya ujenzi, sukari bei juu.

Kuna kampuni niliziuzia nguzo 2017 nikalipwa hela yangu baada ya siku 10 huko Mafinga, Njombe. Mwaka huu jamaa zangu wamepeleka nguzo toka April hawajalipwa mpaka leo. Wana mikopo, wanadaiwa Kodi nk, umasikini umeingia kwao. Tanesco hawalipi madeni kwa wakati kama zamani.

Serikali ije na sera wezeshi kwa sekta binafsi ili ajira ziongezeke, kodi iongezeke na uchumi ukue. Siasa za kiki zitupwe kwenye bean ili hili gurudumu la maendeleo lisonge mbele.
 
Sio kweli kwamba wengi wanalaani hali mbaya. Wengi wanafurahia huduma za afya, elimu zilivyoboreshwa. Pia wanafurahia jinsi usafiri wa abiria na mizigo ulivyorahisishwa. Upatikanaji wa maji vijijini na mijini unawapa faraja akinamama wote. Nidhamu ya utumishi wa umma imeongeza tija na kukonga nyoyo za wananchi.
Maendeleo ni hatua. Tunaendelea vizuri.
Elimu gani imeboreshwa, au elimu ya kuzalisha misukule.
 
Maendeleo hayaji bila jasho kuvuja.

Nchi inaelekea good direction.
Hamna kitu hapa, Magufuli ni kimeo tu.

Hebu chukulia mfano mmoja tu wa kilimo cha mbaazi, ziliporomoka kutoka 1500 hadi 200/-!!!!!!!, baada ya jamaa kuwa harras wanunuzi. Mbaya zaidi hakuwa na mkakati, na hadi sasa hana mkakati wowote wa kuhakikisha bei inapanda ( aliwaambia wazichemshe wale kwani zina protein nyingi). Kwenye mazao mengine ni vilio vitupu.

Huyu jamaa anapuyanga tu, hana vision. Miaka 5 iliyo pita alikuwa anaimba viwanda, sasa hivi kimyaaaaa wala hazungumzii tena.
Jamani tuwe honest, huyu jamaa hafai, natudia tena hafaiiiiiii. Acheni ushabiki wa vyama tujumuike kumuondoa.
 
Watanzania wana macho. Wameona kazi nzuri inayofanywa na serikali yao. Wameamua kuwa mitano tena ni kwa Magufuli...
 
Watanzania wana macho. Wameona kazi nzuri inayofanywa na serikali yao. Wameamua kuwa mitano tena ni kwa Magufuli...
Ndiyo wameona kazi nzuri ya Magufuli ya:-
- kupandisha sukari kutoka 1800 hadi 3000/ kwa kilo
- kazi nzuri ya Magufuli kutopandisha mishahara kwa miaka 5.
- kazi nzuri ya Magufuli ya kupandisha makato ya wanufaika wa bodi ya mikopo kutoka 8% hadi 15% .
- kazi nzuri ya Magufuli kuondoa fao la kujitoa.
- kazi nzuri ya kuleta kikotoo kipya kinachopunja wastaafu.
- kazi nzuri ya magufuli kuvuruga bei za mbaazi kutoka 1500 hadi 200/-!
- kazi nzuri ya Magufuli...................................................ongeza na wewe kwani kazi zake " nzuri" ni nyingi. Na atatuvuruga kweli kweli kwa kazi zake "nzuri".
 
Back
Top Bottom