Hali Mbaya ya Mabenki: Mabenki sasa yawataka wenye viwanda kupunguza maombi ya mikopo

Serikali inasisitiza na kuhamisisisha wananchi wote wahifadhi pesa benki ili hela iingie kwenye mzunguuko wa kiuchumi wakati yenyewe imefungia hela zake BOT, kama sababu ni Serikali kuepuka kujikopesha hela zake kutoka kwenye mabenki za kibiashara basi iziweke kwenye fixed deposit za mabenki ya kibiashara kwa faida, na iache kukopa kwenye mabenki ya biashara badala yake ikope kwenye mabenki na taasisi za kifedha za nje ya nchi, na iache kuuza bonds, tresurery bills, n.k. kwa benki za kibiashara za ndani ya nchi

Hapa umenena mkuu, kulikuwa hamna impact assessment au pengine sizonje aliogopwa ktk kupewa ushauri.

Nia Yake ilikuwa Ni njema kabisa Ila suluhisho alilofanya amekosea Kwa kutokujua athari zake. Lakini sishangai kwasababu alisha Sema kuwa "tutalimia meno", kuna watu alikuwa ana walenga pengine lakini hakujua kuwa ataathiri hadi ambao hawakuwa walengwa
 
Sasa kuna tatizo gani serikali kuhifadhi pesa yake.Niambie ni nchi gani serikali inaweka pesa zake katika benki za biashara.
Kwa Magufuli wote waliozoea vya kunyonga lazima walambe mchanga.
Hizo benki Warekebishe tu cash flows zao ikibidi hata kukopa benki za nje
tutajie hizo nchi na level yake kiuchumi,kuna nchi zina Bill Gates kadhaa,utalinganisha na hapa?

hapa uchumi wa nchi lazima serikali iweke mkono(mojawapo ni kuboost uwezo wa benki kukopesha)

wenzetu wametoka huko,japo kidogo.

makampuni ya madini ambayo yangeubeba uchumi na benki zetu yana akaunti wapi?yanahifadhi pesa wapi?makampuni ya gesi je?

endless list,na nani aliyaruhusu kutohifadhi benki hapa Tanzania?
 
Bank zingine zitakufa kwa kujitakia na wengine wataambulia kukuta mti tu waliotolea mkopo kama shamba.

Wanaendesha biashara kwa 10% I was expecting that to happen.
 
Tumieni Akili basi,

Kwani Bank zilianzishwa ili zitegemee pesa za Serikali kufanyia shughuli zake?

Yaan uanzishe Bank yako halafu utegemee Taasisi za Serikali zi-deposit fedha zake kwenye account ya Bank yako halafu wewe uzitumie hizo hizo pesa kukopesha hata serikali yenyewe! hii haikubaliki.

Bank zijifunze baada ya huu mpito kupita, wasiwe wanategemea kufanya biashara kwa fedha za serikali...
Kuna kiwango cha pesa za kuanzisha Bank, na kiwango cha pesa za kuweka kama dhamana katika Bank kuu ili kulinda amana za wateja, sasa kwa nini Bank ziyumbe? hii ina maana kuwa Bank zilikopesha sana makampuni na taasisi mbalimbali na viwanda mpaka ile mitaji yao ikapungua to the maximum na madeni walikuwa hawakusanyi kabisa, sasa JPM kawabana.
Ngoja niaze kutumia akiri na wewe,
Ma bank hayana shida na hela za serukali lakini uwepo wa hela za serikali ni muhimu kwenye mzunguko wa pesa!!!
Kama viwanda vinashindwa kukopeshwa, unadhani serikali itapata wapi kodi nyingi?
Lakini pia hizo hela zi kikaa bank kuu zina zalisha ni nini?
Kwenye mambo ya msingi kama haya usijifanye unaakiri nyingi kuliko wezako wote, pia punguza mapenzi ya liyo pitiliza
 
Tumieni Akili basi,

Kwani Bank zilianzishwa ili zitegemee pesa za Serikali kufanyia shughuli zake?

Yaan uanzishe Bank yako halafu utegemee Taasisi za Serikali zi-deposit fedha zake kwenye account ya Bank yako halafu wewe uzitumie hizo hizo pesa kukopesha hata serikali yenyewe! hii haikubaliki.

Bank zijifunze baada ya huu mpito kupita, wasiwe wanategemea kufanya biashara kwa fedha za serikali...
Kuna kiwango cha pesa za kuanzisha Bank, na kiwango cha pesa za kuweka kama dhamana katika Bank kuu ili kulinda amana za wateja, sasa kwa nini Bank ziyumbe? hii ina maana kuwa Bank zilikopesha sana makampuni na taasisi mbalimbali na viwanda mpaka ile mitaji yao ikapungua to the maximum na madeni walikuwa hawakusanyi kabisa, sasa JPM kawabana.
Wewe utakuwa ndiye usiyetumia hiyo unayowataka wenzako watumie, kuna mahali banks zimelalamika na kuitaja serikali kuwa ndio chanzo cha wao kuwa na liquidity challenge?
 
Unaiga tu mradi kuiga badala ya kuangalia facts.
Nimekuuliza nitajie nchi moja tu duniani inayoweka hela zake kwenye benki za biashara.
Hiyo biashara ungepewa hata wewe,usingeshindwa
Mfano benki J inakusanya bilioni 200,za serikali,inakaa nazo tu bila ya riba kwa siku 40 mpaka 60,humu wanazizungusha tu
Upewe bilioni 200 ukae nayo mwezi tu FD yake inakutoa maisha yako yote.
Kuna ubaya gani serikali kuhifadhi pesa yake benki kuu?
Yaani unaomba leseni ya kuendesha benki kwa kutegemea pesa ya serikali?
Tulieni tu,mwanzo mtaumia mageuzi yoyote yana maumivu mwanzo,
 
Wewe utakuwa ndiye usiyetumia hiyo unayowataka wenzako watumie, kuna mahali banks zimelalamika na kuitaja serikali kuwa ndio chanzo cha wao kuwa na liquidity challenge?
Yaaani watu wengine mkuu wanajifanya wanaakiri nyingi kumbe wana mapenzi yaliyo pitiliza
 
Nimekuuliza nitajie nchi moja tu duniani inayoweka hela zake kwenye benki za biashara.
Hiyo biashara ungepewa hata wewe,usingeshindwa
Mfano benki J inakusanya bilioni 200,za serikali,inakaa nazo tu bila ya riba kwa siku 40 mpaka 60,humu wanazizungusha tu
Upewe bilioni 200 ukae nayo mwezi tu FD yake inakutoa maisha yako yote.
Kuna ubaya gani serikali kuhifadhi pesa yake benki kuu?
Yaani unaomba leseni ya kuendesha benki kwa kutegemea pesa ya serikali?
Tulieni tu,mwanzo mtaumia mageuzi yoyote yana maumivu mwanzo,
Nini kimeifanya serikali isianze kutoza riba? ukikuta nyani wanakula mahindi shambani mwako utafyeka mahindi au utatafuta namna ya kudhibiti nyani?
 
tutajie hizo nchi na level yake kiuchumi,kuna nchi zina Bill Gates kadhaa,utalinganisha na hapa?

hapa uchumi wa nchi lazima serikali iweke mkono(mojawapo ni kuboost uwezo wa benki kukopesha)

wenzetu wametoka huko,japo kidogo.

makampuni ya madini ambayo yangeubeba uchumi na benki zetu yana akaunti wapi?yanahifadhi pesa wapi?makampuni ya gesi je?

endless list,na nani aliyaruhusu kutohifadhi benki hapa Tanzania?
Huwezi kutegemea kukopesha kwa kutumia hela ya serikali
Benki inakopesha kwa kutegemea amana za wateja wakiwemo wafanyabiashara wakubwa.
Kama benki hazina vitengo madhubuti vya masoko vya kutengeneza mipango itakayowavutia wateja kuweka pesa zitakufa tu.
Na kwa kadhia hii huwezi kusikia benki kama CITY,BARCLAYS NA STANBIC wanalia lia kama watoto wadogo kwa sababu hawakuzoea kufanya biashara kwa kutumia mihela ya serikali
 
Swali la kizushi "mwenyekiti wa ccm taifa huwa anasoma gazeti la the citizen?" Ila kama aliweza kumeza kikombe cha babu loliondo na hizi taarifa za gazeti la the citezen ameze pia.
 
Huku tunakoelekea, itafikia siku tutaamkiana shikamoo wakubwa kwa wadogo. Hivi, ukiweka fedha zako benki, siku ya kuzitoa unakuwa umepata faida au bank charges?
 
Tumieni Akili basi,

Kwani Bank zilianzishwa ili zitegemee pesa za Serikali kufanyia shughuli zake?

Yaan uanzishe Bank yako halafu utegemee Taasisi za Serikali zi-deposit fedha zake kwenye account ya Bank yako halafu wewe uzitumie hizo hizo pesa kukopesha hata serikali yenyewe! hii haikubaliki.

Bank zijifunze baada ya huu mpito kupita, wasiwe wanategemea kufanya biashara kwa fedha za serikali...
Kuna kiwango cha pesa za kuanzisha Bank, na kiwango cha pesa za kuweka kama dhamana katika Bank kuu ili kulinda amana za wateja, sasa kwa nini Bank ziyumbe? hii ina maana kuwa Bank zilikopesha sana makampuni na taasisi mbalimbali na viwanda mpaka ile mitaji yao ikapungua to the maximum na madeni walikuwa hawakusanyi kabisa, sasa JPM kawabana.
Tafuna noti yoyote uniambie imeandikwa ni ya nani vile!!!
Serikali ikiziatamia hela itatotoa majambazi.
 
Chanzo:The citizen

Kama mtu alijua anakomoa mabenki,basi ajue alikuwa anajihujumu mwenyewe na sera zake na ajiandae kupokea matokeo yake.

Na haya maneno ungemalizia kuandika tu kwa kizungu maana umeamua kuandika hivyo umeshindwa kututafasiria sisi....!!
Halafu kwenye lawama Ndo unaandika kwa kiswahili sisi tutajuaje sasa....!!
 
Back
Top Bottom