Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 sehemu kubwa ya wabunge walichukua mikopo mikubwa ili kulipia gharama kubwa walizotumia wakati wa uchaguzi mkuu.
Wengi walitegemea watakapoingia bungeni watapata pesa kutoka kwenye makamati ya bunge na vyanzo vya kutumia wadhifa wa ubunge.
Miaka mingi wakati wa bajeti za serikali huwa kuna matajiri huwa wako pale Dodoma ku lobby bajeti za serikali ili kufanikisha tenda zipite kwa manufaa yao. Na mawaziri wengi huwa wanakuja na mafungu ya pesa kutoa illi bajeti zao zisikwamwishwe.
Serikali ya awamu ya tano na sera ya kubana matumizi imewaathiri kiasi kikubwa wabunge hawa kiasi ambacho badala ya kuwakilisha ama kujadili kwa undani bajeti ya mwaka 2017/18 ni malumbano yasio na tija kwa watu wanaowakilisha.
Ni wakati muhimu kwa wabunge kubadilika na kuacha kutumiwa na watu wasioitakia Tanzania mema serikali ya awamu ya tano itahukumiwa na watanzania mwaka 2020.
Naomba serikali iangalie suala la mbunge anapomaliza muda wake halafu analipwa milioni 200 kiinua mgongo wakati mbunge huyo amehudumia watu kwa miaka 5, kuna watumishi serikali wanastaafu wakiwa wametumikia serikali kwa miaka 30 hawalipwi hata nusu ya hiyo pesa.
Tanzania yenye amani ni kitu bora zaidi.